Tarehe ya mwisho kubadilishwa: 12/8/2026
UBER B.V.
Sheria na Masharti
1. Uhusiano wa Kikandarasi
Sheria hizi za Utumizi ("Sheria") zinatawala ufikiaji au utumizi wako, wa mtu binafsi, kutoka ndani mwa nchi yoyote ulimwenguni (isipokuwa Marekani na maeneo yake na milki zake na Uchina Barani) wa App, tovuti, maudhui, bidhaa, na huduma ("Huduma") zinazotolewa na Uber B.V., kampuni ya kibinafsi iliyoanzishwa nchini Uholanzi, ikiwa na ofisi zake Burgerweeshuispad 301, 1076 HR, Uholanzi, iliyosajiliwa kwenye Idara ya Biashara ya Amsterdam kwa nambari 56317441 ("Uber").
TAFADHALI SOMA SHERIA HIZI KWA UANGALIFU KABLA YA KUFIKIA AU KUTUMIA HUDUMA.
Ufikiaji na utumizi wako wa Huduma unaonyesha makubaliano yako kufungwa na Sheria hizi, jambo linaloanzisha uhusiano wa kikandarasi baina yako na Uber. Ikiwa haukubaliani na sheria hizi, huenda kufikia wala kutumia Huduma. Sheria hizi zinapiku makubaliano na mipango ya awali pamoja nawe. Uber iinaweza kusitisha maramoja Sheria hizi au Huduma zozote zinazohusiana nawe, au kwa ujumla isitishe kukupatia Huduma au ikunyime ufikiaji kwa Huduma hizi au sehemu yazo, wakati wowote kwa sababu yoyote.
Sheria za Nyongeza huenda zikatumika kwa Huduma fulani, kama vile sera za tukio, harakati au ukuzaji fulani wa kibiashara, na sheria hizo za nyongeza zitafichuliwa kwako kuhusiana na Huduma husika. Sheria za nyongeza ni nyongeza kwa, na zitachukuliwa kuwa sehemu ya, Sheria kwa madhumuni ya Huduma husika. Sheria za nyongeza zitapiku Sheria hizi katika tukio la ukinzani panapotokea kuhusiana na Huduma husika.
Uber inaweza kurekebisha Sheria zinazohusiana na Huduma mara kwa mara. Marekebisho yataanza kutumika baada ya Uber kuchapisha Sheria hizo zilizosasishwa katika sehemu hii au sera au sheria za nyongeza zilizorekebishwa kwenye Huduma husika. Ufikiaji au utumizi wako endelevu wa Huduma hii baada ya uchapishaji huo kunaonyesha ridhaa yako ya kufungwa na Sheria hizo, kama zilivyorekebishwa.
Ukusanyaji na utumizi wetu wa taarifa za kibinafsi kuhusiana na Huduma hizi ni kama ilivyoelezwa kwenye Sera ya Faragha ya Uber iliyo katika https://www.uber.com/global/sw/privacy/notice/. Uber inaweza kumpa mwendeshaji madai au mtoa bima taarifa zozote zinazohitaji (ikijumuisha taarifa zako za mawasiliano zako) ikiwa kuna malalamishi, mgogoro au mzozo, ambapo inaweza kujumuisha ajali inayokuhusisha wewe na Mtoa Huduma Mwingine (ikijumuisha Dereva wa kampuni ya mfumo wa usafirishaji) na ikiwa taarifa au data hiyo inahitajika ili kusuluhisha yale malalamishi, mgogoro, au mzozo huo.
2. Huduma
Huduma zile zinajumuisha mfumo wa kiteknolojia unaowawezesha watumizi wa App ya simutamba au tovuti za Uber zinazotolewa kama sehemu ya Huduma (kila moja, "App") ili kupanga na kuratibu huduma za usafirishaji na/au uratibu pamoja na watoa huduma wengine huru wanaotoa huduma hizo, ikijumuisha watoa huduma wengine huru wa huduma za usafirishaji na watoa huduma wengine huru wanaotoa huduma za uratibu chini ya makubaliano na Uber au Washirika fulani wa Uber ("Watoa Huduma Wengine"). Isipokuwa ikubalianwe vingine na Uber katika makubaliano tofauti kwa maandishi pamoja nawe, Huduma zinatolewa kwa utumizi wa kibinafsi na usio wa kibishara pekee. UNATAMBUA KWAMBA UBER HAITOI HUDUMA ZA USAFIRSHAJI AU URATIBU WALA KUTENDA KAMA MWENDESHAJI BIASHARA YA USAFIRISHAJI NA KWAMBA HUDUMA HIZO ZOTE ZA USAFIRISHAJI NA URATIBU ZINATOLEWA NA WANAKANDARASI WENGINE HURU AMBAO HAWAJAAJIRIWA NA UBER AU YEYOTE KATI YA WASHIRIKA WAKE.
Leseni.
Chini ya uambatanaji wako na Sheria hizi, Uber inakupatia leseni yenye kipimo, isiyo yako kipekee, isiyoweza kutolewa leseni ndogo, inayoweza kubatilishwa, na isiyoweza kuhamishika ya: (i) kufikia na kutumia App kwenye kifaa chako binafsi kuhusiana tu na matumizi ya Huduma; na (ii) kufikia na kutumia maudhui, taarifa na nyenzo zozote husiani ambazo zinaweza kufanywa kupatikana kupitia Huduma, katika kila tukio ikiwa kwa utumizi wako binafsi pekee, na usio wa kibiashara. Haki zozote ambazo hazijapeanwa hapa moja kwa moja zimehifadhiwa na Uber na wenye kuipa leseni.
Vikwazo.
Hauwezi: (i) kutoa ilani zozote za haki miliki, alama za kibiashara au zingine za umiliki kutokana na sehemu yoyote ya Huduma; (ii) kuzalisha tena, kurekebisha, kutayarisha kitu chochote kimsingi na, kusambaza, kutoa leseni, kukodisha, kuuza, kuuza tena, kuhamisha, kuonyesha hadharani, kutumaniana, kutiririsha mtandaoni, kupeperusha hewani, au vinginevyo kunyonya Huduma isipokuwa ikama ivyoruhusiwa na Uber moja kwa moja; (iii) kutuoanisha, kugeuza uhandisi au kutenganisha Huduma isipokuwa kama ilivyoruhusiwa na sheria husika; (iv) kuweka viungo kwa, kuigiza au kuwekea mfumo sehemu yoyote ya Huduma; (v) kusababisha au kuzindua programu zozote kwa dhumuni la kunakili, kuorodhesha, kufanyia utafiti, au vinginevyo kudukua data ya sehemu yoyote ya Huduma hizi au kuwekea mzigo isivyostahili au kuzuia oparesheni na/au utendakazi wa kipengee chochote cha Huduma; au (vi) kujaribu kupata ufikiaji ambao haujaidhinishwa au kulemaza kipengele chochote cha zile Huduma au mifumo na mitandao yake husiani.
Utoaji Huduma.
Unatambua kwamba huenda sehemu za Huduma zikawa zinapatikana chini ya bidhaa mbalimbali za Uber au chaguo za maombi husiani na usafirishaji au uratibu, ikijumuisha bidhaa za maombi usafirishaji zinazojulikana kwa sasa kama "Uber," "uberPOP," "uberX," "uberXL," "UberBLACK," "UberSUV," "UberBERLINE," "UberVAN," "UberEXEC," na "UberLUX" na bidhaa za maombi ya uratibu zinazojulikana kwa sasa kama "UberRUSH," "UberFRESH" na "UberEATS". Pia unatambua kwamba Huduma zinaweza kufanywa kupatikana chini ya bidhaa na chaguo hizo za maombi na au kwa uhusiano na: (i) baadhi ya matawi na washirika wa Uber; au (ii) Watoa Huduma Wengine huru, ikijumuisha madereva wa kampuni ya mtandao wa usafirishaji, wamiliki vibali vya usafirishaji au wamiliki vibali sawia vya usafirishaji, idhini au leseni.
Huduma na Maudhui ya Vyombo Vingine.
Huduma zinaweza kufanywa kupatikana au kufikiwa kwa uhusiano na huduma na maudhui ya vyombo vingine (ikijumuisha utangazaji) ambayo Uber haidhibiti. Unatambua kwamba sheria tofauti za utumizi na sera tofauti za faragha huenda zinaweza kutumika kwa utumizi wako wa huduma na maudhui ya vyombo vingine. Uber haiungi mkono huduma na maudhui hayo ya vyombo vingine na hakuna wakati ambapo Uber itawajibika au kuwa na kulaumiwa kwa ajili ya bidhaa au huduma zozote za watoa huduma hao wengine. Kwa kuongezea, Apple Inc., Google, Inc., Microsoft Corporation au BlackBerry Limited na/au matawi na washrika wao wa kimataifa watakuwa wafaidi wengine kwa kandarasi hii ukifikia Huduma kwa kutumia App zilizotengenezewa mifumo ya Apple iOS, Android, Microsoft Windows, au vifaa vya mkononi vya Blackberry. Wafaidi hawa wengine sio wahusika kwenye kandarasi hii na hawawajibiki kwa utoaji au usaidizi kwa Huduma kwa namna yoyote. Ufikiaji wako kwa Huduma hizi ni chini ya sheria zilizowekwa kwenye sheria za huduma za wafaidi wengine husika.
Umiliki.
Huduma na haki zote hapa ni, na zitasalia kuwa mali ya Uber au mali ya wenye kuipa Uber leseni. Sheria hizi wala utumizi wako wa Huduma hauonyeshe wala kukupa wewe haki zozote: (i) katika au kuhusiana na Huduma isipokuwa leseni yenye kipimo iliyopeanwa hapa juu; au (ii) za kutumia au kurejelea kwa njia yoyote majina, nembo, majina ya bidhaa na huduma, alama za kibiashara au alama za huduma za Uber au za wenye kuipa Uber leseni.
3. Utumizi Wako wa Huduma
Akaunti za Watumizi.
Ili kuweza kutumia vipengele vingi vya Huduma, weweni lazima ujisajili na udumishe akaunti amilifu ya kibinafsi Huduma za mtumizi ("Akaunti"). Ni lazima uwe na umri wa angalau miaka 18, au umri wa watu wazima kisheria katika eneo lako (ikiwa ni tofauti na miaka 18), ili kupata Akaunti. Usajili wa Akaunti unakuhitaji uwasilishe kwa Uber taarifa fulani za kibinafsi, kama vile jina, anwani, nambari ya simutamba na umri wako, na pia angalau mbinu moja halali ya malipo (iwe kadi ya malipo au mbia wa malipo anayekubalika). Unakubaliana kudumisha taarifa sahihi, kamili, na ya sasa zaidi katika Account yako. Kushindwa kwako kudumisha taarifa sahihi, kamili, na ya sasa zaidi ya Akaunti, ikijumuisha kuwa na mbinu ya malipo ambayo ni batili au iliyopitwa na wakati, huenda kukakusababishia kutoweza kwako kufikia na kutumia zile Huduma au Uber kusitisha Sheria hizi nawe. Unawajibikia shughuli zote zinazofanyika ndani ya Akaunti yako, na unakubaliana kudumisha usalama na usiri wa jina la mtumizi na nenosiri la Akaunti yako nyakati zote. Isipokuwa iruhusiwe vinginevyo na Uber kwa maandishi, utaweza tu kumiliki Akaunti moja.
Mahitajiko kwa Mtumizi na Tabia.
Huduma hizi hazipatikani kwa utumizi wa watu walio chini ya umri wa miaka 18. Hauwezi kuwapa idhini vyombo vingine kutumia Akaunti yako, na hauwezi kuwaruhusu watu wenye umri wa chini ya miaka 18 kupokea huduma za usafirishaji au uratibu kutoka kwa Watoa Huduma Wengine isipokuwa uandamane nao. Hutakabidhiana au vinginevyo kuhamisha Akaunti yako kwa mtu au chombo kingine. Unakubaliana kuambatana na Sheria zote husika unapotumia Huduma hizi, utatumia tu Huduma zenyewe kwa madhumuni ya kisheria (k.m., hakuna usafirishaji vitu visivyo halali au hatari). Katika utumizi wako wa hizi Huduma, hautasababisha kero, hasira, usumbufu, au uharibifu wa mali, iwe ni kwa Mtoa Huduma Mwingine au mhusika mwingine yeyote. Katika matukio fulani huenda ukaombwa kutoa thibitisho la utambulisho ili kufikia au kutumia Huduma, na unakubaliana kwamba huenda ukanyimwa ufikiaji au utumizi wa Huduma ukikosa kutoa thibitisho la utambulisho.
Kutuma Arafa.
Kwa kufungua Akaunti, unakubaliana kwamba Huduma zinaweza kukutumia arafa (SMS) za taarifa kama sehemu ya shughuli ya kawaida ya biashara ya utumizi wako wa Huduma. Unaweza kujiondoa ili usipokee arafa (SMS) kutoka kwa Uber wakati wowote kwa kutuma barua pepe kwa support@uber.com ukieleza kwamba hautaki tena kupokea jumbe hizo, pamoja na nambari ya simu ya kifaa kinachopokea jumbe hizo. Unatambua kwamba kujiondoa ili usipokee zile arafa (SMS) kunaweza kuathiri utumizi wako wa Huduma.
Misimbo ya Ukuzaji Biashara.
Uber, kwa hiari yake pekee, inaweza kuunda mismbo ya ukuzaji biashara ambayo inaweza kutumiwa kupata salio la Akaunti, au vipengele au manufaa mengine husiani na Huduma na/au huduma za Mtoa huduma Mwingine, chini ya sheria zozote za ziada ambazo Uber inaweza kwa msingi wa kila msimbo cha ukuzaji biashara ("Misimbo ya Ukuzaji Biashara"). Unakubali kwamba Misimbo ya Ukuzaji Biashara: (i) ni lazima itumike kwa hadhira na dhumuni lililokusudiwa, na kwa njia ya kisheria; (ii) haiwezi kunakilishwa, kuuzwa au kuhamishwa kwa namna yoyote, au kufanywa kupatikana kwa umma (iwe ni kuchapishwa kwenye fomu ya umma au vinginevyo), isipokuwa iwe moja kwa moja imekuruhusiwa na Uber; (iii) inaweza kulemazwa na Uber wakati wowote kwa sababu yoyote bila dhima kwa Uber; (iv) inaweza tu kutumika kwa kulingana na sheria mahsusi ambazo Uber imewekea Msimbo huo wa Ukuzaji Biashara; (v) sio halali kubadilishwa na pesa; na (vi) inaweza kupitwa na wakati wake kabla haujaitumia. Uber inahifadhi haki ya kushikilia au kupunguza masalio au vipengele au manufaa mengine yanayopatikana kupitia utumizi wako au wa mtumizi mwingine wa Misimbo ya Ukuzaji Biashara katika tukio ambapo kwamba Uber inaamua au inaamini kwamba utumizi huo wa Msimbo wa Ukuzaji Biashara ulikuwa wa kimakosa, ulaghai, usio halali, au wenye kukiuka sheria za Msimbo husika wa Ukuzaji Biashara au Sheria hizi.
Maudhui Iliyotolewa na Mtumizi.
Uber, kwa hiari ya Uber ya kipekee, inaweza kukuruhusu mara kwa mara kuwasilisha, kupakia, kuchapisha au vinginevyo ukapeana kwa Uber maudhui na taarifa za kimaandishi, sauti, na/au picha za Huduma, ikijumisha maoni husiani na Huduma, kuanzishwa kwa maombi ya usaidizi, na wasilisho la ushiriki katika mashindano na tamasha za ukuzaji ("Maudhui ya Mtumizi"). Maudhui yoyote ya Mtumizi uliyotoa inasalia kuwa mali yako. Hata hivyo, kwa kupeana Maudhui ya Mtumizi kwa Uber, unaipa Uber leseni ya kote ulimwenguni, ya milele, isiyoweza kubatilishwa, isiyoweza kuhamishika, leseni isiyoweza kulipishwa, ikiwa na haki ya kupeana leseni ndogo, ya kutumia, kunakili, kurekebisha, kuunda kazi zinazofanana, kusambaza, kuonyesha hadharani, kufanyia maonyesho hadharani, na vinginevyo kunyonya kwa njia yoyote Maudhui hayo ya Mtumizi katika mifumo na mbinu zote za usambazaji zinazojulikana sasa au zitakazovumbuliwa baadaye (ikijumuisha zinazohusiana na Huduma na biashara ya Uber na kuhusu tovuti na huduma za vyombo vingine), bila ya ilani za ziada kwako au ridhaa kutoka kwako, na bila ya hitajiko la kukulipa wewe au mtu au chombo kingine.
Unawakilisha na kuhakikishia kwamba: (i) wewe ni mmiliki wa kipekee wa Maudhui yote ya Mtumizi au una haki, leseni, ridhaa na vibali vyote vinavyohitajika ili kuipa Uber leseni ya Maudhui ya Mtumizi kama ilivyoelezwa hapo juu; na (ii) Maudhui ya Mtumizi wala wasilisho, upakiaji, uchapishaji wako au vinginevyo kufanya Maudhui hayo ya Mtumizi kupatikana wala utumizi wa Uber wa Maudhui ya Mtumizi kama ilivyoruhusiwa hapa kutakiuka, kutumia vibaya au kukiuka haki miliki au haki za mali, au haki za utangazaji au faragha za chombo kingine, au kusababisha ukiukaji wa sheria au kanuni yoyote husika.
Unakubaliana kutotoa Maudhui ya Mtumizi ambayo ni ya kuchafua jina, ya shutuma za uwongo, ya chuki, ya ghasia, chafu, ya ngono, sio ya kisheria, au vinginevyo ni ya hatia, kama itakavyoamuliwa na Uber kwa hiari yake ya kipekee, iwe nyenzo zile zimelindwa na sheria au la. Uber inaweza, lakini haitakuwa na jukumu la, kukagua, kufuatilia au kuondoa Maudhui ya Mtumizi, kwa hairi ya Uber ya kipekee na wakati wowote na kwa sababu yoyote, bila ilani kwako.
Ufikiaji Mtandao na Vifaa.
Unawajibika kupata ufikiaji unaohitajika kwa mtandao wa data ili kutumia Huduma. Malipo na ada za wavuti na arafa za mtandao wako wa simutamba zinaweza kutumika ukifikia au ukitumia Huduma kwenye kifaa chenye uwezo wa pasi waya na utawajibikia malipo na ada hizo. Una wajibu wa kupata na kusasisha vifaa vinavyoingia au vifaa vinavyohitajika ili kufikia na kutumia Huduma na App na sasisho zozote zake. Uber haihakikishii kwamba Huduma, au sehemu yoyote yake, itafanya kazi kwenye kifaa fulani. Kwa kuongezea, Huduma zinaweza kupatwa na hitilafu na ucheleweshaji unaotokana na utumizi wa Wavuti na mawasiliano ya kielektroniki.
4. Malipo
Unaelewa kwamba utumizi ya Huduma unaweza kukusababishia wewe kutozwa ada kwa ajili ya huduma na bidhaa unazopokea kutoka kwa Mtoa Huduma Mwingine ("Ada "). Baada ya kupokea huduma au bidhaa zinazopatikana kupitia utumizi wa Huduma, Uber itawezesha malipo yako ya Ada husika kwa niaba ya Mtoa Huduma Mwingine kama wakala wa kukusanya malipo wa Mtoa Huduma huyo Mwingine. Ada zinaweza kujumuisha gharama nyingine husika, pamoja na au na ada za jiji, manispaa, gharama za uwanja wa ndege na pia gharama za utekelezaji wa malipo. Malipo ya Ada kwa namna hiyo yatachukuliwa kuwa sawia na malipo yaliyofanywa nawe moja kwa moja hadi kwa Mtoa Huduma huyo Mwingine. Ada zitajumuisha ushuru husiani panapohitajika na sheria. Ada unazolipa ni za mwisho na haziwezi kurejeshwa, isipokuwa iamuliwe vinginevyo na Uber. Utapata taarifa zaidi kuhusu sera ya Uber ya kurejesha pesa hapa kwenye tovuti ya Uber. Unasalia na haki ya kuomba Ada za chini kutoka kwa Mtoa Huduma Mwingine kwa ajili ya huduma au bidhaa unazopokea kutoka kwa Mtoa Huduma huyo Mwingine wakati unapopokea huduma au bidhaa hizo. Uber itajibu ifaavyo ombi lolote kutoka kwa Mtoa Huduma Mwingine la kurekebisha Ada za huduma au bidhaa fulani.
Ada zote zinapaswa kulipwa maramoja na malipo yatawezeshwa na Uber ikitumia mbinu ya malipo inayopendelewa iliyoteuliwa katika Akaunti yako, kisha baadaye Uber litakutumia risiti kwa barua pepe. Ikiwa mbinu msingi ya malipo ya Akaunti yako itapatikana kuwa imeishiwa na muda, ni batili au vinginevyo haiwezi kutozwa ada, unakubaliana kwamba Uber, kama wakala wa kukusanya malipo wa Mtoa Huduma huyo Mwingine, inaweza kutumia mbinu ya upili ya malipo katika Akaunti yako, ikiwa ipo.
Baina yako na Ube, Uber inahifadhi haki ya kuweka, kuondoa na/au kusahihisha Ada za huduma na bidhaa zozote au zote zinazopatikana kutokana na utumizi wa Huduma hizi wakati wowote kwa hiari ya Uber ya kipekee. Zaidi ya hayo, unatambua na kukubaliana kwamba Ada zinazotumika katika maeneo fulani ya kijiografia huenda ikaongezek pakubwa wakati wa nyakati za kuhitajika kwa wingi. Uber itafanya juhudi zinazofaa kukujulisha kuhusu Ada zinazohusika, bora iwe kwamba utashughulikia Ada zinazotozwa Akaunti yako iwe unajua kuhusu Ada au malipo hayo. Uber inaweza mara kwa mara kuwapa watumizi fulani matoleo na mapunguzo ya ukuzaji biashara ambayo huenda ikatokana na viwango tofauti vilivyotozwa kwa ajili ya huduma au bidhaa sawia au zilizofanana zilizopatikana kupitia utumizi wa Huduma, na unakubaliana kwamba matoleo na mapunguzo hayo ya ukuzaji biashara, isipokuwa itolewe kwako pia, hayana uhusiano wowote na utumizi wako wa Huduma au Ada unazotozwa. Unaweza kuchagua kubatilisha ombi lako la huduma au bidhaa kutoka kwa Mtoa Huduma Mwingine wakati wowote kabla ya kuwasili kwa Mtoa Huduma huyo Mwingine, ambapo unaweza kutozwa ada ya ubatilishaji.
Mpangilio huu wa malipo unakusudiwa kumfidia kikamilifu ule Mtoa Huduma huyo Mwingine kwa huduma au bidhaa alizotoa. Isipokuwa kuhusiana na huduma za usafirishaji za teksi zilizoagizwa kupitia App, Uber haitoi sehemu yoyote ya malipo yako kama zawadi au shukrani kwa Mtoa Huduma Mwingine. Uwakilishi wowote wa Uber (kwenye tovuti ya Uber, katika App, au katika nyenzo za uuzaji za Uber) kwamba kupeana zawadi ni "kwa hiari," "hakuhitajiki," na/au "kumejumuishwa" katika malipo unayoyafanya kwa ajili ya huduma au bidhaa zilizotolewa haikusudiwi kumaanisha kwamba Uber fedha zozote za ziada, zaidi ya zile zilizoelezwa hapo juu, Mtoa Huduma huyo Mwingine. Unaelewa na kukubaliana kwamba, ingawa uko huru kutoa malipo ya ziada kama tuzo kwa Mtoa Huduma Mwingine anayetoa huduma au bidhaa zinazopatikana kupitia Huduma hii, hauna jukumu lolote la kufanya hivyo. Tuzo za shukrani ni kwa hiari. Baada ya kupokea huduma au bidhaa zinazopatikana kupitia Huduma, utakuwa na fursa ya kupea alama hisia zako na kutoa maoni ya ziada kuhusu Mtoa Huduma huyo Mwingine.
Ufichuzi wa Malipo
Uber inaweza kuchakata malipo ya kidijitali kwa miamala (kwa bidhaa au huduma unazopewa na washirika wengine wa kujitegemea) unazolipia kupitia Programu ya Uber katika mpaka wa Tanzania kwa kutumia uchakataji wa malipo yake ya kimataifa na/au washirika wa benki. Kwa kuchagua kulipa kwa kutumia njia ya kulipa uliyohifadhi kidijitali kupitia Programu ya Uber, unakiri na kukubali kwamba:
(a) Muamala wako unaweza kuchakatwa nje ya nchi na washirika wa kimataifa wa kuchakata malipo na washirika wa benki wa Uber.
(b) Kwa sababu hiyo, unaweza kuona muamala wako wa Uber ukionekana kama muamala wa nje ya nchi au wa kigeni katika ujumbe au taarifa zozote zinazotolewa na benki yako.
(c) Benki yako inayotoa inaweza kukutoza ada za ziada kwa ajili ya miamala ya kimataifa.
Pia unakubali kwamba kila wakati unapochagua na/au kulipa kwa kutumia njia ya kulipa ya kidijitali iliyohifadhiwa kwenye Wallet yako, kwa ajili ya muamala kupitia Programu za Uber umekiri na kukubali kwamba masharti yaliyo hapo juu yatazingatiwa.
Ada za Ukarabati au Usafishaji.
Utawajibikia gharama ya ukarabati kwa ajili ya uharibifu, au usafishaji unaohitajika wa, magari na mali ya Mtoa Huduma Mwingine inayotokana na utumizi wa Huduma zilizo chini ya Akaunti yako zinazopita uharibifu wa kawaida wa "kuzeeka" na usafishaji unaohitajika ("Ukarabati na Usafishaji"). Katika tukio ambapo Mtoa Huduma Mwingine ataripoti haja ya Ukarabati na Usafishaji, na ombi hilo la Ukarabati au Usafishaji kuthibitishwa na Uber kwa hiari ya Uber ya kipekee, Uber inahifadhi haki ya kuwezesha malipo ya Ukarabati au Usafishaji huo kwa kwa niaba ya Mtoa Huduma Mwingine ikitumia mbinu ya malipo iliyoteuliwa katika Akaunti yako. Fedha hizo zitatumwa na Uber hadi kwa Mtoa Huduma Mwingine husika na haziwezi kurejeshwa.
5. Makanusho; Mpaka ya Dhima; Uondoaji Lawama.
MAKANUSHO.
HUDUMA ZINAPEANWA "KAMA ZILIVYO" NA "KAMA ZINAVYOPATIKANA." UBER INAKANUSHA UWAKILISHI NA UHAKIKISHO WOTE, WA MOJA KWA MOJA, ULIODOKEZWA AU ULIOPO, AMBAO HAUJAWEKWA MOJA KWA MOJA KATIKA SHERIA HIZI, IKIWA NI PAMOJA NA HAKIKISHO ZILIZODOKEZWA ZA KIBIASHARA, KUFAA KWA DHUMUNI FULANI NA KUTOKIUKWA KWAKE. KWA KUONGEZEA, UBER HAIFANYI UWAKILISHO, UHAKIKISHO, AU UDHAMINI WOWOTE KUHUSIANA NA UAMINIFU, UPATIKANAJI WAKATI UNAOFAA, UBORA, UFAAJI AU UPATIKANAJI WA HUDUMA AU HUDUMA AU BIDHAA ZOZOTE ZILIZOAGIZWA KUPITIA UTUMIZI WA HUDUMA, AU KWAMBA HUDUMA HAITADAKIZWA AU HAITAKUWA NA HITILAFU. UBER HAIHAKIKISHII UBORA, UFAAJI AU USALAMA AU UWEZO WA WATOA HUDUMA WENGINE. UNAKUBALIANA KWAMBA HATARI YOTE INAYOTOKANA NA UTUMIZI WAKO WA HUDUMA, NA HUDUMA AU BIDHAA YOYOTE ILOYOANGIZWA KUHUSIANA NAZO, INASALIA NAWE PEKEE, KWA KIWANGO CHA UPEO KILICHORUHUSIWA NA SHERIA HUSIKA.
MPAKA WA DHIMA.
UBER HAITAWAJIBIKIA UHARIBIFU USIO WA MOJA KWA MOJA, USIOPANGIWA, WA KIPEKEE, WA KUIGWA, WA KIADHABU AU UHARIBIFU WA KUTOKANA NA KITU KINGINE, IKIJUMUISHA FAIDA ZILIZOPOTEZWA, DATA ILIYOPOTEZWA, AJALI ZA KIBINAFSI AU UHARIBIFU WA MALI UNAOHUSIANA AU VINGINEVYO UNAOTOKANA NA UTUMIZI WA HUDUMA, HATA KAMA UBER UMESHAURIWA KUHUSU UWEZEKANO WA UHARIBIFU KAMA HUO. UBER HAITAWAJIBIKIA UHARIBIFU, DHIMA AU HASARA ZOZOTE ZINAZOTOKANA NA: (i) UTUMIZI WAKO AU WEWE KUTEGEMEA HUDUMA AU KUTOWEZA KWAKO KUPATA AU KUTUMIA HUDUMA; AU (ii) BIASHARA AU UHUSIANO WOWOTE KATI YAKO NA MTOA HUDUMA MWINGINE, HATA IKIWA UBER IMESHAURIWA KUHUSU UWEZEKANO WA UHARIBIFU KAMA HUO. UBER HAITAWAJIBIKIA UCHELEWESHWAJI AU KUFELI KWA UTENDAKAZI UNAOTOKANA NA SABABU AMBAZO UBER HAIWEZI KUDHIBITI. UNATAMBUA KWAMBA WATOA HUDUMA WENGINE WA USAFIRISHAJI WANAOTOA HUDUMA ZA USAFIRISHAJI ZILIZOOMBWA KUPITIA BIDHAA FULANI ZA MAOMBI ZINAWEZA KUPENDEKEZA HUDUMA ZA USAFIRISHAJI ZA KULIPIA PAMOJA AU ZA KUSHIRIKIANA NA HUENDA ZIZIWE NA LESENI AU VIBALI ZA KITAALAMU. HAKUNA WAKATI UBER ITAKUWA NA DHIMA KAMILI KWAKO KUHUSIANA NA HUDUMA HIZO KWA UHARIBIFU, HASARA NA SABABU ZOTE ZA HATUA ITAKAYOZIDI EURO MIA TANO (€500).
UNAWEZA KUTUMIA HUDUMA ZA UBER KUOMBA NA KURATIBU USAFIRISHAJI, BIDHAA AU HUDUMA ZA URATIBU PAMOJA NA WATOA HUDUMA WEBGINE, LAKINI UNAKUBALIANA KWAMBA UBER HAINA JUKUMU AU DHIMA KWAKO KUHUSIANA NA USAFIRISHAJI, BIDHAA AU HUDUMA ZOZOTE ZA URATIBU ZILIZOTOLEWA KWAKO NA MTOA HUDUMA MWINGINE KANDO NA ILIVYOELEZEWA MOJA KWA MOJA KATIKA SHERIA HIZI.
MIPAKA NA MAKANUSHO KATIKA SEHEMU YA 5 HAIMAANISHI KUPUNGUZA DHIMA AU KUBADILI HAKI ZAKO KAMA MTUMIZI AMBAZO HAZIWEZI KUTENGWA CHINI YA SHERIA HUSIKA.
Uondoaji Lawama.
Unakubalina kuondolea lawama na kuchukulia wasiodhuru Uber na maafisa wake, wakurugenzi wake, wafanyakazi wake, mawakala wake kutokana na madai, hasara, dhima, na gharama zote (ikijumuisha ada za mawakili) zinazotokana na, au kuhusiana na: (i) Utumizi wako wa Huduma au huduma au bidhaa zinazopatikana kupitia utumizi wako wa Huduma; (ii) ukiukaji wako wa yoyote ya Sheria hizi; (iii) utumizi wa Uber wa Maudhui ya Mtumizi (iv) ukiukaji wako wa haki za vyonbo vingine, ikijumuisha Watoa Huduma Wengine.
6. Mali zilizopotea.
Unaelewa na kukubali kwamba ni jukumu lako kuhakikisha kuwa unaondoa mali zako kutoka kweny gari la mtoaji huduma wakati wa kuondoka. Ikitokea umeacha mali yako katika gari la mtoaji huduma, yeye anaweza kukupa mali yako au kufikisha Uber au shirika la huduma ndani ya Uber.
Ingawa unaweza kutarajia watoaji wa huduma kukupa mali yako, ofisi za Uber au shirika la huduma ndani ya Uber, uwajibikaji ni kati ya msafiri na mtoa huduma. Aidha, Uber au kipengele cha huduma ndani ya Uber hakitastahikiwa na hasara au uharibifu wa mali yako wakati unapohamia.
Wakati Uber au sehemu ya huduma ndani ya Uber itachukua hatua nzuri za kumtambua mmiliki wa mali iliyoachwa katika gari la mtoaji huduma ikiwa inarudi kwenye ofisi za Uber au shirika la huduma ndani ya Uber, wakati mali yako iko katika eneo la Uber au Uber wa ndani Umiliki, unaelewa na unakubali kwamba: (i) Uber au shirika la Uber ndani ya eneo hilo litaweka mali yako kuwa milki yake kwa kipindi cha miezi mitatu tangu tarehe ambayo Mtoaji wa Tatu alipeleka mali yako kwa Uber au Uber chombo cha huduma za ndani; Na (ii) unapaswa kushindwa kukusanya mali yako kutoka kwa Uber au sehemu ya huduma ya ndani ya Uber kabla ya muda wa kipindi cha mwezi wa tatu, Uber au shirika la huduma za ndani la Uber litakuwa na haki ya kukabiliana na mali yako kama inavyofaa na wewe Hawatakuwa na madai yoyote dhidi ya Uber au shirika la Uber ndani ya huduma kwa ajiliya mali yako isiyojulikana.
7. Sheria Inayotawlaa; Upatanishi.
Isipokuwa ibainishwe vinginevyo katika Sheria hizi, Sheria hizi zitatawaliwa kipekee, na kutekelezwa kulingana na sheria za Uholanzi, na kutenga sheria zake ambapo sheria zinakinzana. Kongamano la Vienna kuhusu Mauzo ya Bidhaa Kimataifa la 1980 (CISG) halitatumika. Mgogoro, mzozo, madai au utata wowote unaotokana na, au kwa mapana kuhusiana na au unaohusu Huduma au Sheria hizi, ikijumuisha zile zinazohusiana na uhalali wake, ujenzi wake au utekelezwaji wake ("Mgogoro" wowote) kwanza ni lazima uwasilishwa kwa kesi za ipatanishi chini ya Sheria za Upatinishi za Kituo cha Kimataifa cha Biashara ("Sheria za Upatanishi za ICC"). Ikiwa Mgogoro huo haujatatuliwa ndani ya siku sitini (60) baada ya ombi la upataishi kuwasilishwa chini ya Sheria hizo za Upatanishi za ICC, Mgogoro huo unaweza kupigwa rufaa na mwishowe kutatuliwa kwa njia ya usuluhishi pekee chini ya Sheria za Usuluhishi za Kituo cha Kimataifa cha Biashara ("Sheria za Usuluhishi za ICC"). Misimamo ya Msuluhishi wa Dharura wa Sheria za ICC hazitumiki. Mgogoro huo utasuluhishwa na msuluhishi mmoja (1) atakayeteuliwa kulingana na Sheria za ICC. Upatanishi na usuluhishi utafanyiwa mjini Amsterdam, Uholanzi, bila kupuuza haki zozote ulizo nazo chini ya Kifungu cha 18 cha Sheria ya Brussels I bis (OJ EU 2012 L351/1) na/au Kifungu cha 6:236n cha Sheria za Umma za Uholanzi. Lugha ya upatanishi na/au usuluhishi itakuwa Kiingereza, isipokuwa kama hazungumzi Kiingereza, ambapo upatanishi na/au usuluhishi utaendeshwa kwa Kiingereza na kwa lugha yako ya nyumbani. Uwepo na maudhui ya kesi za upatanishi na usuluhishi, ikijumuisha nyaraka na taarifa fupi zilizowasilishwa na wahusika, mawasiliano kutoka na kuelekea kwa Kituo cha Kimataifa cha Biashara, mawasiliano kutoka kwa mpatanishi, na mawasiliano barua, amri na tuzo zinazotolewa na mpatanishi wa pekee, zitabakia za siri na hazitafichuliwa kwa chombo kingine bila ridhaa ya moja kwa moja kwa maandishi kutoka kwa yule mhusika huyo mwingine isipokuwa: (i) ufichuzi kwa chombo kingine unahitajika katika muktadha wa kuendesha ykesi za upatanishi au usuluhishi; na (ii) chombo hicho kingine kinakubali bila masharti kwa maandishi kufungwa na jukumu la usiri lililoelezewa hapa.
8. Misimamo Mengine
Madai ya Ukiukaji wa Haki Miliki.
Madai ya Ukiukaji wa Haki Miliki yanafaa kutumwa kwa wakala mteule wa Uber. Tembelea tovuti ya Uber kwenye uber.com/legal kwa anwani teule na taarifa za ziada.
Ilani.
Uber inaweza kupeana ilani kwa njia ya ilani jumla kuhusu Huduma, barua pepe kwa anwani yako ya barua pepe iliyo katika Akaunti yako, au kwa mawasiliano ya maandishi kutumwa kwa anwani yako iliyoelezwa katika Akaunti yako. Unaweza kupa Uber ilani kwa mawasiliano ya maandishi kwa anwani ya Uber ambayo ni Burgerweeshuispad 301, 1076 HR Amsterdam, Netherlands.
Jumla.
Hauwezi kukabidhiana au kuhamisha Sheria hizi zote au sehemu yake bila kwanza kupata idhini la Uber llwa maandishi. Unapeana idhini yako kwa Uber ya kukabidhaina au kuhamisha Sheria hizi zote au sehemu yake, ikijumuisha kwa: (i) tawi au mshirika; (ii) mnunuzi wa hisa za Uber, biashara au mali; au (iii) mrithi kwa njia ya kuungana. Hakuna uhusiano wa uwekezaji pamoja, ajira au uwakala upo baina yako na Uber au Mtoa Huduma Mwingine unaotokana na kandarasi baina yako na Uber au utumizi wa Huduma.
Ikiwa msimamo wowote wa Sheria hizi utachukuliwa kuwa sio halali, ni batili au hauwezi kutekelezeka, wote au sehemu yake, chini ya sheria yoyote, msimamo huo au sehemu yake utachukuliwa kuwa sio sehemu ya Sheria hizi lakini uhalali na utekelezaji wa sehemu iliyosalia ya misimamo mingine ya Sheria hizi haitaathirika. Katika tukio ambapo, wale wahusika watabadilisha msimamo, au sehemu yake, usio halali, batili au usioweza kutekelezeka kwa msimamo, au sehemu yake, ambao ni halali au unaoweza kutekelezeka na ambao, kwa kiwango kikubwa zaidi, una athari sawia na msimamo, au sehemu yake, usio halali, batili au usioweza kutekelezeka, kulingana na maudhui na dhumuni la Sheria hizi. Sheria hizi zinajumuisha makubaliano na maelewano yote kamili ya wahusika kuhusiana na suala husika na yanachukua nafasi na kupiku makubaliano na hatua zote za awali kuhusiana na suala husika. Katika Sheria hizi, maneno "ikijumuisha" na "kujumuisha" yanamaanisha "ikijumuisha, lakini sio tu."
Kuhusu