Ruka uende katika maudhui ya msingi
Uber
Uber

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Seattle-Tacoma (SEA)

Tumia Uber kusafiri popote, iwe unasafiri kutoka Uwanja wa Ndege wa Sea-Tac hadi Space Needle au kutoka Pike Place Market hadi Sea-Tac.

17801 International Boulevard, Seattle, WA 98158
+1 206-787-5388

Njia bora zaidi ya kusafiri

Itisha usafiri kote ulimwenguni

Bonyeza tu kitufe ili upate usafiri wa angani katika zaidi ya viwanja vikuu 500.

Safiri kama mwenyeji

Acha App na dereva wako ashughulikie masuala ya kina ili usisumbuke kutafuta maelekezo katika jiji ambapo wewe ni mgeni.

Safiri bila wasiwasi kwa kutumia Uber

Pata vipengele unavyovipenda, ikiwa ni pamoja na bei zinazooneshwa moja kwa moja na uwezo wa kulipa bila pesa taslimu, hata ukiwa ugenini.

Mfumo wa Uber wa kukadiria nauli

Sampuli za bei za msafiri ni makadirio tu na hazioneshi mabadiliko yanayotokana na mapunguzo, kucheleweshwa kwenye foleni na mambo mengine. Tunaweza kutumia nauli isiyobadilika na bei za chini zaidi. Bei halisi zinaweza kubadilika.

Njia za kusafiri

 • Pool1-2

  Usafiri wa pamoja, bei nafuu

 • UberX1-4

  Affordable, everyday rides

 • Comfort1-4

  Newer cars with extra legroom

Kupata gari kwenye Uwanja wa Ndege wa Sea-Tac

Ita gari ukiwa tayari kutoka nje

Na uchague gari linalotoshea wasafiri na mizigo mliyo nayo.

Ondoka kupitia ghorofa inayofaa

Ikiwa umeitisha UberBlack, Select, SUV au UberXL, kutana na dereva wako katika Kituo cha 1 cha Wanaowasili.

Kwa aina nyingine za usafiri, ondoka kwenye ghorofa ya wanaowasili halafu ukutane na dereva wako katika ghorofa ya 3 ya jengo la maegesho.

Kutana na dereva wako

Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana na yeye kupitia programu ili umthibitishie mahali ulipo.

Ada za maegesho katika Uwanja wa Ndege wa Sea-Tac

Ikiwa unapanga safari ya kwenda Uwanja wa Ndege wa Sea-Tac na unatarajia kuendesha gari, unaweza kupata ada za maegesho hapa.

Aina ya maegesho

Maegesho kwenye Ghorofa Sawa na Kituo

Jumla

Ya Mashirika

Ada

$39 kila siku
$32 per day
$22 kila siku
Huenda ada za maegesho zikawa zimebadilika; taarifa hii iliwekwa Tarehe 20 Novemba, 2018.

Ramani ya Uwanja wa Ndege wa Sea-Tac

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Seattle-Tacoma una jengo moja kuu lenye Kituo Kikuu na vituo 2 vya kando, Kituo cha Kando cha Kaskazini na Kituo cha Kando cha Kusini.

Maswali ambayo wasafiri wanauliza sana

Ndiyo. Bonyeza hapa ili uone orodha ya viwanja vya ndege kote duniani unakoweza kuitisha usafiri wa Uber.

Nauli ya usafiri wa Uber kuenda (au kutoka) Uwanja wa Ndege wa SEA inategemea hali kama vile aina ya usafiri, kadirio ya umbali na muda wa safari, ada ya vibali barabarani na idadi ya maombi ya usafiri.

Unaweza kuona kadirio la bei kabla ya kuitisha usafiri kwa kuweka eneo la kuchukuliwa na mahali unakoenda katika zana ya kukadiria nauli katika Uber hapo juu. Kisha, unapoitisha usafiri utaona nauli yako halisi kwenye programu kwa kutegemea hali za wakati huo.

Maeneo ya kuchukuliwa yanategemea aina ya usafiri unaoitisha na ukubwa wa uwanja wa ndege. Fuata maagizo kwenye programu kuhusu eneo utakakomkuta dereva wako. Unaweza pia kuangalia mabango yanayoashiria maeneo ya usafiri wa pamoja yaliyobainishwa kwenye uwanja wa ndege.

Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kupitia programu.

Maelezo zaidi

Unatumia mfumo wa Uber kuendesha gari?

Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kurahisisha huduma unayopokea katika viwanja vya ndege, zikiwemo sheria na kanuni za nchi husika.

Je, unaelekea uwanja tofauti wa ndege?

Unaweza kupelekwa na kuchukuliwa kutoka zaidi ya viwanja 500 vya ndege kote duniani.

Maelezo kwa wageni kwenye Uwanja wa Ndege wa Sea-Tac

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Seattle-Tacoma ni wa 31 miongoni mwa viwanja vya ndege vyenye idadi kubwa ya wasafiri ulimwenguni, huku ukiwahudumia zaidi ya wasafiri milioni 46 kila mwaka. Uwanja upo maili 14 (kilomita 23) kusini mwa katikati ya jiji la Seattle na maili 18 (kilomita 29) kaskazini mashariki mwa katikati ya jiji la Tacoma, ni mwendo usiozidi nusu saa kwa gari kutoka miji yote miwili.

Vituo katika Uwanja wa Ndege wa Sea-Tac

Uwanja wa Ndege wa SEA una majengo 3 ya vituo: Kituo Kikuu na vituo 2 vya nje (Kaskazini na Kusini) Kituo kikuu kimegawanywa katika njia 4 (A, B, C na D). Kumbi za Uwanja wa Ndege wa Seattle zipo katika vituo vyote. Unaweza kupanga safari yako ukitumia taarifa zilizo hapa chini.

Kituo Kikuu katika SEA

 • Aer Lingus
 • Air Canada
 • Alaska
 • American
 • Delta
 • Frontier
 • JetBlue
 • Kusini magharibi
 • Spirit
 • Sun Country
 • United
 • Alaska Lounge
 • Delta Sky Club
 • The Club at SEA
 • United Club
 • Ukumbi wa USO

Kituo SEA North Satellite

 • Alaska
 • Alaska Lounge

Kituo SEA South Satellite

 • Aeroméxico
 • Air France
 • All Nippon
 • Asiana
 • British Airways
 • Condor
 • Emirates
 • Eurowings
 • EVA Air
 • Hainan
 • Hawaiian
 • Icelandair
 • Korean Air
 • Lufthansa
 • Norwegian
 • Thomas Cook
 • Virgin Atlantic
 • Volaris
 • Xiamen
 • Ukumbi wa British Airways Club
 • Delta Sky Club
 • The Club at SEA

Kituo cha kimataifa katika Sea-Tac

Kuabiri kwa ajili ya safari za kuondoka katika Uwanja wa Ndege wa Seattle hufanyika katika Kituo South Satellite ambacho kina malango 14 (S1-S12, S15-S16). SEA una safari 28 za moja kwa moja za kimataifa.

Kupata chakula katika Uwanja wa Ndege wa Sea-Tac

Kuna zaidi ya maeneo 40 ya kupata chakula katika uwanja wa ndege wa Seattle yanayouza vyakula na vinywaji. Wasafiri wanaweza kuchagua kati ya migahawa maarufu inayouza vyakula vya kufungashiwa au migahawa iliyo na chaguo la huduma ya kulia mezani. Migahawa mingi ya Uwanja wa Ndege wa Seattle ipo katika Kituo Kikuu.

Kusafiri katika Uwanja wa Ndege wa Sea-Tac

Usafiri wa abiria katika Uwanja wa Ndege wa SEA hufanyika kupitia mfumo otomatiki ulio na laini 3 unaoitwa Satellite Transit System (STS). Mfumo huu wa chini ya ardhi huwapeleka watu katika njia 4 zilizo kwenye kituo kikuu na vituo 2 vya nje. STS una stesheni 6 zilizo katika maeneo yafuatayo:

 • Upande wa Kusini mwa Kituo Kikuu (karibu na njia ya Ukumbi wa A)
 • Ukumbi wa B
 • Ukumbi wa C
 • Upande wa Kaskazini mwa Kituo Kikuu (karibu na njia ya Ukumbi wa D)
 • Kituo cha North Satellite (Malango ya N)
 • Kituo South Satellite (Malango ya S)

Mambo ya kufanya katika Uwanja wa Ndege wa Sea-Tac

Uwanja wa Ndege wa Seattle huwa mwenyeji wa mradi wa muziki wa moja kwa moja, unaowahusisha wanamuziki kutoka kote Marekani. Sanaa ya kutazama ipo katika Njia ya Uwanja wa Sea-Tac, umbali wa nusu maili ulio na zaidi ya sehemu 16 za kudumu za sanaa. Wasafiri wanaotafuta shughuli za kufanya wakiwa katika uwanja wa ndege wanaweza kukandwa au kutembelea saluni ya mapambo ya makucha iliyo katika Njia ya Ukumbi wa C. Maduka yaliyo katika Uwanja wa Ndege wa Seattle ni pamoja na rafu za kuuza majarida na maduka ya nguo.

Kubadilisha fedha katika Uwanja wa Ndege wa Sea-Tac

Ofisi za kubadilisha fedha katika Uwanja wa Ndege wa Seattle kwa ajili ya wasafiri zinaweza kupatikana kabla ya sehemu ya ukaguzi wa usalama, katika sehemu ya kuchukua mizigo na katika Kituo cha South Satellite.

Hoteli zilizo karibu na Uwanja wa Ndege wa Sea-Tac

Iwe unasubiri ndege nyingine au ndege imechelewa usiku kucha, au kama unahitaji mahali pa kukaa karibu na Sea-Tac, kuna zaidi ya hoteli 35 na maeneo ya kulala karibu.

Maeneo ya kuzuru karibu na SEA

 • Capitol Hill
 • Pike Place Market
 • Snoqualmie Falls, Snoqualmie
 • Space Needle

Pata maelezo zaidi kuhusu Sea-Tac hapa.

Facebook
Instagram
Twitter