Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi

Sachin Kansal

Afisa Mkuu wa Bidhaa

Sachin Kansal ni Afisa Mkuu wa Bidhaa, anayehusika na huduma za Safari na Usafirishaji wa Bidhaa, ikijumuisha usimamizi wa bidhaa, usanifu na uendeshaji wa bidhaa. Kama sehemu ya jukumu lake, pia anasimamia mkakati wa bidhaa na teknolojia kwenye baadhi ya mipango mipya ya Uber kama vile magari yanayojiendesha, uendelevu, teksi na Uber kwa Vijana Wadogo. Alijiunga na kampuni hii mwaka 2017 kama kiongozi wa kwanza wa bidhaa akilenga zaidi teknolojia ya usalama.

Hapo awali Sachin alikuwa Makamu wa Rais wa Bidhaa huko Lookout, kampuni inayoongoza katika usalama wa vifaa vya mkononi, aliposimamia bidhaa zao za Wateja na akakuza biashara hiyo hadi kufikia zaidi ya watumiaji milioni 120. Kabla ya hapo, Sachin aliwahi kuwa Afisa Mkuu wa Bidhaa Flywheel Software, kampuni inayotoa huduma za Usafiri panapohitajika kupitia huduma ya taxicabs. Katika miaka yake ya awali ya kazi, alihudumu katika kampuni ya Palm (iliyonunuliwa na HP), kama Mkurugenzi wa Usimamizi wa Bidhaa katika masuala ya mfumo wa uendeshaji wa vifaa vya mkononi wa Palm wa webOS na programu za vifaa vya mkononi.

Sachin alihitimu na shahada ya kwanza ya uhandisi katika Chuo Kikuu cha Gujarat na shahada ya uzamili katika sayansi ya usimamizi na uhandisi katika Chuo Kikuu cha Stanford. Ameandika hati kadhaa za udhahiri katika nyanja za mawasiliano ya vifaa vya mkononi, teknolojia ya kuonyesha mahali na vyombo vya habari.

Sachin anaishi katika eneo la Bay na mke na watoto wake wawili. Katika muda wake wa ziada, anapenda kuendesha gari na kusafirisha chakula kwenye mfumo wa Uber Eats.