Ruka uende katika maudhui ya msingi
Uber
Uber

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Toronto Pearson (YYZ)

Tumia Uber kwenda popote, iwe unasafiri kutoka Uwanja wa Ndege wa YYZ kwenda katikati ya mji au kutoka North York kurudi kwenye Uwanja wa Ndege.

6301 Silver Dart Drive, Mississauga, ON, L5P 1B2, Canada
+1 416-247-7678

Bonyeza tu kitufe ili upate usafiri wa angani katika zaidi ya viwanja vikuu 500.

Acha programu na dereva wako ashughulikie masuala ya kina ili usisumbuke kutafuta maelekezo katika jiji ambapo wewe ni mgeni.

Pata vipengele unavyovipenda, ikiwa ni pamoja na bei zinazooneshwa moja kwa moja na uwezo wa kulipa bila pesa taslimu, hata ukiwa ugenini.

Sampuli za bei za msafiri ni makadirio tu na hazioneshi mabadiliko yanayotokana na mapunguzo, kucheleweshwa kwenye foleni na mambo mengine. Tunaweza kutumia nauli isiyobadilika na bei za chini zaidi. Bei halisi zinaweza kubadilika.

 • Usafiri wa pamoja, bei nafuu

 • Affordable, everyday rides

Chagua aina ya gari linalotosha idadi ya wasafiri na mizigo mliyo nayo. Ukiombwa na programu, chagua eneo la kuchukuliwa kisha ufuate ishara kwenye uwanja wa ndege hadi “Ride App Pickups.”

Kwa UberX na UberXL

 • Ukiwa katika Kituo cha 1, dereva wako atakupata ghorofa ya chini kwenye daraja la chini nje ya Mlango wa Q. Tafuta eneo samawati kando ya barabara.

 • Ukiwa katika Kituo cha 3, dereva wako atakupata katika Daraja la Wanaowasili nje ya Mlango wa D kwenye eneo la nje kando ya barabara. Fuata mabango ili uvuke mtaa kisha usubiri kwenye sehemu ya samawati kando ya barabara kwenye Eneo la 3.

Kwa Uber Black, Select na SUV

 • Ukiwa katika Kituo cha 1, dereva wako atakupata kwenye Daraja la Wanaowasili nje ya Mlango wa A.

 • Kwa Kituo cha 3, mpate dereva wako katika Ghorofa ya Wanaowasili nje ya Mlango wa A Safu ya 9.

Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kupitia programu.

Ikiwa unapanga safari ya kwenda Uwanja wa Ndege wa Toronto na unatarajia kuendesha gari, unaweza kupata ada za maegesho hapa.

Aina ya maegesho

Maegesho ya Muda Mfupi

Mhudumu wa Kuegesha

Maegesho ya Kulipia kwa Siku

Value Park Garage

Value Park Lot

Ada

$50 kila siku
$40 kila siku
$30 kila siku
$25 kila siku
$20 kila siku
Huenda ada za maegesho zikawa zimebadilika; taarifa hii iliwekwa Tarehe 17 Desemba, 2018.
Uwanja wa Ndege wa Toronto una vituo 2, Kituo cha 1 na 3. Vituo hivi viwili vina uwezo wa kuhudumia safari za ndege za nchini, za nchi zinazopakana na za kimataifa.
 • Chagua Toronto Pearson Wi-Fi kwenye orodha mitandao
 • Weka alama kwenye kisanduku kuonesha kwamba unakubali vigezo na masharti yote
 • Bonyeza kitufe cha kijani kwenye ukurasa wa kuanza

Unaweza kupata SIM kadi kutoka sehemu ya kuuzia magazeti iliyo katika eneo la wasafiri wanaoondoka kuelekea Marekani katika Vituo vya 1 na 3. Unaweza kupata kadi za muda mrefu kutoka 7-Eleven katika Kituo cha 1 na katika maegesho ya Value Park.

Ikiwa mko wengi na mna mizigo mingi au ungependa nafasi kubwa, tunakushauri utumie uberXL.

Ndiyo. Bonyeza hapa ili uone orodha ya viwanja vya ndege kote duniani unakoweza kuitisha usafiri wa Uber.

Nauli ya usafiri wa Uber kuenda (au kutoka) Uwanja wa Ndege wa YYZ inategemea hali kama vile aina ya usafiri, kadirio ya umbali na muda wa safari, ada ya vibali barabarani na idadi ya maombi ya usafiri.

Unaweza kuona kadirio la bei kabla ya kuitisha usafiri kwa kuweka eneo la kuchukuliwa na mahali unakoenda katika zana ya kukadiria nauli katika Uber hapo juu. Kisha, unapoitisha usafiri utaona nauli yako halisi kwenye programu kwa kutegemea hali za wakati huo.

Maeneo ya kuchukuliwa huenda yakategemea aina ya usafiri unaoitisha na ukubwa wa uwanja wa ndege. Fuata maagizo kwenye programu kuhusu eneo utakakomkuta dereva wako. Unaweza pia kuangalia mabango yanayoashiria maeneo ya usafiri wa pamoja yaliyobainishwa kwenye uwanja wa ndege.

Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kupitia programu.

Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kurahisisha huduma unayopokea katika viwanja vya ndege, zikiwemo sheria na kanuni za nchi husika.
Unaweza kupelekwa na kuchukuliwa kutoka zaidi ya viwanja 500 vya ndege kote duniani.

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Toronto Pearson (YYZ) ndio uwanja wenye shughuli nyingi zaidi nchini Kanada, huku ukiwahudumia zaidi ya wasafiri milioni 47 kila mwaka. Uwanja huu uko karibu na katikati ya jiji la Mississauga, na kilomita 23 (maili 14) kutoka katikati ya jiji la Toronto, takribani dakika 20 kwa kuendesha gari wakati hakuna foleni au vikwazo vingine barabarani.

Vituo katika Uwanja wa Ndege wa Toronto Airport

Uwanja wa Ndege wa YYZ una vituo 2: Kituo cha 1 na Kituo cha 3, vyote vikiwa na malango 104. Kumbi za Uwanja wa Ndege wa Toronto zinaweza kupatikana katika vituo vyote viwili. Unaweza kupanga safari yako ukitumia taarifa zilizo hapa chini.

Kituo cha 1 katika YYZ

 • Air Canada
 • Air Canada Rouge
 • Air China
 • Air New Zealand
 • All Nippon
 • Asiana
 • Austrian
 • Avianca
 • Brussels
 • Copa
 • Egyptair
 • Emirates
 • Ethiopian
 • EVA
 • LOT
 • Lufthansa
 • SAS
 • Singapore
 • SWISS
 • THAI
 • TAP Air Portugal
 • Turkish
 • United
 • Ukumbi wa Air Canada Maple Leaf
 • Ukumbi wa Plaza Premium

Kituo cha 3 katika YYZ

 • Aer Lingus
 • Aeroméxico
 • Air France
 • Air Transat
 • Alaska
 • American
 • Azores
 • British Airways
 • Caribbean
 • Cathay Pacific
 • China Eastern
 • China Southern
 • Condor
 • Cubana
 • Delta
 • El Al
 • Etihad
 • Flair
 • Fly Jamaica
 • Hainan
 • Iberia
 • Icelandair
 • Interjet
 • Japan
 • Jet Airways
 • KLM
 • Korean Air
 • LAN
 • Miami Air International
 • Pakistan International
 • Philippine
 • Qantas
 • Saudia
 • Sunwing
 • Ukraine International
 • WestJet
 • Air France–KLM Lounge
 • American Airlines Admirals Club
 • Ukumbi wa Plaza Premium

Vituo vya kimataifa katika YYZ

Safari za kimataifa katika Uwanja wa Ndege wa Toronto zinaweza kuabiriwa katika Vituo vyote viwili vya 1 na 3. YYZ huwa na safari za moja kwa moja kuelekea zaidi ya maeneo 90 ya kimataifa.

Kupata chakula katika Uwanja wa Ndege wa Toronto

YYZ una zaidi ya maeneo 45 katika vituo vyote viwili, yakiwemo ya kuuza vyakula vya kufungashiwa, baa na migahawa iliyo na huduma ya kulia mezani. Sehemu ya kula katika Uwanja wa Ndege wa Toronto ipo katika kituo cha 1 kwenye ghorofa la chini kabisa.

Kusafiri ukiwa katika Uwanja wa Ndege wa Toronto

Wasafiri katika YYZ wanaweza kutumia Link Train, ambao ni mfumo wa kiotomatiki wa kutoa safari za bila malipo katika Uwanja wa Ndege wa Toronto kati ya Kituo cha 1, Kituo cha 3, maegesho, na hoteli ya uwanja wa ndege.

Mambo ya kufanya ukiwa katika Uwanja wa Ndege Toronto

Toronto Pearson ina kitengo cha kudumu cha kuoneshea kazi za sanaa zilizokusanywa kutoka kwa wasanii kote duniani. Unaweza kuona sanaa hizo katika maeneo yote ya uwanja wa ndege. Katika sehemu ya kuondoka katika Kituo cha 3, utapata sehemu ya kukandwa katika Uwanja wa Ndege wa Toronto, Kadhalika kuna saluni kwa ajili ya mapambo ya kucha katika Kituo cha 1 karibu na malango ya Daraja la 2. Maeneo ya watoto kuchezea yapo kati ya Malango ya 24 na 26 katika Kituo cha 1. Ili kuwafaa wasafiri wanaotaka kununua vitu, Uwanja wa Ndege wa Toronto una maduka ya kuuza zawadi, bidhaa zisizotozwa ushuru na bidhaa za mitindo ya juu.

Kubadilisha fedha katika Uwanja wa Ndege wa Toronto

Unaweza kupata ofisi za kubadilisha fedha katika maeneo yafuatayo kwenye Uwanja wa Ndege wa Toronto:

 • Kituo cha 1: Daraja la 1 wanaowasili
 • Kituo cha 1: Malango ya Daraja la 2
 • Kituo cha 1: Sehemu ya kuingia katika Daraja la 3
 • Kituo cha 3: sehemu ya wanaoondoka
 • Kituo cha 3: sehemu ya wanaowasili

Hoteli zilizo karibu na Uwanja wa Ndege wa Toronto

Iwe unasubiri ndege nyingine au ndege imechelewa usiku kucha, au kama unahitaji mahali pa kukaa karibu na YYZ, kuna zaidi ya hoteli 30 na maeneo ya kulala karibu.

Vivutio karibu na Uwanja wa Ndege wa Toronto

 • CN Tower
 • Distillery District
 • St. Lawrence Market
 • Visiwa vya Toronto

Pata maelezo zaidi kuhusu Uwanja wa Ndege wa Toronto hapa.

Facebook
Instagram
Twitter