Ruka uende katika maudhui ya msingi

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Pittsburgh (PIT)

Tumia Uber kusafiri popote, iwe unasafiri kutoka Uwanja wa Ndege wa Pittsburgh hadi Hifadhi ya Wanyama ya Pittsburgh au kutoka katikati mwa mji hadi PIT.

1000 Airport Boulevard, Pittsburgh, PA 15231
+1 412-472-3525

Njia bora zaidi ya kusafiri

Itisha usafiri kote ulimwenguni

Bonyeza tu kitufe ili upate usafiri wa angani katika zaidi ya viwanja vikuu 500.

Safiri kama mwenyeji

Acha App na dereva wako ashughulikie masuala ya kina ili usisumbuke kutafuta maelekezo katika jiji ambapo wewe ni mgeni.

Safiri bila wasiwasi kwa kutumia Uber

Pata vipengele unavyovipenda, ikiwa ni pamoja na bei zinazooneshwa moja kwa moja na uwezo wa kulipa bila pesa taslimu, hata ukiwa ugenini.

Punguzo la hadi $15

Pata punguzo la $5 kwenye safari zako tatu za kwanza. Tumia kuponi ya ofa NEWRIDER15. Muda wa kuitumia unakwisha siku 30 baada ya kuweka kuponi ya ofa kwenye akaunti yako ya Uber.

Aina za usafiri ukiwa eneo husika

 • UberX

  1-3

  Affordable everyday trips

 • Comfort

  1-3

  Newer cars with extra legroom

 • UberXL

  1-5

  Affordable rides for groups up to 5

1/3

Kupata gari kwenye Uwanja wa Ndege wa Pittsburgh

Ita gari ukiwa tayari kutoka nje

Chagua aina ya gari linalotosha idadi ya wasafiri na mizigo mliyo nayo.

Ondoka kwenye sehemu ya kuchukua mizigo

Kutoka kwenye mlango wa 4, tafuta eneo la biashara la kuchukulia abiria kando ya barabara lenye rangi ya zambarau. Hapa ndipo madereva wote washirika wa Uber katika uwanja wa ndege wa PIT huwapata na kuwachukua wasafiri.

Kutana na dereva wako

Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kupitia programu.

Ada za maegesho katika Uwanja wa Ndege wa Pittsburgh

Ikiwa unapanga safari ya kwenda Uwanja wa Ndege wa Pittsburgh na unatarajia kuendesha gari, unaweza kupata ada za maegesho hapa.
Ada za maegesho katika Uwanja wa Ndege wa Pittsburgh

Ada

$26 kila siku
$16 kila siku
$8 kila siku
Huenda ada za maegesho zikawa zimebadilika; taarifa hii iliwekwa Tarehe 20 Novemba, 2018.

Ramani ya Uwanja wa Ndege wa Pittsburgh

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Pittsburgh una majengo 2 makuu, Kituo cha Upande wa Nje na Kituo cha Upande wa Ndege. Kituo cha Upende wa Ndege kina kumbi 4, huku Ukumbi wa C ukihudumia wanaowasili kutoka safari za kimataifa.

Maswali ambayo wasafiri wanauliza sana

 • Ndiyo. Bonyeza hapa ili uone orodha ya viwanja vya ndege kote duniani unakoweza kuitisha usafiri wa Uber.

 • Nauli ya usafiri wa Uber kuenda (au kutoka) Uwanja wa Ndege wa PIT inategemea hali kama vile aina ya usafiri, kadirio ya umbali na muda wa safari, ada ya vibali barabarani na idadi ya maombi ya usafiri.

  Unaweza kuona kadirio la bei kabla ya kuitisha usafiri kwa kuweka eneo la kuchukuliwa na mahali unakoenda katika zana ya kukadiria nauli katika Uber hapo juu. Kisha, unapoitisha usafiri utaona nauli yako halisi kwenye app kwa kutegemea hali za wakati huo.

 • Maeneo ya kuchukuliwa yanategemea aina ya usafiri unaoitisha na ukubwa wa uwanja wa ndege. Fuata maagizo kwenye App kuhusu eneo utakakomkuta dereva wako. Unaweza pia kuangalia mabango yanayoashiria maeneo ya usafiri wa pamoja yaliyobainishwa kwenye uwanja wa ndege.

  Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kupitia programu.

Maelezo zaidi

Unatumia mfumo wa Uber kuendesha gari?

Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kurahisisha huduma unayopokea katika viwanja vya ndege, zikiwemo sheria na kanuni za nchi husika.

Je, unaelekea uwanja tofauti wa ndege?

Unaweza kupelekwa na kuchukuliwa kutoka zaidi ya viwanja 600 vya ndege kote duniani.

Maelezo kwa wageni kwenye Uwanja wa Ndege wa Pittsburgh

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Pittsburgh (PIT) ndio wa 47 kwa shughuli nyingi nchini Marekani, ukiwahudumia zaidi ya wasafiri milioni 8 kila mwaka. Upo umbali wa takribani maili 18 ( kilomita 29) kutoka katikati ya jiji la Pittsburgh, ambao ni umbali wa dakika 20 kwa kuendesha gari wakati hakuna foleni au vikwazo vingine barabarani.

Vituo vya abiria katika Uwanja wa Ndege wa Pittsburgh

Uwanja wa Ndege wa PIT una vituo 2 vikuu: Kituo cha Upande wa Abiria na Kituo cha Upande wa Ndege Kituo cha Upande wa Abiri kina sehemu ya kuchukua mizigo, kukata tiketi, ukaguzi wa usalama na usafiri wa ardhini. Kituo cha Upande wa Ndege kina kumbi 4 (A, B, C na D) huku kukiwa na malango 75. Kumbi za uwanja wa ndege wa Pittsburgh zipo katika Vituo vya B na C. Unaweza kupanga safari yako kwa kutumia taarifa zilizo hapa chini.

Ukumbi wa A katika Kituo cha upande wa Ndege katika PIT

 • Air Canada
 • Boutique
 • Kusini Magharibi
 • United

Ukumbi wa B katika Kituo cha upande wa Ndege katika PIT

 • Alaska
 • American
 • Southern Airways Express
 • Spirit
 • American Airlines Admirals Club

Ukumbi wa C katika Kituo cha Upande wa Ndege katika PIT

 • Allegiant
 • British Airways
 • Condor
 • WOW
 • The Club Lounge

Ukumbi wa D katika Kituo cha Upande wa Ndege katika PIT

 • Delta
 • Frontier
 • JetBlue

Kituo cha kimataifa katika PIT

Safari za kimataifa katika Uwanja wa Ndege wa Pittsburgh huwasili na kuondoka kutoka upande wa Ndege wa Ukumbi wa C, ulio na malango ya C51 hadi C61. Uwanja wa Ndege wa PIT una safari za moja kwa moja za kuelekea zaidi ya vituo 20 vya kimataifa.

Kupata chakula katika Uwanja wa Ndege wa Pittsburgh

Kuna zaidi ya chaguo 30 za kupata mlo katika Uwanja wa Ndege wa PIT katika Upande wa Abiria na Upande wa Ndege, zikiwemo baa, maduka ya kahawa, maduka ya vitafunio na migahawa ya huduma za kulia mezani. Vyakula katika Uwanja wa Ndege wa Pittsburgh vinajumuisha vyakula vya kawaida vya Marekani na hata vyakula vya mtindo wa kimataifa.

Kusafiri katika Uwanja wa Ndege wa Pittsburgh

Wasafiri katika PIT wanaweza kutumia People Mover, mfumo wa kiotomatiki ulioundwa mahususi kupitia chini ya ardhi na kuwasafirisha wasafiri kutoka Kituo cha Upande wa Abiria na Upande wa Ndege. Vilevile, usafiri katika Uwanja wa ndege wa Pittsburgh unatolewa kwa kuweka sehemu za kutembelea karibu na kila upande ili kuwe na urahisi kwa abiria.

Mambo ya kufanya ukiwa katika Uwanja wa Ndege wa Pittsburgh

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Pittsburgh una mpango wa sanaa katika uwanja wa ndege unaoonesha sanaa za wasanii wa karibu, wa kitaifa na wa kimataifa. Sanaa huoneshwa katika Ukumbi wa Upande wa Abiria na katika Ukumbi wa Upande wa Ndege katika Kituo cha C. Ukumbi kwa ajili ya watoto upo Upande wa Ndege katika Kituo cha C, na una vipengele vya kuvutia na kuchezewa na watoto. Spaa zipo katika Ukumbi wa B katikati ya Kituo cha Upande wa Ndege.

Kubadilisha sarafu katika Uwanja wa Ndege wa Pittsburgh

Ofisi ya kubadilisha sarafu katika Uwanja wa Ndege wa Pittsburgh kwa ajili ya abiria IKo katika Kituo cha Upande wa Abiria, katika sehemu ya kuondokea.

Hoteli zilizo karibu na Uwanja wa Ndege wa Pittsburgh

Iwe unasubiri ndege nyingine au ndege imechelewa usiku kucha, au kama unahitaji mahali pa kukaa karibu na PIT, kuna zaidi ya hoteli 25 na maeneo ya kulala karibu.

Vivutio katika Uwanja wa Ndege wa Pittsburgh

 • Cathedral of Learning
 • Grandview Overlook
 • Bustani ya mimea na uhifadhi ya Pittsburgh
 • Bustani ya Raccoon Creek State, Hookstown

Pata maelezo zaidi kuhusu PIT hapa.

Facebook
Instagram
Twitter

Ukurasa huu una taarifa kutoka kwenye tovuti za washirika wengine ambazo hazisimamiwi na Uber na zinaweza kugeuzwa au kubadilishwa mara kwa mara. Maelezo yoyote yaliyojumuishwa kwenye ukurasa huu ambayo hayahusiani moja kwa moja na Uber au kazi zake yanatumika kuarifu tu na hayafai kutegemewa, au kuchukuliwa au kufasiliwa kwa namna inayoweka dhamana ya aina yoyote, iwe ya moja kwa moja au inayokisiwa, kuhusu maelezo yaliyo hapa. Baadhi ya masharti na vipengele hutofautiana kutegemea nchi, eneo na jiji. Ofa ya punguzo inawalenga watumiaji wapya pekee. Huwezi kutumia ofa hii pamoja na ofa nyinginezo na haiwezi kutumiwa katika bakshishi. Inapatikana kwa muda mfupi. Vigezo na masharti ya ofa vinaweza kubadilika.