Ruka uende katika maudhui ya msingi

Weka magari yako barabarani na huenda ukachuma pesa zaidi

Iwe unamiliki gari moja au msururu wa magari, unaweza kuimarisha uwezo wako wa mapato kwa kuyafanya yapatikane kwa madereva wanaotumia programu ya Uber.

LandingPage_MoneyArrowUp-Icon_Desktop_48x48-2x

Ongeza mapato yako ya magari

Iwe ndiyo kwanza unaanza au tayari uko barabarani, Uber hurahisisha kuongeza uwezo wako wa kuchuma mapato, bila kujali wingi wa magari yako.

LandingPage_Notes-Icon_Desktop_48x48-2x

Chambua utendaji wa magari

Dhibiti madereva na usaidie kuhakikisha kuwa magari mengi yapo barabarani iwezekanavyo. Unaweza kuongeza, kubadilisha, au kuondoa madereva inavyohitajika.

LandingPage_ID-Cards-Icon_Desktop_48x48-2x

Tumia rasilimali za Uber—bila malipo

Angalia salio lako, fuatilia miamala na upakue ripoti za mapato, ili uweze kufanya maamuzi yenye ufahamu zaidi.

Zana za mafanikio katika kila hatua

Fleet Hub ya Uber hukuruhusu kuanzisha biashara yako kwa urahisi, kupata magari barabarani na kukusaidia kuongeza mwonekano wa magari.

LandingPage_Step02-Car_Desktop_360x202-2x

Jisajili kwa urahisi

Jisajili mtandaoni bila malipo na usajili gari lako, ili uweze kuanza kuchuma mapato.

LandingPage_Step02-Car_Desktop_360x202-2x

Ongeza magari yako

Baada ya kujisajili, pakia hati zinazohitajika na utayarishe magari yako kwenda mtandaoni.

LandingPage_Step03-Graph_Desktop_360x202-2x

Pata takwimu za uchanganuzi

Angalia mapato yako kupitia programu na uyapakue kama ripoti ukitaka.

LandingPage_Step04-Chat_Desktop360x202-2x

Pata usaidizi unapohitajika

Tumia kitufe cha Usaidizi katika Fleet Hub ili kupata majibu ya maswali yako au kushughulikia matatizo uliyo nayo.

Anza kupata mapato kwa kutumia magari yako

Maswali yanayoulizwa sana

Je, Fleet Hub ya Uber ni nini?

Fleet Hub ni zana ya udhibiti wa msururu wa magari inayotegemea wavuti inayowaruhusu watu binafsi, wajasiriamali, na wamiliki wa biashara kudhibiti msururu wa magari yao, madereva, na mapato yao kwa urahisi kwenye mfumo wa Uber, bila gharama.

Nenda kwenye Fleet Hub

Je, kuna idadi ya chini zaidi ya magari ninayopaswa kuwa nayo ili kuanza?

Unaweza kuanza kwa gari moja. Hakuna kikomo kwa idadi ya magari unayoweza kuorodhesha kwa ajili ya kukodisha.

Ninaweza kufungua akaunti ya mtoa huduma wa Uber vipi?

Ili kujisajili kwa akaunti ya muuzaji wa Uber, bofya hapa. Kisha upakie hati zinazohitajika ili kukamilisha usajili wa msururu wa magari yako. Usajili ukishakamilika, unaweza kutumia Fleet Hub ya Uber kupata madereva na kudhibiti magari yako.

Ninaweza kupata usaidizi vipi?

Unapokuwa sehemu ya jumuiya ya Uber, unakuwa pamoja na watu wakati wote. Tumia kitufe cha Usaidizi katika Fleet Hub kupata usaidizi.

Je, ninaweza kuongeza vipi magari yangu kwa Uber?

Kwanza utahitaji kujisajili kama muuzaji hapa. Kisha pakia hati zinazohitajika ili kukamilisha usajili wa msururu wa magari yako. Usajili ukishakamilika, unaweza kutumia Fleet Hub ya Uber kuongeza magari yako.