Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi

Mwongozo wa jinsi ya kutumia Uber

Iwe unafanya shughuli mjini au unazuru mji wa mbali, safiri kwa urahisi. Pata maelezo zaidi kuhusu kusafiri kwa kutumia programu ya Uber.

Jinsi ya kutumia App ya Uber

Fungua akaunti

All you need is an email address and phone number. You can request a ride from your browser or from the Uber app. To download the app, go to the App Store or Google Play.

Weka mahali unakoenda

Fungua App na uweke mahali unakoenda katika kisanduku cha Unaenda wapi. Gonga ili uthibitishe mahali utakakochukuliwa kisha ugongeThibitisha tena ili ukutanishwe na dereva aliye karibu nawe.

Kutana na dereva wako

Unaweza kufuatilia muda atakaowasili kwenye ramani. Akiwa karibu, msubiri kwenye eneo la kuchukuliwa.

Kagua usafiri wako

Kila unaposafiri kwa Uber, tafadhali hakikisha unaabiri gari lililo na dereva anayefaa kwa kulinganisha maelezo ya namba pleti, aina na muundo wa gari na picha ya dereva na maelezo yaliyo kwenye App yako.

Unaweza tu kuitisha usafiri wa Uber kwenye App, kwa hivyo usiwahi kuabiri gari au kubebwa na dereva ambaye ha'lingani na maelezo yaliyo kwenye App.

Keti na utulie

Ni rahisi kulipa ukiwasili. Una chaguo mbalimbali, kulingana na eneo lako. Lipa kwa pesa taslimu au kwa kutumia njia ya malipo kama vile kadi ya benki au salio la Uber Cash.

Kadiria ubora wa safari yako

Hebu tujulishe jinsi safari yako ilivyokuwa. Pia unaweza kumpa dereva wako pongezi au uongeze kiinua mgongo katika App yako.

Safari rahisi kutoka mwanzo hadi mwisho

Boresha hali ya kuchukuliwa

Ukiitisha usafiri, programu itakupendekezea kiotomatiki mahali mwafaka pa kukutana na dereva wako. Ili ubadilishe mahali ulipo, andika eneo jipya au buruta kipini cha mahali kwenye ramani ndani ya mduara wa rangi ya kijivu.

Mfahamu dereva wako

Angalia Wasifu wa Madereva katika App ili uone vidokezo vya kuvutia kuhusu dereva wako, ikijumuisha ukadiriaji na pongezi.

Ukadiriaji na bakshishi

Tusaidie kuboresha huduma za usafiri kwa kutoa ukadiriaji wa safari. Pia unaweza kumpa dereva kiinua mgongo ikiwa amekuhudumia vizuri.

Unapata utulivu wa mawazo kila unaposafiri

Tunaupa kipaumbele usalama wako, kupitia hatua kama vile uchunguzi wa madereva, bima, vipengele vya programu vinavyokuwezesha kufuatilia safari yako na kusalia mtandaoni.

Njia ambazo watu hutumia kusafiri kote ulimwenguni

App ya Uber inakupa uwezo wa kufika unakotaka kwenda kwa kutumia aina mbalimbali za usafiri katika zaidi ya miji 10,000.

Tunakuletea Uber Lite

Pata safari zilezile za kuaminika kama kwenye programu mpya. Uber Lite hutumika katika simu yoyote ya Android na inaokoa nafasi na data. Isitoshe, Uber Lite ni rahisi kutumia na imeundwa kuyafaa maeneo yenye intaneti hafifu.

Nenda mbali zaidi kwa kutumia Lime

Je, unajua kwamba unaweza kukodisha baiskeli za umeme na skuta za Lime katika baadhi ya miji kwa kutumia App ya Uber? Fuata maelekezo kwenye programu ili upate baiskeli na skuta zilizo karibu nawe.

Maswali ambayo wasafiri wanauliza sana

  • Unaweza kuratibisha safari siku 30 kabla ya kusafiri. Fungua App kisha ubonyeze aikoni ya gari na saa karibu na kisanduku cha Unaenda wapi?.

  • Fungua App kisha ugonge kisanduku cha Unaenda wapi?. Ukibonyeza, utafungua chaguo la kusogeza chini la Badilisha Msafiri. Gonga kipengele hiki kisha uchague rafiki yako. Watapokea ujumbe ulio na maelezo ya safari, ikijumuisha muundo wa gari na namba pleti, jina la dereva na maelezo ya mawasiliano, na Muda Atakaowasili.

  • Nauli hukadiriwa kulingana na saa na umbali. Nauli hizi zinaweza kubadilika, unaweza kulipia ada za barabara, ada ya kughairi safari na ya muda wa kusubiri, panapohitajika, na ada za kuweka nafasi.

    Mamia ya pointi za data zitatumika kukokotoa nauli utakayolipa. Kiasi cha nauli hutegemea muda uliotumika katika safari, umbali kutoka kituo cha kwanza hadi mahali unakokwenda, wakati, barabara uliyofuata na wingi wa wasafiri. Kiasi cha nauli pia hutegemea ada za barabara, kodi, ada za ziada na ada nyinginezo.

  • Ukadiriaji hufanywa kwa madereva na wasafiri. Baadhi ya maoni tunayopokea mara nyingi kutoka kwa madereva ni kwamba wanapenda wasafiri wakiwa na mjadala wa kuchangamsha, walitumie vizuri gari na mali yao, ikijumuisha kufunga mlango wa gari bila kuugongesha wanapoingia au kushuka, na wasiwasumbue wanapoendesha gari. Angalia Mwongozo wa Jumuiya yetu ili upate ushauri zaidi.

  • Unaweza kuongeza hadi vituo 2 kabla au wakati wa safari yako. Bonyeza kipengele cha + karibu na kisanduku cha Unaenda wapi? ili uweke anwani yako. Nauli yako inaweza kurekebishwa kulingana na muda na umbali wa mahali unakoenda.

*Kipengele hiki hakipatikani kwenye App ya Uber Lite. Maelezo yaliyotolewa kwenye ukurasa wa tovuti hii yatatumiwa kutoa maelezo pekee na haiwezi kutumiwa katika nchi, eneo au mji wako. Inaweza kubadilika na huenda tukaibadilisha bila kukuarifu.