Ruka uende katika maudhui ya msingi
Uber
Uber

Uwanja wa Ndege wa Istanbul Sabiha Gökçen (SAW)

Iwe unasafiri kuelekea Istanbul kutoka Uwanja wa Ndege wa SAW au kutoka Istanbul kuelekea Uwanja wa Ndege wa SAW, iamini Uber kukufikisha unakoenda.

Sanayi Mh., 34906 Pendik/Istanbul, Turkey
+90 216-588-88-88

Njia bora zaidi ya kusafiri

Itisha usafiri kote ulimwenguni

Bonyeza tu kitufe ili upate usafiri wa angani katika zaidi ya viwanja vikuu 500.

Safiri kama mwenyeji

Acha App na dereva wako ashughulikie masuala ya kina ili usisumbuke kutafuta maelekezo katika jiji ambapo wewe ni mgeni.

Safiri bila wasiwasi kwa kutumia Uber

Pata vipengele unavyovipenda, ikiwa ni pamoja na bei zinazooneshwa moja kwa moja na uwezo wa kulipa bila pesa taslimu, hata ukiwa ugenini.

Mfumo wa Uber wa kukadiria nauli

Sampuli za bei za msafiri ni makadirio tu na hazioneshi mabadiliko yanayotokana na mapunguzo, kucheleweshwa kwenye foleni na mambo mengine. Tunaweza kutumia nauli isiyobadilika na bei za chini zaidi. Bei halisi zinaweza kubadilika.

Njia za kusafiri

 • Taxi Yellow1-4

  Taxi rides made easy

 • Taxi Turquoise1-4

  Premium taxi ride with comfortable vehicle

Jinsi ya kupata usafiri wa Uber kutoka uwanja wa ndege

Fungua App yako ili uitishe usafiri

Ukiwa tayari kutoka nje, fungua programu yako kisha uitishe usafiri. Chagua usafiri unaotoshea idadi ya wasafiri na mizigo mliyo nayo.

Fuata maelekezo katika App

Utapata maelekezo kuhusu eneo la kuchukua wasafiri moja kwa moja katika programu. Pia kunaweza kuwa na alama katika uwanja wa ndege.

Kutana na dereva wako

Nenda katika eneo la kuchukuliwa jinsi ilivyobainishwa katika App. Tafadhali kumbuka, eneo hilo huenda halitakuwa karibu kabisa na lango unaloondokea. Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kupitia App.

Vidokezo vya kuzingatia katika Uwanja wa Ndege wa Istanbul

WiFi katika Uwanja wa Ndege wa Istanbul

Ingawa Uwanja wa Ndege wa Sabiha hautoi huduma za WiFi bila malipo, wageni wanaweza kupata intaneti isiyotumia waya kwa kulipia ada kidogo isiyobadilika. Kuna vibanda 8 katika uwanja wa ndege ambapo unaweza kupata intaneti ukiwa Sabiha Gökçen.

Maegesho katika Uwanja wa Ndege wa Istanbul Sabiha Gökçen

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Sabiha Gökçen una chaguo mbalimbali za maegesho ya ghorofa yaliyo umbali wa kutembea kutoka jengo kuu la kituo.

Kuhifadhi mizigo katika uwanja wa ndege wa Sabiha Gökçen

Ofisi ya mizigo—ipo katika Ukumbi wa Kimataifa—inafanya kazi saa 24 kwa siku na inakuruhusu kuhifadhi mizigo yako baada ya kulipa ada ndogo. Uwanja wa Ndege wa Sabiha pia una huduma ya makuli.

Maswali ambayo wasafiri wanauliza sana

Uber inapatikana katika Uwanja wa Ndege wa SAW, kwa hivyo unaweza kufurahia usafiri wa starehe na uhakika popote unapotaka kwenda.

Ili kupata eneo la kuchukuliwa, angalia programu ya Uber baada ya kuitisha usafiri.

Even if a trip is not very long, Uber rates to and from Sahiba Gökçen Airport may still be affected by time, traffic, and other factors. Check the Uber price estimator for approximate trip prices.

Muda wa kuchukuliwa unaweza kuwa tofauti kulingana na wakati, idadi ya madereva wanaopatikana na masuala mengine.

Maelezo zaidi

Je, unaelekea uwanja tofauti wa ndege?

Unaweza kupelekwa na kuchukuliwa kutoka zaidi ya viwanja 500 vya ndege kote duniani.
Pata uwanja wa ndege

Mambo ya kufanya katika kituo cha Uwanja wa Ndege wa Istanbul

Uber ni chaguo bora kwa wasafiri wanaowasili au kuondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa SAW. Uwanja wa Ndege wa Sabiha Gökçen ni moja ya nyanja za shughuli nyingi mjini Istanbul. Unahudumia wasafiri katika upande wa mashariki mwa mji huu na huwahudumia zaidi ya wasafiri milioni 25 kila mwaka. Uwanja wa ndege wa Sabiha Gökçen unapatikana upande wa Asia wa Istanbul, takribani kilomita 50 (maili 31) kutoka katikati mwa mji. Kwa mtu yeyote anayesafiri kuelekea upande wa Asia wa mji, na pia mji wa Darika, uwanja huu ni chaguo bora lenye vifaa vya kisasa kwa wasafiri. Lina ukubwa wa mita 320,000 mraba (fiti 3.4 mraba).

Kituo cha Uwanja wa Ndege wa Istanbul

Uwanja wa Sabiha Gökçen una jengo moja la kituo kinachohudumia safari za kimataifa na za nchini na kina vibanda 112 ya kuripoti. Katika uwanja wa ndege na majengo ya karibu, kuna ukumbi wa mikutano na jengo la VIP, pamoja na maegesho ya magari, hoteli na eneo la vyakula. Mashirika ya ndege yanayohudumu kwenye Uwanja wa Ndege wa Sabiha yanajumuisha:

 • Emirates
 • flydubai
 • Qatar
 • SunExpress
 • Turkish Airlines

Kusafiri kwenye Uwanja wa Ndege wa SAW

kwa vile Uwanja wa Ndege wa SAW una jengo moja la kituo, hamna haja kutumia gari kusafiri kutoka kituo kimoja hadi kingine. Usafiri mbalimbali unapatikana kuwapeleka na kuwaondoa watu kwenye uwanja wa ndege, zikiwemo teksi, mabasi, treni na Uber. Kuna pia kuna njia moja kwa moja ya kwenda kwenye barabara kuu ya TEM, hivyo kuwezesha watu wanaokodisha magari kwenye uwanja wa Ndege wa Istanbul Sabiha Gökçen kufikia mji wa Istanbul kwa urahisi. Maegesho yana ghorofa 4 na yanawafaa wasafiri wanaowasili kwenye uwanja wa ndege kwa kutumia magari yao.

Mambo ya kufanya kwenye Uwanja wa Ndege wa Sabiha Gökçen

Uwanja wa Ndege wa SAW una maduka mengi yanayofunguliwa kila wakati, kwa hivyo iwe unataka kununua vitu unavyohitaji safarini kabla ya safari au unataka kununulia marafiki na ndugu zako zawadi, kuna chaguo za kutosha. Bidhaa hizi hazitozwi kodi na kuna huduma nyingi. Una ukubwa wa mita 4,500 mraba (fiti 48,400 mraba).

Sebule katika Uwanja wa Ndege wa Istanbul Sabiha Gökçen

Kuna sebule mbalimbali kwenye Uwanja wa Ndege wa SAW, kwenye kumbi zote mbili za Nchini na za kimataifa, zinazokupa nafasi ya kupumzika baada ya shughuli kwenye uwanja wa ndege.

Hoteli karibu na Uwanja wa Ndege wa Sabiha Gökçen

Hoteli moja iko kwenye Uwanja wa Ndege wa Sabiha. Ni chaguo bora kwa yeyote anayesubiri ndege nyingine au anayewasili Istanbul alfajiri. Hoteli hii ina ghorofa 3 na vyumba 128. Inatosha kukidhi mahitaji ya wasafiri na inaweza kufikiwa katika pande zote za uwanja. Katika umbali wa dakika 30 kutoka uwanja wa ndege, wasafiri wanaweza kupata malazi mengi ya bei nafuu na pia hoteli za kifahari. Vyumba vya mikutano pia vinapatikana katika hoteli nyingi. Pia kuna vituo vya biashara, hivyo basi kumwezesha mfanyabiashara aendelee na kazi popote alipo.

Sehemu za kuvutia karibu na Uwanja wa Ndege wa SAW

Ikiwa unasubiri ndege nyingine kwa mrefu katika Uwanja wa Ndege wa Sabiha, una vivutio na maeneo mengi ya kuzuru, haswa ikiwa una muda wa kuelekea katikati mwa mji wa kihistoria wa Istanbul, yakiwemo:

 • The Blue Mosque
 • Mnara wa Galata
 • Grand Bazaar
 • Hagia Sophia
 • Kasri ya Topkapi

Pata maelezo zaidi kuhusu Uwanja wa Ndege wa Istanbul SAWhapa.

Facebook
Instagram
Twitter