Weka nafasi mapema, ghairi siku ya
Weka nafasi ya usafiri wako hadi siku 90 mapema¹ na ufurahie kughairi bila malipo siku ambayo utachukuliwa.⁷
Mapendekezo
Weka nafasi mapema, safiri kwa urahisi
Kughairi kwa urahisi
Umebadilisha mipango? Unaweza kughairi nafasi uliyoweka siku hiyohiyo bila malipo—hakuna na hakuna malipo.⁷
Kuaminika kwa wakati
Teknolojia yetu husaidia kuhakikisha kwamba unachukuliwa kwa wakati ili usafiri bila usumbufu.²
Tuko tayari kila wakati
Safari yako itafanyika jinsi ulivyopanga, kutakuwa na dakika 15 za kusubiri.³
Imeandaliwa kukufaa wewe
Chaguo za usafiri kwa kila bajeti na tukio—na umwite Dereva Unayempenda.⁴
Ni bora kwa usafiri
Unaweza kuweka nafasi za kwenda au kutoka kwenye viwanja vikuu vya ndege. Teknolojia yetu ya kufuatilia ndege inakuhakikishia kwamba utapata usafiri ukitua mahali unakoenda—hata ikiwa ndege yako itachelewa.⁵
Weka nafasi
Gusa aikoni ya Weka nafasi kwenye programu ya Uber iliyosasishwa. Weka nafasi angalau dakika 15 mapema.⁶
Pokea thibitisho
Rejelea maelezo yako ya kuweka nafasi ya usafiri kwenye programu na umkague dereva safari yako inapokaribia. Ghairi bila malipo hadi saa moja mapema.⁷
Safari
Kutana na dereva wako nje ndani ya muda wa kusubiri uliojumuishwa katika nafasi uliyoweka. Furahia safari yako.
¹ Unapoomba usafiri wa Uber Reserve, bei ya safari unayoona itakuwa makadirio ambayo yanajumuisha ada ya kuweka nafasi inayoweza kutofautiana kulingana na eneo la kuchukuliwa na/au siku na saa ya safari. Ada hii hulipwa na wasafiri kwa muda wa ziada ambao dereva wao anasubiri na umbali au muda anaotumia kusafiri hadi eneo la kukuchukua.
² Uber haikuhakikishii kuwa dereva atakubali ombi lako la usafari. Safari yako huthibitishwa mara unapopokea maelezo kumhusu dereva wako. Huduma ya Reserve inapatikana katika miji mahususi.
³ Muda wa kusubiri hutofautiana kulingana na aina ya gari unalochagua.
⁴ Kipengele cha dereva unayependa kinapatikana tu katika maeneo mahususi.
⁵ Inapatikana tu katika viwanja mahususi vya ndege. Hutatozwa ada ya kusubiri hadi saa moja baada ya makadirio ya muda wa kuwasili kwa ndege yako. Baada ya hapo, dereva anaweza kughairi ombi la usafiri na utatozwa nauli yote. Ombi lako la usafiri huthibitishwa mara unapopokea maelezo ya safari yako. Hata hivyo, dereva wako bado anaweza kughairi ombi lako la usafiri. Katika hali hii, ombi la usafiri litakabidhiwa dereva mwingine aliye karibu. Tafadhali kumbuka kwamba Uber haiwezi kukuhakikishia kwamba dereva atakubali ombi lako la usafiri.
⁶ Inatumika kwa UberX na aina nyingine nyingi za usafiri. Baadhi ya aina za usafiri zinaweza kuhitaji muda zaidi wa kuchakata ombi la kusafiri. Angalia masharti ya Reserve katika programu yako ili upate maelezo.
⁷ Ada ya kughairi ya Reserve ni nyingi kuliko ya kuomba usafiri unapohitajika. Unaweza kughairi bila kutozwa hadi dakika 60 kabla ya muda wa kuchukuliwa Uliowekea nafasi. Ukighairi chini ya dakika 60 kabla ya muda Uliowekea nafasi kufika, utatozwa ada ya kughairi iliyo hapa chini ili kufidia muda wa dereva. Hutatozwa ada ya kughairi ikiwa bado hakuna Dereva aliyethibitisha safari yako. Utapokea arifa dereva wako akiwa njiani kuja uliko.
Unaweza kuangalia kiasi cha ada ya kughairi kinachotumika kwenye safari yako kwa kubofya " Angalia masharti" kutoka kwenye skrini ya uteuzi wa muda ya ndani ya programu inayoonyesha unapoweka nafasi ya safari na kusogeza chini hadi kwenye aina ya huduma unayopendelea.
Kuhusu
Chunguza
Viwanja vya Ndege