Jipatie Maili za Flying Blue ukitumia Uber
Uber inashirikiana na Flying Blue, mpango wa uaminifu wa Air France-KLM Group, ili kuwapa wasafiri fursa ya kupata Flying Blue Miles kupitia safari za Uber.
Iwe unatalii mji mpya au unasafiri katika mji wako, Uber inaweza kukusaidia kusafiri karibu popote, wakati wowote. Sasa, jipatie hadi Flying Blue Miles 2 kwa kila euro unayotumia popote uendapo. Badilisha safari ziwe Miles and Miles katika likizo yako ijayo.
Unganisha tu akaunti zako ili uanze kujipatia mapato. Kwenye kompyuta? Sogeza chini ili uchanganue msimbo wa QR kwenye kifaa chako cha mkononi ili uanze.
Je, nitapata Maili ngapi?
Ufaransa
Utapokea Maili 1 kwa kila Euro utakayotumia kwenye Uber X Priority, Berline, Comfort, Teksi, Van na Uber Reserve nchini Ufaransa.
Uholanzi
Utapata Maili 1 ya Flying Blue kwa kila Euro unayotumia kwenye safari zote za Uber nchini Uholanzi.
Baada ya safari 4 ukitumia Uber ndani ya mwezi mmoja
Utapata Maili MARA MBILI (Maili 2 kwa kila Euro unayotumia) kwenye safari zote za Uber mjini Ufaransa na Uholanzi kwa muda uliosalia wa mwezi huo na miezi 3 inayofuata! Kwa mfano, ukikamilisha safari 4 ukitumia Uber kati ya tarehe 1 na 15 Agosti, utapokea Maili 2 kwa kila Euro utakayotumia kwenye safari zako zote katika kipindi kilichosalia cha Agosti, Septemba, Oktoba na hadi mwisho wa Novemba!
Utaratibu wake
Je, una akaunti ya Flying Blue na ya Uber? Kuunganisha huchukua dakika moja pekee.
Changanua tu msimbo wa QR au ubofye kitufe cha "Unganisha akaunti" kilicho hapa chini ili uunganishe akaunti zako ndani ya programu ya Uber
Kisha, safiri ukitumia Uber - kupata Maili ni rahisi!
Maili unazopata zitawekwa kwenye akaunti yako ya Flying Blue.
Je, huna Akaunti ya Flying Blue?
Anza kupata Maili sasa!
Sheria na Masharti: Ushirikiano kati ya Flying Blue na Uber
Sheria na masharti yafuatayo yanabainisha ushirikiano kati ya Flying Blue na Uber, unaotoa manufaa na zawadi za kipekee kwa washiriki wa Flying Blue wanaotumia huduma za Uber. Kwa kushiriki katika ushirikiano huu, washiriki wa Flying Blue wanaweza kupata Maili za Flying Blue wanaposafiri wakitumia Uber wanapotumia bidhaa zinazotimiza masharti. Tafadhali soma sheria na masharti yafuatayo kwa umakini ili uelewe maelezo ya ofa, ikijumuisha taratibu za usajili, mipango ya mapato na usimamizi wa akaunti.
Sifa
Ni lazima uwe mshiriki wa mpango wa Flying Blue na uwe na akaunti ya Uber inayotumika ili unufaike kutokana na ofa hii. Bila kujali hali yao ya ushiriki, washiriki wote wa Flying Blue wanaweza kupata Maili za Flying Blue wanaposafiri wakitumia Uber kwa kutumia bidhaa katika nchi zilizosajiliwa katika ofa. Baada ya kujisajili kwenye ushirikiano, Maili utakazopata zitawekwa kwenye akaunti yako ndani ya muda usiozidi saa 48 baada ya kukamilisha safari inayotimiza masharti.
Kujisajili katika ushirikiano wa Uber na Flying Blue
2.1 Unaweza kujisajili katika ushirikiano wa Uber na Flying Blue kupitia www.flyingblue.com, programu ya Flying Blue, programu ya Air France, programu ya KLM au programu ya Uber. Ukijisajili kupitia programu ya Uber, ni lazima uingie kwenye wasifu wako wa Uber kisha uingie kwenye akaunti yako ya mtandaoni ya Flying Blue ili uunganishe akaunti yako ya Flying Blue. Kisha, akaunti zote mbili zitaunganishwa. Ikiwa bado hujajisajili kwenye mpango wa Flying Blue, ni lazima kwanza ujisajili kwenye mpango huu kupitia www.flyingblue.com au https://login.flyingblue.com/enrol/flyingblue kisha uunganishe akaunti uliyofungua ya Flying Blue kwenye akaunti yako ya Uber kama inavyoelezwa hapo juu.
2.2 Kuchagua Flying Blue katika Programu ya Uber
Kufuatia usajili wako kama inavyoelezwa katika Sehemu ya 2.1 hapo juu, itabidi uchague Flying Blue kama mpango wa zawadi utakazochagua katika Programu ya Uber. Wakati mwingine Uber inaweza kuonyesha zaidi ya mpango mmoja wa zawadi. Katika hali hiyo, itabidi uchague Flying Blue kwenye orodha ya mipango inayotolewa ya zawadi katika Programu ya Uber.
Mpango na taratibu za kupata Maili.
Kufuatia kukamilika kwa hatua zilizoelezwa katika Sehemu ya 2.1. na 2.2. unaweza kupata Maili ukitumia Flying Blue unaposafiri ukitumia bidhaa za Uber zinazopewa zawadi. Baada ya kukamilisha safari zinazotimiza masharti ukitumia Uber, Maili za Flying Blue zitawekwa kwenye akaunti yako ya Flying Blue kulingana na yafuatayo:
Ufaransa Maili 1 ya Flying Blue Mile kwa kila Euro iliyotumika kwenye Uber X Priority, Comfort, Berline, Taxi na Van, nchini Ufaransa. Hii ni pamoja na safari zilizowekewa nafasi kupitia Uber Reserve bila kujumuisha Uber Central.
Ikiwa msafiri alisafiri angalau mara 4 (safari za aina yoyote) katika mwezi wowote wa kalenda, mshiriki atapata Maili 2 za Flying Blue kwa kila Euro aliyotumia kwenye safari ya tano na safari zote zilizosalia kwenye bidhaa zote katika mwezi huo wa kalenda na miezi 3 ya kalenda ifuatayo nchini Ufaransa.
Kwa mfano, nchini Ufaransa, ikiwa umesafiri mara 4 kupitia Uber Green kati ya tarehe 1 na 15 Agosti, utapokea Maili 2 kwa kila Euro utakayotumia katika usafiri wako katika kipindi kilichosalia cha Agosti, Septemba, Oktoba na hadi mwisho wa Novemba.
Uholanzi Maili 1 ya Flying Blue kwa kila Euro unayotumia kwenye safari zote zinazofanyika nchini Uholanzi kwenye bidhaa zifuatazo - UberX, Saver, Uber Pet, Green, Comfort, Black, Van, Uber Priority, Uber XShare na 'bidhaa yoyote mpya' na 'ya muda/kipindi' kwenda mbele. Hii ni pamoja na safari zilizowekewa nafasi kupitia Uber Reserve bila kujumuisha Uber Central.
Ikiwa msafiri alisafiri angalau mara 4 (safari za aina yoyote) katika mwezi wowote wa kalenda, mshiriki atapata Maili 2 za Flying Blue kwa kila Euro aliyotumia kwenye safari ya tano na safari zote zilizosalia kwenye bidhaa zote katika mwezi huo wa kalenda na miezi 3 ya kalenda ifuatayo nchini Uholanzi.
Kwa mfano, nchini Uholanzi, ikiwa umesafiri mara 4 ukitumia Uber X kati ya tarehe 1 na 15 Agosti, utapokea Maili 2 kwa kila Euro utakayotumia katika usafiri wako katika kipindi kilichosalia cha Agosti, Septemba, Oktoba na hadi mwisho wa Novemba.
Huweza kupata Maili kwenye bidhaa na mifumo ifuatayo ya Uber: UberEats, Vocha, UberRentals, Usafiri wa Umma na Usafiri wa magurudumu mawili.
Changia Nauli
Uber inatoa utendaji maalum unaoitwa "Changia Nauli". Unaposafiri pamoja na marafiki au makundi ya watu, mnaweza kuchangia nauli. Hamna haja ya kubadilishana pesa taslimu, iambie programu ikufanyie hesabu kisha ikutumie bei ya nauli. Kwa kutegemea ikiwa watumiaji wameunganisha akaunti yao ya Uber na akaunti yao ya Flying Blue, kila mpokeaji wa bei ya nauli atapata Maili kulingana na kiasi anacholipa.
Kusitisha na Kuondoa Akaunti
Washiriki wanaweza kuamua kujiondoa kwenye ofa ya ushirikiano wa Uber na Flying Blue wakati wowote. Ili kufanya hivyo, unapaswa kuondoa akaunti: Baada ya kuunganisha akaunti zako, ili uondoe akaunti unapaswa kuchagua mpango uliounganishwa ambapo utaweza kuchagua kitufe cha 'Ondoa' ili uondoe akaunti yako.
Ukijiondoa kwenye ofa ya ushirikiano wa Uber na Flying Blue, akaunti zako za Uber na Flying Blue zitaendelea kutumika. Unaweza kujisajili tena katika ofa baadaye, hata hivyo ikiwa ulizawadiwa Kifurushi cha Kukukaribisha kwenye Mpango wa Maili (toleo la muda mfupi linalobuniwa ili kuhamasisha kuunganisha akaunti), tafadhali kumbuka kuwa hutatimiza masharti ya kupokea Kifurushi cha Kukukaribisha kwenye Mpango wa Miles unapojisajili tena. Ukijiondoa kwenye ofa, Maili zozote ulizopata ambazo bado hazijawekwa kwenye akaunti wakati wa kuondoa akaunti zitaondolewa.
Faragha
Kujisajili katika ofa ya ushirikiano wa Uber na Flying Blue kunahitaji Uber na Flying kushughulikia data binafsi ya Washiriki. Kwa kujisajili katika ofa hii, Washiriki wanakubali waziwazi kushughulikiwa kwa data yao binafsi, itakayotumika kwa madhumuni ya kudhibiti ofa ya ushirikiano na kuweka alama kwenye mpango wa maili za Flying Blue. Data binafsi inayoshughulikiwa inaweza kujumuisha, lakini si tu, jina, anwani ya barua pepe, namba ya kadi ya uaminifu ya Flying Blue ya Mshiriki na idadi ya pointi au maili zitakazowekwa. Uber na Flying Blue zitatii sheria na kanuni zote zinazotumika zinazosimamia ulinzi wa data binafsi na zitachukua hatua zinazofaa za kiufundi na za shirika ili kudumisha usalama na usiri wa data binafsi inayoshughulikiwa. Washiriki wana haki ya kufikia, kurekebisha na kufuta data zao binafsi, pamoja na haki ya kupinga uchakataji wa data zao binafsi kwa sababu halali.
Sheria na masharti yote yanatii sera za faragha za Uber na Flying Blue ili kuhakikisha kuwa data ya mteja inalindwa. https://privacy.uber.com/center https://www.flyingblue.com/en/privacy-policy
Kubadilisha Sheria na Masharti
Uber na Flying Blue zinahifadhi haki ya kurekebisha au kubadilisha ofa, ikijumuisha kuongeza au kusitishwa kwa baadhi ya bidhaa au huduma zinazotimiza masharti ya kupata Maili za Flying Blue. Kukitokea mabadiliko yoyote, Uber na Flying Blue zitawajulisha washiriki wote wa Flying Blue ambao wamejisajili katika ushirikiano wa Flying Blue na Uber.
Kuhusu