Habari, Uber Hero.
Karibu kwenye mpango mpya unaokuwezesha kupata pesa kwa kuwaelekeza watu kwenye mfumo wa Uber.
Tutakuomba utupe hati, zikiwemo lakini si tu: nakala ya kitambulisho chako cha kitaifa, taarifa ya benki na picha ya wasifu unapojisajili kwenye Uber Hero.
Utaratibu wa Uber Hero
Ikiwa una ujuzi, Uber Hero inakupa zana. Tafuta 'waalikwa' wako na uwaweke kwenye akaunti yako ya Uber Hero. Wasaidie kukamilisha ukaguzi wa hati mbalimbali ili kuwezesha akaunti zao za madereva. Wape usaidizi na utaalamu wanapoanza kuwa madereva na wanapokamilisha idadi fulani ya safari, utapokea malipo kutoka kwa Uber.
Ukitumia Uber Hero unaweza kuanzia kiwango cha chini, lakini pia ni rahisi kukuza biashara haraka. Ni bora kwa watu wenye ari, na wanaopenda jamii.
Jipatie pesa kwa kutumia App ya Uber Hero
Kila kitu mahali pamoja
Uber Hero huhifadhi maelezo yote muhimu kadri waalikwa wako wanapokuwa madereva na kukuonesha kiasi cha pesa utakachopata dereva anapokamilisha kima cha chini cha safari.
Okoa muda kupitia mpangilio bora
Uber Hero huwapanga madereva katika vikundi vizuri. Angalia ni nani anahitaji kukamilisha ukaguzi wa hati au ambao hawatumii huduma, hali inayokuruhusu kutumia muda wako vyema.
Hufanya kazi kwenye vifaa vingi
Ukiwa ofisini au safarini—tumia Uber Hero kwenye kompyuta ya mezani au simu, wakati wowote. Unachohitaji ni kivinjari.
Usaidizi kwa Mashujaa
Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kuwa mmoja wa Uber Hero kupitia mwongozo wetu wa elimu. Kwa maswali yoyote ambayo hayajashughulikiwa, unaweza kuomba usaidizi.
Kutoka kwa miongozo ya elimu kuhusu jinsi ya kutumia App ya Uber Hero na vidokezo zaidi vya jumla kuhusu biashara.
Kuhusu