Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi

Weka nafasi ya safari ukitumia Uber mapema katika Uwanja wa Ndege wa Kaunti ya Detroit Metropolitan Wayne

Kamilisha mipango yako leo kwa kuweka nafasi ya safari ukitumia Uber kwenda Uwanja wa Ndege wa Kaunti ya Detroit Metropolitan Wayne. Omba safari hadi siku 30 kabla ya safari yako ya ndege, wakati wowote na siku yoyote ya mwaka.

Mahali unakoenda
Chagua tarehe na saa

Date format is yyyy/MM/dd. Press the down arrow or enter key to interact with the calendar and select a date. Press the escape button to close the calendar.

Selected date is 2023/09/29.

4:19 PM
open

Huenda huduma ya kuweka nafasi isipatikane katika eneo lako la kuchukuliwa

Omba safari kote ulimwenguni

Bofya kitufe sasa na upate usafiri wa uwanja wa ndege katika zaidi ya vituo vikuu 600.

Safiri kama mkazi

Acha programu na dereva wako washughulikie maelezo ya kina ili usisumbuke kutafuta maelekezo katika mji usiofahamu.

Safiri bila wasiwasi ukitumia Uber

Pata vipengele unavyovipenda, ikiwemo bei za wakati halisi na malipo ya kielektroniki, hata ukiwa ugenini.

Njia za kusafiri katika eneo husika

 • UberX

  1-4

  Safari za bei nafuu, kila siku

 • Raha

  1-4

  Magari mapya zaidi yaliyo na nafasi ya kutosha

 • Starehe Electric

  1-4

  Magari ya Premium yasiyo na uchafuzi

 • UberXL

  1-6

  Affordable rides for groups up to 6

 • Uber Pet

  1-4

  Affordable rides for you and your pet

 • Connect

  1-4

  Send packages to friends & family

1/6

Chukua msafiri katika Uwanja wa Ndege wa Kaunti ya Detroit Metropolitan Wayne (DTW)

Fungua programu yako ili uombe safari

Ukiwa tayari, fungua programu ya Uber ili uombe safari ya kuelekea mahali unakoenda. Chagua chaguo la usafiri wa uwanja wa ndege wa DTW linalokidhi mahitaji ya idadi ya wasafiri na mizigo yenu.

Fuata ishara ya kuelekea Ground Transportation Center

Utapata maelekezo kuhusu maeneo ya kuchukuliwa katika Uwanja wa Ndege moja kwa moja kwenye programu. Pata ishara za Kusafiri Pamoja kwenye uwanja wa ndege wa GTC.

Kutana na dereva wako

Nenda kwenye eneo lako la kuchukuliwa la DTW kama ilivyobainishwa kwenye programu. Tafadhali kumbuka: eneo hili huenda lisiwe kwenye lango la kutoka lililo karibu zaidi nawe. Jina la dereva wako, nambari ya leseni na rangi ya gari itaonyeshwa kwenye programu. Thibitisha gari lako kabla ya kuingia. Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kupitia programu.

Uwanja wa Ndege wa Detroit Ramani

Uwanja wa Ndege wa Detroit una vituo 2 vikuu. Kituo cha McNamara kina Ukumbi wa A-C, huku Kituo cha Kaskazini kikiwa na Ukumbi wa D.

Ramani ya Uwanja wa Ndege wa Detroit

Maswali ambayo wasafiri wanauliza sana

 • Ndiyo. Bonyeza hapa ili uone orodha ya viwanja vya ndege kote duniani unakoweza kuitisha usafiri wa Uber.

 • Nauli ya usafiri wa Uber kuenda (au kutoka) Uwanja wa Ndege wa DTW inategemea hali kama vile aina ya usafiri, kadirio ya umbali na muda wa safari, ada ya vibali barabarani na idadi ya maombi ya usafiri.

  Unaweza kuona kadirio la bei kabla ya kuitisha usafiri kwa kuweka eneo la kuchukuliwa na mahali unakoenda katika zana ya kukadiria nauli katika Uber hapo juu. Kisha, unapoitisha usafiri utaona nauli yako halisi kwenye app kwa kutegemea hali za wakati huo.

 • Maeneo ya kuchukuliwa yanategemea aina ya usafiri unaoitisha na ukubwa wa uwanja wa ndege. Fuata maagizo kwenye App kuhusu eneo utakakomkuta dereva wako. Unaweza pia kuangalia mabango yanayoashiria maeneo ya usafiri wa pamoja yaliyobainishwa kwenye uwanja wa ndege.

  Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kupitia programu.

Taarifa zaidi

 • Unaendesha gari ukitumia Uber?

  Kuanzia eneo la kuwachukua wasafiri hadi kufuata sheria na kanuni za mahali husika, fahamu jinsi ya kufanya safari zako za uwanja wa ndege ziwe bora zaidi.

 • Unaelekea uwanja tofauti wa ndege?

  Unaweza kushushwa na kuchukuliwa kutoka zaidi ya viwanja 600 vya ndege kote ulimwenguni.

1/2

Maelezo kwa wageni kwenye Uwanja wa Ndege wa Detroit

Uwanja wa Ndege wa Kaunti ya Detroit Metropolitan Wayne (DTW) ndio uwanja wenye shughuli nyingi mno katika eneo la Michigan na moja ya maeneo yenye shughuli nyingi za usafiri wa ndege nchini Marekani. DTW upo takribani maili 20 (kilomita 32) katikati ya jiji la Detroit (mwendo wa takribani dakika 30 kwa gari wakati hakuna foleni au vikwazo vingine barabarani). Uwanja unaweza kufikika kwa wasafiri wanaoenda au kutoka katika miji ya Detroit, Lake Michigan na Toledo katika jimbo jirani la Ohio.

Vituo katika Uwanja wa Ndege wa Detroit

Uwanja wa Ndege wa DTW una vituo 2 vikuu: Kituo cha McNamara na Kituo cha North. Kituo cha McNamara kimegawanywa katika kumbi 3: A, B na C. Kituo cha North kina ukumbi mmoja: D. Unaweza kupanga safari yako ukitumia taarifa zilizo hapa chini.

Kituo cha McNamara katika DTW

 • Aeroméxico
 • Air France
 • Delta

Kituo cha North katika DTW

 • Air Canada
 • Alaska
 • American
 • Frontier
 • JetBlue
 • Lufthansa
 • Royal Jordanian
 • Kusini Magharibi
 • Spirit
 • United
 • Wow
 • Lufthansa Club

Kituo cha Kimataifa katika DTW

Safari za kimataifa za Uwanja wa Ndege wa Detroit hufika na kuondoka katika vituo vyote viwili vya McNamara na North. Kituo cha McNamara kina malango 12 yanayotumiwa kwa ajili ya safari za kuondoka na kuwasili, na Kituo cha North kina malango 26. DTW huwa na safari za moja kwa moja kuelekea zaidi ya maeneo 30 ya kimataifa.

Kupata chakula katika Uwanja wa Ndege wa Detroit

Uwanja wa Ndege wa Detroit unakupa chaguo nyingi za kupata chakula, kuna zaidi ya maeneo 100 kati ya vituo hivyo 2, yakiwemo maduka ya kahawa, migahawa inayouza vyakula vya kufangashiwa na migahawa iliyo na huduma za kulia mezani. Vilevile, Uwanja wa Ndege wa Detroit una baa zilizo katika sehemu mbalimbali za vituo.

Kusafiri katika Uwanja wa Ndege wa Detroit

Vituo vyote viwili vya Uwanja wa Ndege wa Detroit vina mikanda ya kutembelea inayojisogeza yenyewe. Kuna ExpressTram katika Ukumbi wa A katika Kituo cha McNamara, huu ni mfumo wa uchukuzi ambao huwasafirisha abiria kwa umbali wa maili 3 kati ya vituo 3 ambapo mfumo wenyewe upo ifuatavyo:

 • Stesheni ya Kituo: hiki ipo katikati ya ukumbi na unaweza kufikia malango kuanzia A29 hadi A55, eneo la kuingia, sehemu ya kuchukua mizigo, usafiri wa ardhini na njia ya chini kwa chini inayoelekea Kumbi za B na C
 • Stesheni South: inafanikisha usafiri kwenda malango ya A1 hadi A28
 • Stesheni ya North: inafanikisha usafiri kwenda malango ya A56 hadi A78

Isitoshe, abiria wanaweza kusafiri kwa mabasi kati ya vituo vya North na McNamara. Mabasi yanayohudumu kwenye uwanja wa ndege wa Detroit hutoka kila baada ya dakika 10 kutoka kwenye vituo vya usafiri wa ardhini na kwenye lango la Westin Hotel.

Mambo ya kufanya katika Uwanja wa Ndege wa Detroit

Kuna vivutio vingi vya kufurahia na shughuli za kufanya katika Uwanja wa Ndege wa DTW. Wasafiri wanaotafuta shughuli za kujituliza wanaweza kukandwa, kupambwa uso, kupata matunzo ya makucha ya miguu na mikono katika spaa iliyo kwenye uwanja wa ndege. Uwanja wa Ndege wa Detroit una maduka ya majarida, vipodozi na maduka ya nguo. Tundu lenye mwangaza lililo katika muunganisho kati ya njia ya A, B na C hucheza onesho la mwangaza na muziki kwa urari.

Kubadilisha sarafu katika Uwanja wa Ndege wa Detroit

Ofisi za kubadilisha fedha katika uwanja wa ndege wa Detroit zipo katika maeneo yafuatayo: - Kituo cha McNamara: sehemu ya kuondoka (Central Link karibu na Lango la A38) na katika sehemu ya wanaoondoka kuelekea safari za kimataifa - Kituo cha North: sehemu ya kuondoka (moja kwa moja kutoka Lango la D9) na katika eneo la wanaowasili (karibu na sehemu ya kuchukua mizigo)

Hoteli zilizo karibu na Uwanja wa Ndege wa Detroit

Iwe unasubiri ndege nyingine au ndege imechelewa usiku kucha, au kama unahitaji mahali pa kukaa karibu na DTW, kuna zaidi ya hoteli nyingi na maeneo ya kulala karibu, katika maeneo ya Dearborn na jijini Detroit.

Sehemu za kuvutia karibu na Uwanja wa Ndege wa Detroit

 • Belle Isle Park
 • Eastern Market
 • Ford Field
 • Jumba la makumbusho la Detroit kuhusu muziki wa Motown

Pata maelezo zaidi kuhusu Uwanja wa Ndege wa DTWhapa.

Facebook
Instagram
Twitter

Ukurasa huu una taarifa kutoka kwenye tovuti za wahusika wengine ambazo hazidhibitiwi na Uber na zinazoweza kubadilishwa au kusasishwa kila baada ya kipindi fulani. Taarifa yoyote iliyojumuishwa kwenye ukurasa huu ambayo haihusiani moja kwa moja na Uber au uendeshaji wake ni kwa madhumuni ya kuarifu pekee na haifai kutegemewa au kufasiriwa au kuchambuliwa kwa namna inayoweka dhamana za aina yoyote, iwe zimeelezewa au kudokezewa, kuhusu taarifa iliyomo. Matakwa na vipengele fulani hutofautiana kulingana na nchi, eneo na mji. Uokoaji wa pesa kwenye ofa unatumika kwa watumiaji wapya pekee. Huwezi kutumia ofa hii pamoja na ofa nyinginezo na haiwezi kutumiwa katika bakshishi. Inapatikana kwa muda mfupi. Ofa na masharti yanaweza kubadilika.