
Uber, sisi hufanya jitihada usiku na mchana ili kutoa huduma iliyo bora zaidi kadri iwezekanavyo kwa madereva na abiria katika miji yote duniani kote. Lakini pia tunafahamu kuwa ni lazima kutakuwa na nyakati ambazo utahitaji kuwasiliana na sisi: mkoba umesahaulika kwenye gari, nauli isiyo sahihi, tatizo kwenye programu yako.
Unapohitaji kuwasiliana na sisi, lengo letu ni kurahisisha mchakato huu wa kuwasiliana nasi kwa uwepesi kadri iwezekanavyo ili kuweza kupata huduma inayokuridhisha.
Licha ya yote, kama unaweza kufanya safari kwa kubonyeza kitufe tu, kwanini usiweze kupata huduma nzuri ya msafiri vilevile kiganjani mwako iwapo umepata tatizo? Mrejesho? Njia rahisi ya kupata majibu kwenye programu yako.
Unahitaji kuulizia koti lako ulilopoteza ulivyotoka usiku? Unahitaji kuangalia tathmini ya msafiri wako? Wasilisha swali kuhusu risiti unayodhani haiko sawa au njia ya safari iliyo na mashaka.
Bonyeza “Usaidizi” kwenye programu na maelezo yote utakayohitaji yatakuwa hapo.
Usaidizi unaoweza kupata kwenye programu yako ni rahisi kama kuomba safari!
Posted by Uber Editor
Get a trip when you need one
Start earning in your city
Get a trip when you need one
Start earning in your city
Related articles
Most popular
Shinda Vocha za KFC na PizzaHut ukitumia App ya Uber
Pata 10% ya nauli yako ukilipia safari za Uber kwa TigoPesa!

Heshima ni kwa pande zote mbili
