Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi

Ripoti ya Watu na Utamaduni ya 2021

Mwaka wa kuchukua hatua

Tangu siku za mwanzo za Uber, mwingiliano rahisi wa "bofya kitufe na uweze kusafiri" umebadilisha maisha ya watu. Na sasa umekuwa jambo la kina zaidi. Hapa Uber, tunajitahidi kufikiria upya jinsi ulimwengu unavyoendelea kuwa bora. Tunaamini kwamba kila mtu anapaswa kuwezeshwa kusafiri kwa uhuru zaidi na kwa usalama—kimwili, kiuchumi na kijamii. Ili kufanya hivyo, lazima tupambane na ubaguzi wa rangi na kuwa bingwa wa usawa kamili, ndani na nje ya kampuni yetu na kwenye tovuti yetu. Lazima tutumie ufikiaji wetu wa kimataifa, teknolojia yetu, data zetu na muhimu zaidi, sauti yetu—ili kusaidia kuunda kampuni salama, jumuishi zaidi na kuwa mshirika mkubwa kwa jumuiya zote tunazohudumia.

Mwaka 2020 ulikuwa na changamoto nyingi sana, kwani Uber na jamii zilipambana sana na athari za kiafya na kiuchumi za janga la ugonjwa na ukadiriaji wa kimataifa kuhusu mbari. Athari mbaya hazikuhisiwa kwa usawa, kwani COVID ilileta utambuzi mkali wa ukosefu wa haki ambao umeendelea kuwepo katika jamii kwa muda mrefu sana. Kupitia yote hayo, Uber imejitahidi kusaidia wafanyakazi wetu, majiji yetu na wasafiri, madereva, watu wanaosafirisha bidhaa, mikahawa na wafanyabiashara wanaotumia tovuti yetu kuungana na kazi na biashara.

Bo Young Lee, Ofisa Mkuu Anayesimamia Masuala ya Uanuwai na Ujumuishaji

"Tunajua kuwa maendeleo huchukua muda, lakini si ukosefu wa suluhisho ambao hupunguza kasi yetu; kampuni zinajitahidi kufanya maendeleo wakati hazina ujasiri wa kujizatiti na kupinga ubaguzi wa rangi na tabia za ukuu wa Watu Weupe. Watu na kampuni hupoteza motisha wakati hawaoni mabadiliko ya haraka. Lakini mabadiliko ya polepole ni endelevu zaidi. Ukosefu wa usawa na ubaguzi wa rangi haukuibuka mara moja na hauwezi kurekebishwa kwa suluhisho rahisi. Kazi haikamiliki kamwe. Ninaamini kwamba tukiendelea kujizatiti, mabadiliko yatatokea. Uber daima imekuwa na ujasiri wa kujizatiti kwa hatua endelevu na kulingana nami hayo ni mafanikio ya mwanzoni.

“Tunaishi katika nyakati zisizo za kawaida. Hebu tuhakikishe tunaboresha kwa ajili ya mabadiliko.”

Dara Khosrowshahi, Afisa Mkuu Mtendaji

“Kama kampuni inayowezesha kusafiri, lengo letu ni kuhakikisha kwamba kila mtu anaweza kusafiri kwa urahisi na kwa njia salama, iwe kimwili, kiuchumi au kijamii. Ili kufanya hivyo, lazima tusaidie kupambana na ubaguzi wa rangi ambao unaendelea katika jamii na kuwa bingwa wa usawa, ndani na nje ya kampuni yetu.

"Jambo moja ni wazi kwetu: hatuwezi tu kutumaini kwamba bidhaa zetu pekee zitaboresha usawa na haki. Lazima tutumie upana wetu wa kimataifa, teknolojia yetu na data zetu kusaidia kufanya mabadiliko, haraka—ili tuwe kampuni ya kupambana zaidi na ubaguzi wa rangi; kampuni na tovuti salama na jumuishi zaidi na mshirika mwaminifu kwa jumuiya zote tunazohudumia.”

Ahadi ya uongozi ya kuleta uanuwai

Kubuni usawa wa juu ni mojawapo ya vipaumbele 6 vya kampuni vilivyowekwa na Afisa Mtendaji Mkuu, Dara Khosrowshahi, kwa mwaka wa 2021. Hii inamaanisha kuzidisha uanuwai wa kidemografia katika Uber na kuwa kampuni ambayo haina ubaguzi wa rangi na kuwa rafiki kwa jumuiya tunazohudumia. Kila mwanachama wa Timu ya Uongozi anafanya kazi yake ili kufanikisha jambo hili, hasa kuhakikisha kwamba shirika lote linachangia. Kuzidisha uanuwai, usawa na ujumuishaji ni lengo kuu katika mikakati ya kampuni na jitihada yake huanzia juu.

Makundi ya nyenzo ya wafanyakazi wa Uber yanatoa ufahamu kuhusu utambulisho na kundi la kijamii, pamoja na fursa za ukuzaji wa uongozi kwa ajili ya wanachama.

Able at Uber

Jumuiya ya Uber ya walezi na wafanyakazi wenye ulemavu

Asian at Uber

Jumuiya ya Uber ya Asia

Black at Uber

Jumuiya ya Uber kwa ajili ya wafanyakazi na washirika Weusi

Equal at Uber

Jumuiya ya Uber kwa ajili ya ujumuishaji wa kijamii na kiuchumi

Immigrants at Uber

Jumuiya ya Uber kwa ajili ya wahamiaji

Interfaith at Uber

Jumuiya ya Uber kwa ajili ya watu wa imani na tamaduni anuwai za kiroho

Los Ubers

Jumuiya ya Uber kwa ajili ya wafanyakazi na washirika wa Kihispania na Amerika Kusini

Parents at Uber

Jumuiya ya Uber kwa ajili ya wazazi na walezi

Sages at Uber

Jumuiya ya Uber kwa ajili ya wafanyakazi wa vizazi vyote

Veterans at Uber

Jumuiya ya Uber kwa ajili ya wanajeshi waliostaafu

Women at Uber

Jumuiya ya Uber kwa ajili ya wanawake

Ripoti za Uanuwai na Ujumuishaji

1/3