Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hong Kong (HKG)
Je, unatafuta mbinu mbadala ya usafiri ambayo si basi la kawaida la Uwanja wa Ndege wa Hong Kong au teksi? Iwe unasafiri kutoka Uwanja wa Ndege wa Hong Kong hadi Kowloon City au kutoka Disneyland hadi Uwanja wa Ndege wa Hong Kong, fika unakoenda ukitumia programu ya Uber unayoijua tayari. Omba gari la kukupeleka na kukurudisha kutoka HKG kwa kubofya kitufe.
+852 2181-8888
Weka nafasi ya safari ukitumia Uber mapema katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hong Kong
Kamilisha mipango yako leo kwa kuweka nafasi ya safari ukitumia Uber kwenda Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hong Kong. Omba safari hadi siku 90 kabla ya safari yako ya ndege, wakati wowote na siku yoyote ya mwaka.
Omba safari kote ulimwenguni
Bofya kitufe sasa na upate usafiri wa uwanja wa ndege katika zaidi ya vituo vikuu 700.
Safiri kama mkazi
Acha programu na dereva wako washughulikie maelezo ya kina ili usisumbuke kutafuta maelekezo katika mji usiofahamu.
Safiri bila wasiwasi ukitumia Uber
Pata vipengele unavyovipenda, ikiwemo bei za wakati halisi na malipo ya kielektroniki, hata ukiwa ugenini.
Njia za kusafiri katika eneo husika
Chukua msafiri katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hong Kong (HKG)
Omba safari ukiwa tayari kuondoka
Uko katika kikundi kisichozidi wasafiri 4? Itisha UberX au Black. Mkiwa wasafiri 5 au 6 au mna mzigo, chagua UberXL.
Ondoka kupitia ukumbi wa wanaowasili
Ungependa kupata sehemu ya kuchukuliwa iliyo karibu nawe zaidi? Ukiwa katika Ukumbi wa Wanaowasili wa A, chagua Maegesho ya 4. Ukiwa katika Ukumbi wa Wanaowasili wa B, chagua Maegesho ya 1. Rejelea ramani hapa chini ili kupata maelekezo.
Mtafute dereva wako
Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kupitia programu.
Uwanja wa Ndege wa Hong Kong Ramani
Uwanja wa Ndege wa Hong Kong umegawanywa katika Kituo cha 1 na 2.
Maswali ambayo wasafiri wanauliza sana
Taarifa zaidi
Unaendesha gari ukitumia Uber?
Kuanzia eneo la kuwachukua wasafiri hadi kufuata sheria na kanuni za mahali husika, fahamu jinsi ya kufanya safari zako za uwanja wa ndege ziwe bora zaidi.
Unaelekea uwanja tofauti wa ndege?
Unaweza kushushwa na kuchukuliwa kutoka zaidi ya viwanja 700 vya ndege kote ulimwenguni.
Maelezo kwa wageni kwenye Uwanja wa Ndege wa Hong Kong
Uwanja wa Ndege wa Hong Kong Airport, ambao pia huitwa Uwanja wa Ndege wa Chek Lap Kok, ni moja kati ya viwanja vya ndege vyenye shughuli nyingi zaidi duniani, huwa unawahudumia zaidi ya wasafiri milioni 72 wanaopitia Hong Kong kila mwaka.
Vituo vya Uwanja wa Ndege wa Hong Kong
Uwanja huu una vituo 2 vilivyotenganishwa na stesheni ya MTR. Kituo cha 1 ni makao ya mashirika mengi ya ndege, huku Kituo cha 2 kikihudumia sana mashirika ya usafiri nafuu wa ndege. Unaweza kupanga safari yako ukitumia taarifa zilizo hapa chini.
Kituo cha 1
Kituo cha 1 ndicho sehemu ya kuondoka na kuwasili.
Kituo cha 2
Kituo cha 2 ni kwa ajili ya kuingia na huduma za michakato ya kuwaandaa abiria kuondoka, hakina malango au huduma za kupokea wanaowasili. Wasafiri wote walioingia kupitia Kituo cha 2 husafirishwa kuelekea katika malango ya kuondoka katika Kituo cha 1 kupitia mfumo wa chini ya ardhi.
Mambo ya kufanya katika Uwanja wa Ndege wa Hong Kong
Uwanja wa Ndege wa Hong Kong una mambo mengi ya kufanya. Wasafiri wanaotafuta kitu cha kuchangamkia wanaweza kutembelea Kituo cha Aviation Discovery, klabu ya gofu ya ndani ya Greenlive, UA IMAX @ Airport na njia ya I-Sports. Ili kupata vyakula na vinywaji katika Uwanja wa Ndege wa Hong Kong, kuna chaguo tele, ipo migahawa ya vyakula vya kufungashiwa, mapishi ya Kifaransa, Kiasia na mengine mengi.
Kubadilisha sarafu katika Uwanja wa Ndege wa Hong Kong
Ukiwa katika Uwanja wa Ndege wa Hong Kong, unaweza kupata vituo vingi vya Global Exchange kwa ajili ya kubadilisha hela zako.
Hoteli zilizo karibu na Uwanja wa Ndege wa Hong Kong
Kuna hoteli kadhaa zilizo hatua ya kutembea au usafiri wa muda mfupi kwa basi kutoka katika uwanja wa ndege. Ukiamua kuvinjari jijini, unaweza kupata hoteli na sehemu za kulala mwendo wa karibu kwa gari.
Maeneo ya kuvutia karibu na Uwanja wa Ndege wa Hong Kong
- Bustani ya Lantau Country
- Lantau Trail
- Gari la kamba la Ngong Ping 360
- Tian Tan Buddha
- Wisdom Path
Pata maelezo zaidi kuhusu Uwanja wa Ndege wa Hong Kong (HKG) hapa.
Ukurasa huu una taarifa kutoka kwenye tovuti za wahusika wengine ambazo hazidhibitiwi na Uber na zinazoweza kubadilishwa au kusasishwa kila baada ya kipindi fulani. Taarifa yoyote iliyojumuishwa kwenye ukurasa huu ambayo haihusiani moja kwa moja na Uber au uendeshaji wake ni kwa madhumuni ya kuarifu pekee na haifai kutegemewa au kufasiriwa au kuchambuliwa kwa namna inayoweka dhamana za aina yoyote, iwe zimeelezewa au kudokezewa, kuhusu taarifa iliyomo. Matakwa na vipengele fulani hutofautiana kulingana na nchi, eneo na mji.
Kampuni