Tunakuletea ‘Trip Radar’
Kila siku tunafikiria jinsi ya kuboresha huduma zetu kwenye App ya Uber, leo hii tunafurahi kukuletea njia mpya ya kupokea safari itakayo kuongezea wewe urahisi!
“Trip Radar” ni boresho ambalo litakupa wewe na madereva wengine wa Uber Poa nafasi ya kuona na kuchagua safari zinazotokea katika maeneo uliyopo kwa wakati huo. Sasa unaweza kuona vitu vingi zaidi ili uweze kuchagua safari inayokufaa zaidi – na bado utaendelea kupata safari binafsi!
Inafanyaje kazi?
Tafuta safari
Kama haupo kwenye safari, utaona notifikesheni ya ‘Trip Radar’. Ibonyeze, utaona machaguo ya maombi ya safari yanayofanyika karibu na wewe, na una uwezo wa kulinganisha safari kulingana na sehemu ya kumchukulia/ kumshusha abiria, pamoja na nyota za abiria huyo.
Pokea Haraka
Bonyeza chaguo la safari unayoitaka kwa haraka. Madereva wengine walio karibu nawe wataona machaguo kama wewe, kwahiyo yule atakae pokea safari wa kwanza ndie atakaeipata hiyo safari.
Hakuna faini
Chagua safari unazotaka tu – kiwango chako cha kukubali safari hakita athiriwa na safari ambazo hautazipokea.
Kanusho: Taarifa zote zilizotolewa humu, kwa ufahamu bora wa Uber, zilikuwa sahihi na kamili kama wakati zinatolewa. Uber haitawajibishwa kwa taarifa yoyote isiyo kamili au isiyo sahihi. Nyenzo zilizotolewa hapa huenda zisitumike katika nchi, eneo au jiji lako. Inaweza kubadilika na inaweza kusasishwa bila taarifa. Watumiaji wa Uber App lazima wawe na umri wa miaka 18 au zaidi.
Uber