Mwongozo wa mtumiaji wa mnyama wa huduma
Kutumia teknolojia ili kuwezesha ufikiaji wa huduma za usafiri zinazotegemeka na zinazoweza kufikiwa kwa ajili ya wasafiri ambao ni vipofu au wenye uoni hafifu.
Mwongozo wa kupata Sera ya Uber ya Mnyama wa Huduma
Kwenye kompyuta
Kituo cha Usaidizi cha Ufikiaji
- Bonyeza kiungo hiki kwa Sera ya Huduma ya Wanyama
Kwenye programu ya Uber
Kituo cha Msaada wa Ufikiaji
- Bofya kitufe cha menyu kwenye kona ya juu kushoto.
- Chagua Msaada.
- Telezesha chini hadi sehemu ya Ufikiaji.
- Chagua Kusafiri pamoja na Wanyama wa Huduma, kisha Marekani Sera ya Mnyama wa Huduma.
Kuripoti malalamiko kuhusu kunyimwa huduma ya mnyama wa huduma
Timu yetu mahususi ya usaidizi hushughulikia malalamiko yote yanayohusu wanyama wa huduma ili kuhakikisha kuwa matukio yanachunguzwa, kuandikwa na kutatuliwa ifaavyo. Ripoti hizi zinaweza kuandikishwa kwenye Kituo chetu cha Msaada wa Ufikiaji.
Kuna njia kadhaa za kuripoti malalamiko ya kunyimwa huduma ya mnyama wa huduma:
Kwenye kompyuta kwa ajili ya watumiaji walio na akaunti za Uber
Kituo cha Msaada wa Ufikiaji
- Ingia kwenye help.uber.com ukitumia maelezo yako ya kuingia kwenye akaunti ya Uber.
- Telezesha chini kisha ubofye Ufikiaji.
- Tafuta "sera ya mnyama wa huduma" kisha uchague Sera ya Mnyama wa Huduma ya Marekani.
- Telezesha chini hadi sehemu ya Ninataka kuripoti tatizo la mnyama wa huduma.
Safari zilizokamilika
- Ingia kwenyehelp.uber.com ukitumia maelezo yako ya kuingia kwenye akaunti ya Uber.
- Kwenye ukurasa wa Matatizo ya Safari na Urejeshaji wa Fedha, chagua safari husika ukitumia menyu kunjuzi ya historia ya safari kwenye ramani.
- Bofya Zaidi chini ya maelezo ya safari kwa ajili ya safari iliyochaguliwa.
- Chagua Ninataka kuripoti tatizo la mnyama wa huduma katika sehemu ya Matatizo ya Jumla.
Kwenye kompyuta kwa ajili ya watumiaji wasio na akaunti za Uber
Tafuta fomu ya malalamiko kuhusu mnyama wa huduma hapa.
Kwenye programu ya Uber
Kituo cha Msaada wa Ufikiaji
- Bofya menyu kwenye kona ya juu kushoto.
- Chagua Msaada.
- Kisha uchague Ufikiaji.
- Bofya Ninataka kuripoti tatizo la mnyama wa huduma.
Safari zilizokamilika
- Bofya menyu kwenye kona ya juu kushoto.
- Chagua Msaada.
- Kisha uchague Tazama Matatizo Yote.
- Bofya Ninataka kuripoti tatizo ya mnyama wa huduma.
By Phone
Call +1 (833) 715-8237 to reach Uber's Safety Incident reporting line. This phone number connects directly to a team of safety agents trained in the unique issues facing riders traveling with service animals.
Ada na kurejesha fedha
Tozo ya kughairi
Ikiwa utatozwa ada ya kughairi kwa sababu ya kunyimwa huduma, malipo haya yatarejeshwa na timu yetu ya usaidizi ikiwa utatoa taarifa Uber kuhusu suala hilo. Tafadhali kumbuka kwamba fedha zilizorejeshwa zinaweza kuchukua hadi siku 5 za kazi hadi zikufikie kwenye mbinu yako ya malipo.
Sera ya Mnyama wa Huduma
Sheria za jimbo na za serikali kuu zinapiga marufuku madereva wanaotumia programu ya Dereva wa Uber kuwanyima huduma au kuwabagua wasafiri walio na wanyama wa huduma. Kama ilivyoelezwa kwenye Mwongozo wa Jumuiya wa Uber na Sera ya Mnyama wa Huduma, madereva wanaohusika katika tabia ya ubaguzi kwa kukiuka jukumu hili la kisheria watazuiwa kutumia programu ya Dereva.
Je, una maswali yoyote?
Ili kupata taarifa zaidi kuhusu akaunti yako ya Uber, vinjari maswali yanayoulizwa mara nyingi au utoe maoni kuhusu safari yako ya hivi karibuni.
Ikiwa ungependa kupata maelezo zaidi kuhusu kusafirisha wasafiri wenye ulemavu, angalia nyenzo hizi kwa ajili ya madereva.
*Haitumiki nchini Ufaransa.
Kuhusu