Ruka uende katika maudhui ya msingi

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Raleigh-Durham (RDU)

Tumia Uber kusafiri popote, iwe unasafiri kutoka Uwanja wa Ndege wa RDU hadi kwenye Makavazi ya North Carolina au kutoka katikati mwa mji wa Durham hadi Uwanja wa Ndege wa RDU.

2400 John Brantley Boulevard, Morrisville, NC 27560
+1 919-840-2123

Njia bora zaidi ya kusafiri

Itisha usafiri kote ulimwenguni

Bonyeza tu kitufe ili upate usafiri wa angani katika zaidi ya viwanja vikuu 500.

Safiri kama mwenyeji

Acha App na dereva wako ashughulikie masuala ya kina ili usisumbuke kutafuta maelekezo katika jiji ambapo wewe ni mgeni.

Safiri bila wasiwasi kwa kutumia Uber

Pata vipengele unavyovipenda, ikiwa ni pamoja na bei zinazooneshwa moja kwa moja na uwezo wa kulipa bila pesa taslimu, hata ukiwa ugenini.

Punguzo la hadi $15

Pata punguzo la $5 kwenye safari zako tatu za kwanza. Tumia kuponi ya ofa NEWRIDER15. Muda wa kuitumia unakwisha siku 30 baada ya kuweka kuponi ya ofa kwenye akaunti yako ya Uber.

Aina za usafiri ukiwa eneo husika

 • UberX

  1-3

  Affordable everyday trips

 • Comfort

  1-3

  Newer cars with extra legroom

 • UberXL

  1-5

  Affordable rides for groups up to 5

 • Uber Green

  1-3

  Low-emission rides

 • Connect

  1-4

  Send packages to friends & family

1/5

Kupata gari kwenye Uwanja wa Ndege wa RDU

Ita gari ukiwa tayari kutoka nje

Na uchague gari linalotoshea wasafiri na mizigo mliyo nayo.

Ondoka kupitia ghorofa ya wanaowasili

Ukiwa katika Kituo cha 1, elekea nje kupitia sehemu ya kuchukua mizigo hadi eneo la kuchukua wasafiri la 1. Katika Kituo cha 2, ondoka kwenye sehemu ya kuchukua mizigo kisha uende katika eneo la 17. Hapa ndipo madereva wote washirika wa Uber katika uwanja wa ndege wa RDU huwapata na kuwachukua wasafiri.

Kutana na dereva wako kando ya barabara

Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana na yeye kupitia programu ili umthibitishie mahali ulipo.

Ramani ya Uwanja wa Ndege wa RDU

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Raleigh-Durham una vituo 2 na kumbi 3. Kituo cha 2 kina malango 4 ya kimataifa.

Maswali ambayo wasafiri wanauliza sana

 • Ndiyo. Bonyeza hapa ili uone orodha ya viwanja vya ndege kote duniani unakoweza kuitisha usafiri wa Uber.

 • Nauli ya usafiri wa Uber kuenda (au kutoka) Uwanja wa Ndege wa RDU inategemea hali kama vile aina ya usafiri, kadirio ya umbali na muda wa safari, ada ya vibali barabarani na idadi ya maombi ya usafiri.

  Unaweza kuona kadirio la bei kabla ya kuitisha usafiri kwa kuweka eneo la kuchukuliwa na mahali unakoenda katika zana ya kukadiria nauli katika Uber hapo juu. Kisha, unapoitisha usafiri utaona nauli yako halisi kwenye app kwa kutegemea hali za wakati huo.

 • Maeneo ya kuchukuliwa yanategemea aina ya usafiri unaoitisha na ukubwa wa uwanja wa ndege. Fuata maagizo kwenye App kuhusu eneo utakakomkuta dereva wako. Unaweza pia kuangalia mabango yanayoashiria maeneo ya usafiri wa pamoja yaliyobainishwa kwenye uwanja wa ndege.

  Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kupitia programu.

Maelezo zaidi

Unatumia mfumo wa Uber kuendesha gari?

Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kurahisisha huduma unayopokea katika viwanja vya ndege, zikiwemo sheria na kanuni za nchi husika.

Je, unaelekea uwanja tofauti wa ndege?

Unaweza kupelekwa na kuchukuliwa kutoka zaidi ya viwanja 600 vya ndege kote duniani.

Maelezo kwa wageni kwenye Uwanja wa Ndege wa RDU

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Raleigh-Durham (RDU) ni wa 39 kati ya viwanja vyenye shughuli nyingi mno Marekani kwa kuzingatia idadi ya abiria. Unawahudumia zaidi ya wasafiri milioni 11 kila mwaka. RDU unapatikana Kaunti ya Wake, North Carolina, maili 14 (kilomita 23), mwendo wa dakika 20 kwa kuendesha gari wakati hakuna foleni au vikwazo vingine barabarani, iwe ni kutoka katikati ya jiji la Raleigh, ambalo ndilo jiji kuu la jimbo na vilevile jiji la Durham.

Vituo katika Uwanja wa Ndege wa RDU

Uwanja wa Ndege wa RDU una vituo 2 vya abiria—Kituo cha 1 na Kituo cha 2—vituo hivi 2 vina milango 45. Kumbi za Uwanja wa Ndege wa RDU ziko katika Kituo cha 2. Unaweza kupanga safari yako ukitumia taarifa zilizo hapa.

Kituo cha 1 katika RDU

 • Kusini Magharibi

Kituo cha 2 katika RDU

 • Air Canada
 • Alaska
 • Allegiant
 • American
 • Delta
 • Frontier
 • JetBlue
 • United
 • American Airlines Admirals Club
 • Delta Sky Club
 • Ukumbi wa USO

Kituo cha kimataifa katika uwanja wa RDU

Eneo la kuabiri kwa ajili ya usafiri wa kimataifa lipo katika Kituo cha 2 cha RDU. RDU ina vituo 8 vya usafiri wa moja kwa moja wa kimataifa.

Vyakula katika Uwanja wa Ndege wa RDU

Wasafiri wanaweza kuchagua miongoni mwa vituo 20 vilivyo katika Uwanja wa RDU, vikiwemo baa, migahawa inayouza vyakula vya kufungashiwa pamoja na iliyo na meza ya kulia. Sehemu za kula na kunywa katika Uwanja wa Ndege wa RDU zinapatikana katika vituo vyote.

Usafiri katika Uwanja wa Ndege wa RDU

Vituo hivyo 2 havina usafiri kutoka sehemu ya kuabiria ndege. Wasafiri wanaotoka kituo kimoja kwenda kingine wanaweza kutumia mabasi ya usafiri katika Uwanja wa Ndege wa RDU au watumie njia ya kutembelea inayotokea katika maegesho yaliyo katika vituo.

Mambo ya kufanya ukiwa katika Uwanja wa Ndege wa RDU

Uwanja wa Ndenge wa Raleigh-Durham una shughuli na sehemu kadhaa za kuvutia, ikiwemo maonesho ya sanaa yaliyo na majengo ya muda na ya kudumu katika eneo lote la uwanja wa ndege. Kuna spaa katika Kituo cha 1 karibu na Lango la A7 na katika Kituo cha 2 karibu na Lango la C3.

Kubadilisha sarafu katika Uwanja wa Ndege wa RDU

Ofisi za kubadilisha sarafu katika uwanja wa ndege wa RDU ziko katika Kituo cha 2 kwenye ukumbi wa tiketi karibu na sehemu ya kuchukua mizigo.

Hoteli zilizo karibu na Uwanja wa Ndege wa RDU

Iwe unasubiri ndege nyingine au ndege imechelewa usiku kucha, au kama unahitaji mahali pa kukaa karibu na RDU, kuna zaidi ya hoteli 20 na maeneo mengine ya kulala karibu.

Vivutio karibu na Uwanja wa Ndege wa RDU

 • Chapel Hill’s Planetarium
 • Makumbusho ya sanaa na historia ya Raleigh
 • Vyuo vikuu vya The Research Triangle
 • Lake Johnson

Pata maelezo zaidi kuhusu Uwanja wa Ndege wa RDUhapa.

Facebook
Instagram
Twitter

Ukurasa huu una taarifa kutoka kwenye tovuti za washirika wengine ambazo hazisimamiwi na Uber na zinaweza kugeuzwa au kubadilishwa mara kwa mara. Maelezo yoyote yaliyojumuishwa kwenye ukurasa huu ambayo hayahusiani moja kwa moja na Uber au kazi zake yanatumika kuarifu tu na hayafai kutegemewa, au kuchukuliwa au kufasiliwa kwa namna inayoweka dhamana ya aina yoyote, iwe ya moja kwa moja au inayokisiwa, kuhusu maelezo yaliyo hapa. Baadhi ya masharti na vipengele hutofautiana kutegemea nchi, eneo na jiji. Ofa ya punguzo inawalenga watumiaji wapya pekee. Huwezi kutumia ofa hii pamoja na ofa nyinginezo na haiwezi kutumiwa katika bakshishi. Inapatikana kwa muda mfupi. Vigezo na masharti ya ofa vinaweza kubadilika.