Ruka uende katika maudhui ya msingi

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Norman Y. Mineta San Jose (SJC)

Iwe unatoka Uwanja wa Ndege wa San Jose kwenda San Francisco au katikati ya mji wa San Jose, utapata gari la kukusafirisha kutoka au kwenda uwanja wa ndege wakati wowote

1701 Airport Boulevard, San Jose, CA 95110
+1 408-392-3600

Njia bora zaidi ya kusafiri

Itisha usafiri kote ulimwenguni

Bonyeza tu kitufe ili upate usafiri wa angani katika zaidi ya viwanja vikuu 500.

Safiri kama mwenyeji

Acha App na dereva wako ashughulikie masuala ya kina ili usisumbuke kutafuta maelekezo katika jiji ambapo wewe ni mgeni.

Safiri bila wasiwasi kwa kutumia Uber

Pata vipengele unavyovipenda, ikiwa ni pamoja na bei zinazooneshwa moja kwa moja na uwezo wa kulipa bila pesa taslimu, hata ukiwa ugenini.

Punguzo la hadi $15

Pata punguzo la $5 kwenye safari zako tatu za kwanza. Tumia kuponi ya ofa NEWRIDER15. Muda wa kuitumia unakwisha siku 30 baada ya kuweka kuponi ya ofa kwenye akaunti yako ya Uber.

Aina za usafiri ukiwa eneo husika

 • UberX

  1-3

  Affordable rides, all to yourself

 • Comfort

  1-3

  Newer cars with extra legroom

 • UberXL

  1-5

  Affordable rides for groups up to 5

 • Uber Green

  1-3

  Low-emission rides

 • Connect

  1-4

  Send packages to friends & family

 • Pool - Unavailable

  1-2

  Temporarily unavailable

1/6

Kupata gari kwenye Uwanja wa Ndege wa San Jose

Ita gari ukiwa tayari kutoka nje

Na uchague gari linalotoshea wasafiri na mizigo mliyo nayo.

Ondoka kwenye eneo la wanaowasili au sehemu ya kuchukua mizigo

Elekea nje na ufuate mabango hadi kwenye eneo la kuchukua wanaosafiri kwa pamoja. Hapa ndipo madereva wote washirika wa Uber katika uwanja wa ndege wa SJC huwapata na kuwachukua wasafiri.

Kwa uchukuzi wa Kituo cha A, kutana na dereva wako nje ya sehemu ya kuchukua mizigo, kwenye Kituo cha 1. Kwa uchukuzi kwenye Vituo cha A, kutana na dereva wako katika kisiwa cha trafiki, Kituoni cha 9.

Mtafute dereva wako

Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana na yeye kupitia programu ili umthibitishie mahali ulipo.

Ramani ya Uwanja wa Ndege wa San Jose

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa San Jose una vituo 2: Upande wa kuabiri uliounganisha Kituo cha A na B. Vituo vya A na B vinashughulikia wanaowasili kutoka safari za kimataifa.

Maswali ambayo wasafiri wanauliza sana

 • Ndiyo. Bonyeza hapa ili uone orodha ya viwanja vya ndege kote duniani unakoweza kuitisha usafiri wa Uber.

 • Nauli ya usafiri wa Uber kuenda (au kutoka) Uwanja wa Ndege wa SJC inategemea hali kama vile aina ya usafiri, kadirio ya umbali na muda wa safari, ada ya vibali barabarani na idadi ya maombi ya usafiri.

  Unaweza kuona kadirio la bei kabla ya kuitisha usafiri kwa kuweka eneo la kuchukuliwa na mahali unakoenda katika zana ya kukadiria nauli katika Uber hapo juu. Kisha, unapoitisha usafiri utaona nauli yako halisi kwenye app kwa kutegemea hali za wakati huo.

 • Maeneo ya kuchukuliwa yanategemea aina ya usafiri unaoitisha na ukubwa wa uwanja wa ndege. Fuata maagizo kwenye App kuhusu eneo utakakomkuta dereva wako. Unaweza pia kuangalia mabango yanayoashiria maeneo ya usafiri wa pamoja yaliyobainishwa kwenye uwanja wa ndege.

  Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kupitia programu.

Maelezo zaidi

Unatumia mfumo wa Uber kuendesha gari?

Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kurahisisha huduma unayopokea katika viwanja vya ndege, zikiwemo sheria na kanuni za nchi husika.

Je, unaelekea uwanja tofauti wa ndege?

Unaweza kupelekwa na kuchukuliwa kutoka zaidi ya viwanja 600 vya ndege kote duniani.

Maelezo kwa wageni kwenye Uwanja wa Ndege wa San Jose

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mineta San Jose (SJC) ndio uwanja wa ndege unaokua kwa kasi zaidi nchini Marekani kwa kuzingatia idadi ya wasafiri, huku ukiwahudumia zaidi ya abiria milioni 12.5 kila mwaka. Uwanja upo takribani maili 4 (kilomita 6) kutoka katikati ya jiji la San Jose, ni mwendo wa dakika 8 kwa gari wakati hakuna foleni au vikwazo vingine barabarani.

Vituo katika Uwanja wa Ndege wa San Jose

Uwanja wa Ndege wa SJC umegawanywa katika vituo 2, A na B, ukiwa na jumla ya malango 31 ya kupanda katika vituo hivyo viwili. Kumbi za Uwanja wa Ndege wa San Jose zinapatikana katika Kituo cha A. Unaweza kupanga safari yako ukitumia taarifa zilizo hapa chini.

Kituo cha A katika SJC

 • Aeroméxico
 • Air Canada
 • American
 • ANA
 • California Pacific
 • Delta
 • Frontier
 • Hawaiian
 • JetBlue
 • United
 • Volaris
 • The Club at SJC

Kituo cha B katika SJC

 • Alaska
 • British Airways
 • Hainan
 • Kusini magharibi

Kituo cha kimataifa katika SJC

Safari za kimataifa katika Uwanja wa Ndege wa San Jose huanzia katika vituo vyote viwili. Uwanja wa Ndege wa SJC hutoa usafiri wa moja kwa moja kuelekea maeneo 16 ya kimataifa.

Kupata mlo katika Uwanja wa Ndege wa San Jose

Wasafiri wanaweza kuchagua miongoni mwa chaguo 30 za milo katika SJC, ikiwemo migahawa inayouza vyakula vya kufungashiwa, baa na migahawa iliyo na huduma ya kulia mezani. Unaweza kununua vyakula na vinywaji katika vituo vyote viwili katika Uwanja wa Ndege wa San Jose.

Kusafiri katika Uwanja wa Ndege wa San Jose

Wasafiri katika uwanja wa ndege wa SJC wanaweza kutumia mabasi ya uwanja wa ndege. Mabasi ya Uwanja wa Ndege wa San Jose huzunguka kila wakati kati ya Kituo cha A, Kituo cha B, na sehemu za maegesho. Mabasi huondoka kila baada ya dakika 7 hadi 10 kutoka kila kituo, sehemu ya magari ya kukodisha na Maegesho ya Daily Lot 4.

Mambo ya kufanya ukiwa katika Uwanja wa Ndege wa San Jose

SJC una mradi wa sana ambao unaonesha wajibu wa eneo kama kituo cha kimataifa cha teknolojia na uvumbuzi. Kuna kazi za sanaa katika ukumbi wa Kituo cha B cha wanaowasili, South Concourse na kwenye ghorofa ya mezzanine. Kuna piano katika Blue Dot katika Kituo cha A na sehemu ya kuchukua mizigo katika Kituo cha B. Uwanja wa Ndege wa San Jose una maeneo 24 kwa ajili ya shughuli za ununuzi katika vituo vyote viwili, yanayouza vipodozi, mapambo na vifaa vya kielektroniki. Uwanja una mbwa 23 wa kuliwaza ambao husaidia kuwatuliza wasafiri walio na mihemko kabla ya kupaa.

Kubadilisha fedha katika Uwanja wa Ndege wa San Jose

Ofisi za kubadilisha fedha katika uwanja wa ndege wa San Jose zipo katika Kituo cha A karibu na Lango la 15 na sehemu ya kuchukua mizigo.

Hoteli zilizo karibu na Uwanja wa Ndege wa San Jose

Iwe unasubiri ndege nyingine au ndege imechelewa usiku kucha, au kama unahitaji mahali pa kukaa karibu na SJC, kuna zaidi ya hoteli 25 na maeneo ya kulala karibu.

Maeneo ya kuzuru karibu na Uwanja wa Ndege wa San Jose

 • Bustani za Ufuo wa Guadalupe River
 • Mexican Heritage Plaza
 • Majumba ya makumbusho ya historia ya teknolojia katika San Jose

Pata maelezo zaidi kuhusu Uwanja wa Ndege wa San Jose hapa.

Facebook
Instagram
Twitter

Ukurasa huu una taarifa kutoka kwenye tovuti za washirika wengine ambazo hazisimamiwi na Uber na zinaweza kugeuzwa au kubadilishwa mara kwa mara. Maelezo yoyote yaliyojumuishwa kwenye ukurasa huu ambayo hayahusiani moja kwa moja na Uber au kazi zake yanatumika kuarifu tu na hayafai kutegemewa, au kuchukuliwa au kufasiliwa kwa namna inayoweka dhamana ya aina yoyote, iwe ya moja kwa moja au inayokisiwa, kuhusu maelezo yaliyo hapa. Baadhi ya masharti na vipengele hutofautiana kutegemea nchi, eneo na jiji. Ofa ya punguzo inawalenga watumiaji wapya pekee. Huwezi kutumia ofa hii pamoja na ofa nyinginezo na haiwezi kutumiwa katika bakshishi. Inapatikana kwa muda mfupi. Vigezo na masharti ya ofa vinaweza kubadilika.