Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi

Weka nafasi ya safari ukitumia Uber mapema katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa O'Hare

Kamilisha mipango yako leo kwa kuweka nafasi ya safari ukitumia Uber kwenda Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa O'Hare. Omba safari hadi siku 90 kabla ya safari yako ya ndege, wakati wowote na siku yoyote ya mwaka.

Mahali unakoenda
Chagua tarehe na saa

Date format is yyyy/MM/dd. Press the down arrow or enter key to interact with the calendar and select a date. Press the escape button to close the calendar.

Selected date is 2024/02/21.

10:41 AM
open

Huenda huduma ya kuweka nafasi isipatikane katika eneo lako la kuchukuliwa

Omba safari kote ulimwenguni

Bofya kitufe sasa na upate usafiri wa uwanja wa ndege katika zaidi ya vituo vikuu 700.

Safiri kama mkazi

Acha programu na dereva wako washughulikie maelezo ya kina ili usisumbuke kutafuta maelekezo katika mji usiofahamu.

Safiri bila wasiwasi ukitumia Uber

Pata vipengele unavyovipenda, ikiwemo bei za wakati halisi na malipo ya kielektroniki, hata ukiwa ugenini.

Njia za kusafiri katika eneo husika

Chukua msafiri katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa O'Hare (ORD)

Fungua programu yako ili uombe safari

Ukiwa tayari, fungua programu ya Uber ili uombe safari ya kuelekea mahali unakoenda. Chagua chaguo la usafiri wa Chicago O’Hare linalokidhi mahitaji ya idadi ya wasafiri na mizigo yenu.

Ondoka kwenye kituo

Utapata maelekezo kuhusu maeneo ya kuchukua wasafiri katika ORD moja kwa moja kwenye programu. Maeneo ya kuchukua wasafiri yanaweza kutofautiana kulingana na kituo na huduma.

Katika maombi mengi, utakutana na dereva wako wa safari ya pamoja katika eneo la Wanaoondoka kwenye Kituo cha 2.

Ili uombe safari ya Uber Black au SUV katika ORD, tafadhali kutana na dereva wako katika eneo la Wanaowasili kwenye kituo chochote.

Thibitisha mahali ulipo

Chagua kituo na eneo lako la kuchukuliwa la ORD kama ilivyobainishwa kwenye programu. Tafadhali kumbuka: eneo hili huenda lisiwe kwenye lango la kutoka lililo karibu zaidi nawe.

Jina la dereva wako, nambari ya leseni na rangi ya gari itaonyeshwa kwenye programu. Thibitisha gari lako kabla ya kuingia. Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kupitia programu.

Uwanja wa Ndege wa Chicago O'Hare Ramani

Uwanja wa Ndege wa ORD una vituo 4 vya wasafiri—Vituo vya 1, 2, 3 na 5—vilivyo na jumla ya malango 191. Kituo cha 5 kinashughulikia wanaowasili kutoka mataifa mengine.

Ramani ya O'Hare

Maswali ambayo wasafiri wanauliza sana

 • Ndiyo. Nenda kwenye orodha hii ya viwanja vya ndege kote ulimwenguni unakoweza kuomba safari ukitumia Uber.

 • Nauli ya safari ya Uber kwenda (au kutoka) kwenye Uwanja wa Ndege wa ORD inategemea hali kama vile aina ya safari unayoomba, kadirio la umbali na muda wa safari, tozo za barabarani na uhitaji wa usafiri kwa sasa.

  Unaweza kuona kadirio la bei kabla ya kuomba safari kwa kuenda hapa na kuweka eneo lako la kuchukuliwa na mahali unakoenda. Kisha, unapoomba safari utaona bei yako halisi kwenye programu kulingana na sababu za wakati halisi.

 • Maeneo ya kuchukuliwa yanategemea aina ya safari unayoomba na ukubwa wa uwanja wa ndege. Fuata maelekezo kwenye programu kuhusu mahali pa kukutana na dereva wako. Unaweza pia kutafuta ishara zinazoonyesha maeneo ya kusafiri pamoja yaliyobainishwa kwenye uwanja wa ndege.

  Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kupitia programu.

 • Hapo awali Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa O’Hare Chicago ulikuwa kiwanda cha ndege kilichoitwa Orchard Place, hii ndiyo asili ya jina fupi la uwanja huo, ORD.

Taarifa zaidi

 • Unaendesha gari ukitumia Uber?

  Kuanzia eneo la kuwachukua wasafiri hadi kufuata sheria na kanuni za mahali husika, fahamu jinsi ya kufanya safari zako za uwanja wa ndege ziwe bora zaidi.

 • Unaelekea uwanja tofauti wa ndege?

  Unaweza kushushwa na kuchukuliwa kutoka zaidi ya viwanja 700 vya ndege kote ulimwenguni.

1/2

Maelezo kwa wageni kwenye Uwanja wa Ndege wa O’Hare

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa O’Hare (ORD) ndio uwanja wa ndege wa 6 wenye shughuli nyingi zaidi ulimwenguni, unaowahudumia takribani wasafiri milioni 80 kila mwaka. O’Hare upo maili 16 (kilomita 26), mwendo wa dakika 35 kwa gari wakati hakuna msongamano wa magari au vikwazo vingine barabarani, kutoka eneo la biashara la jiji la Chicago na fukwe za Ziwa Michigan.

Vituo katika Uwanja wa Ndege wa ORD

ORD ina vituo 4: Kituo cha 1, Kituo cha 2, Kituo cha 3 na Kituo cha 5. Kumbi za Uwanja wa Ndege wa Chicago zipo katika vituo vyote. Unaweza kupanga safari yako ukitumia taarifa zilizo hapa chini.

Kituo cha 1 katika ORD

 • All Nippon
 • Lufthansa
 • United
 • Ukumbi wa United Club na Polaris

Kituo cha 2 katika ORD

 • Air Canada
 • Alaska
 • JetBlue
 • United Club

Kituo cha 3 katika ORD

 • American
 • Cape Air
 • Contour Airlines
 • Denver Air Connection/Key Lime
 • Iberia
 • Japan
 • Southern Airways Express
 • Spirit
 • Kilabu cha American Airlines Admirals na Ukumbi wa Flagship

Kituo cha 5 katika ORD

 • Aer Lingus
 • Aeroméxico
 • Air France
 • Air India
 • Air New Zealand
 • All Nippon
 • Austrian
 • British Airways
 • Cathay Pacific
 • Copa
 • Delta
 • Emirates
 • Etihad
 • Ethiopian
 • EVA Air
 • Finnair
 • Frontier
 • Icelandair
 • KLM Royal Dutch
 • Korean Air
 • LOT Polish
 • Qatar
 • Royal Jordanian
 • Scandinavian
 • Southwest
 • Sun Country
 • SWISS
 • TAP Air Portugal
 • Turkish
 • VivaAerobus
 • Volaris
 • WestJet
 • Delta Sky Club
 • Ukumbi wa SAS
 • Ukumbi wa Swissport

Kituo cha kimataifa katika ORD

Kuabiri na kuwasili kwa safari za ndege za kimataifa kwenye Uwanja wa Ndege wa O’Hare kunaweza kupatikana hasa katika Kituo cha 5, lakini baadhi ya ndege za safari za kimataifa huondoka kutoka Kituo cha 1 na 3.

Kituo chenye Matumizi Mengi (MMF)

Kituo chenye Matumizi Mengi (MMF): Kituo chenye Matumizi Mengi (MMF au Eneo la Maegesho ya Bei Nafuu F) katika 10255 W. Zemke Blvd., Chicago, IL 60666 sasa ni eneo la kuchukua wasafiri kwa mabasi ya mahali husika ikiwemo:

 • Coach USA / Van Galder
 • Express Air Coach (EAC)
 • Lafayette Limo
 • Peoria Charter Coach
 • Reindeer Shuttle
 • Wisconsin Coach USA

Kupata mlo katika Uwanja wa Ndege wa ORD

Zaidi ya maeneo 135 ya kupata chakula katika Uwanja wa Ndege wa Chicago, ikiwemo maduka ya kahawa, baa, migahawa ya vyakula vinavyotayarishwa haraka na migahawa ya Uwanja wa Ndege wa Chicago iliyo na huduma ya kulia mezani, yanapatikana kotekote katika uwanja wa ndege. Wasafiri wanaweza kupata aina mbalimbali ya vyakula katika ORD ikiwemo sushi, vyakula vya Mediterania, kuki, bisi, vyakula vya mtindo wa California, piza ya mtindo wa Naples na kadhalika.

Kusafiri kwenye Uwanja wa Ndege wa ORD

Wasafiri wanaweza kutumia mfumo wa usafiri katika Uwanja wa Ndege wa Chicago unaoitwa Airport Transit System (ATS), kusafiri. Mfumo huu wa kiotomatiki wa kusafirisha watu wenye urefu wa maili 2.5 (kilomita 4) hufanya kazi saa 24 kwa siku, ukiunganisha vituo vyote 4 na maeneo ya kuegesha ya mbali. Stesheni zimebainishwa waziwazi katika kila kituo.

Mambo ya kufanya kwenye Uwanja wa Ndege wa ORD

Uwanja wa ndege wa Chicago una vivutio mbalimbali, ikiwemo mpango wa sanaa ya umma unaojumuisha sanamu, michoro na michoro ya ukutani na maonyesho yaliyo katika maeneo mbalimbali ya uwanja wa ndege. Kielelezo cha kiunzi cha mifupa ya dinosau aina ya Brachiosaurus chenye urefu wa futi 72 (mita 22), ambacho kimeazimwa kutoka Jumba la Makumbusho la Chicago la Field, kipo katika ghorofa ya juu ya Kituo cha 1 katika Ukumbi wa B. Chumba cha yoga kilicho na sakafu endelevu ya mbao za mianzi, vioo vyenye urefu unaoanzia sakafuni hadi darini kwenye ukuta mmoja pamoja na mikeka ya mazoezi, kinapatikana kwa ajili ya matumizi katika Kituo cha 3 karibu na Urban Garden. Maduka katika Uwanja wa Ndege wa Chicago yana vibanda vya kuuzia magazeti na maduka yanayouza nguo zenye mtindo wa hali ya juu.

Kubadilisha sarafu katika Uwanja wa Ndege wa ORD

Ofisi za kubadilisha sarafu katika uwanja wa ndege wa O’Hare zipo katika maeneo yafuatayo:

 • Kituo cha 1: Malango ya B9 na C18
 • Kituo cha 2: Ukumbi mkuu
 • Kituo cha 3: Lango la K11
 • Kituo cha 5: Ghorofa za juu na chini

Hoteli zilizo karibu na Uwanja wa Ndege wa ORD

Iwe unasubiri ndege nyingine au ndege imechelewa usiku kucha au unahitaji mahali pa kukaa kwa ajili ya matembezi karibu na ORD, kuna zaidi ya hoteli na malazi 30 karibu, pamoja na hoteli nyingi za kuchagua zilizo ndani na nje ya eneo la biashara la jiji la Chicago.

Vivutio karibu na Uwanja wa Ndege wa ORD

 • Tangi la samaki la Chicago
 • Makumbusho ya sanaa ya Chicago
 • The Magnificent Mile
 • Navy Pier
 • Willis Tower

Pata taarifa zaidi kuhusu Uwanja wa Ndege wa ORD hapa.

Facebook
Instagram
Twitter

Ukurasa huu una taarifa kutoka kwenye tovuti za wahusika wengine ambazo hazidhibitiwi na Uber na zinazoweza kubadilishwa au kusasishwa kila baada ya kipindi fulani. Taarifa yoyote iliyojumuishwa kwenye ukurasa huu ambayo haihusiani moja kwa moja na Uber au uendeshaji wake ni kwa madhumuni ya kuarifu pekee na haifai kutegemewa au kufasiriwa au kuchambuliwa kwa namna inayoweka dhamana za aina yoyote, iwe zimeelezewa au kudokezewa, kuhusu taarifa iliyomo. Matakwa na vipengele fulani hutofautiana kulingana na nchi, eneo na mji.