Pata chochote unachohitaji ili uweze kufuatilia mafanikio yako unaposafiri.
Dhibiti njia zako za kulipa, kagua historia ya safari na zaidi.
Unaona maelezo ya Washington D.C.. Ili uone vipengele na huduma zilizo mahali pengine, tafadhali chagua mji tofauti.
Iwe unakwenda katikati ya jiji kutoka Uwanja wa Ndege wa Madrid au kutoka Museo del Prado kuelekea katika Uwanja wa Ndege wa Madrid, itegemee Uber kukufikisha.
Av de la Hispanidad, s/n, Madrid 28042 Uhispania
+34 913-21-10-00
Bonyeza tu kitufe ili upate usafiri wa angani katika zaidi ya viwanja vikuu 500.
Acha App na dereva wako ashughulikie masuala ya kina ili usisumbuke kutafuta maelekezo katika jiji ambapo wewe ni mgeni.
Pata vipengele unavyovipenda, ikiwa ni pamoja na bei zinazooneshwa moja kwa moja na uwezo wa kulipa bila pesa taslimu, hata ukiwa ugenini.
Sampuli za bei za wasafiri ni makadirio tu na hazioneshi mabadiliko yanayosababishwa na ofa, jiografia kucheleweshwa kwenye foleni na mambo mengine. Tunaweza kutumia nauli isiyobadilika na bei za chini zaidi. Bei halisi za safari na safari zilizopangwa huenda zikawa tofauti.
Affordable rides with VTC and Taxi
Luxury rides with professional drivers
Ukiwa tayari kutoka nje, fungua App yako kisha uitishe usafiri. Chagua aina ya gari linalofaa ukubwa wa kikundi chako na mizigo mnayohitaji kubebewa.
Utapata maelekezo kuhusu eneo la kuchukua wasafiri moja kwa moja katika App. Pia kunaweza kuwa na mabango katika uwanja wa ndege.
Nenda katika eneo la kuchukuliwa jinsi ilivyobainishwa katika App. Tafadhali kumbuka, eneo hilo huenda halitakuwa karibu kabisa na lango unaloondokea. Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kupitia App.
Uwanja wa Ndege wa Madrid huwapa wasafiri wote Wi-Fi bila malipo. Fuata maelekezo haya ili uingie katika mtandao: - Tafuta mtandao wa AIRPORT FREE WIFI AENA - Jisajili kwa kutumia Facebook, LinkedIn, barua pepe Aena Club Cliente
MAD ina ofisi ya mizigo ambapo wasafiri wanaweza kulipia ada na kuacha mizigo yao kwa hadi siku 14. Ofisi ya mizigo pia ina bidhaa kadhaa muhimu kwa usafiri, masanduku ya baiskeli na huduma za uchapishaji.
MAD ina maegesho ya muda mfupi na ya muda mrefu, maeneo ya kuchukua na kushusha wasafiri haraka, maegesho ya VIP, maegesho ya daraja la kwanza na maegesho nafuu. Pia kuna maegesho tofauti kwa ajili ya pikipiki na baiskeli.
Uber inapatikana katika Uwanja wa Ndege wa Madrid, kwa hivyo unaweza kufurahia usafiri wa starehe na uhakika popote unapotaka kwenda.
Maeneo ya kuchukua wasafiri wa Uber katika viwanja vya ndege yanaweza kubadilika, kwa hivyo ili kupata eneo la kuchukuliwa, angalia App yako ya Uber kila baada ya kuitisha usafiri.
Ada za safari za Uber kwenda na kutoka katika Uwanja wa Ndege wa Madrid zinaweza kuathiriwa na wakati, foleni na masuala mengine. Angalia mfumo wa Uber wa kukadiria nauli kwenye App ya Uber ili ufahamu makadirio ya nauli ya safari.
Unapoitisha usafari, App itakupa makadirio ya muda ambao dereva atachukua kufika katika eneo la kuchukua wasafiri.
Safari za kwanza za ndege za kibiashara ziliondoka Uwanja wa Ndege wa Madrid mwaka 1933. Kuanzia wakati huo, uwanja huo umekuwa mojawapo ya vituo muhimu kwa watalii wanaoingia Uhispania. Kila mwaka, MAD hupokea takribani wasafiri milioni 58 na kushughulikia zaidi ya safari 400,000 za ndege. Uwanja wa Ndege wa Madrid-Barajas uko takribani kilomita 15 (maili 9) kaskazini mashariki mwa eneo la katikati ya jiji la Madrid, safari ya takribani dakika 20, hivyo kufanya Uber iwe chaguo bora la usafiri wako.
Uwanja wa Ndege wa Madrid una vituo 5: T1, T2, T3, T4 na T4S. Vituo vyote vinashughulikia safari za kimataifa, kitaifa, za Schengen na zisizo za Schengen. Kuna usafiri wa basi bila malipo kwa ajili ya kuwapeleka wasafiri katika vituo mbalimbali.
MAD ni uwanja mkubwa wa ndege ambao una aina mbalimbali za vyakula kwa wasafiri, iwe unataka mlo mkuu, kinywaji cha kukuburudisha au kitafunwa chepesi kabla au baada ya safari yako. Uwanja huu una migahawa kadhaa yenye vyakula unavyoweza kujichagulia yakiwemo mapishi kutoka duniani kote kama vile vyakula vya Kijapani, Kifaransa, bila kusahau Tapas na vyakula vingine vya Kihispania. Ikiwa huna muda wa kula ndani ya mgahawa, kuna aina kadhaa ya vyakula vya kufungashwa kama vile sandwichi, aina kadhaa za maandazi, saladi na vitafunwa vingine vitamu, vilevile kuna vyakula vya kuchukua haraka kama vile chipsi na baga. Pia kuna baa kadhaa zinazouza bia, mivinyo na pombe za mchapalo.
Wanaopenda ununuzi wa rejareja watafurahia maduka yaliyo katika Uwanja wa Ndege wa Madrid, hasa sehemu ya msururu wa maduka ya bidhaa zisizotozwa kodi, ambayo ndiyo sehemu kubwa kabisa Uhispania na ina bidhaa za kiwango cha kimataifa zinazouzwa kwa bei nafuu. Katika maeneo yote ya uwanja wa ndege kuna maduka yanayouza vifaa vya mavazi, nguo, mapambo, saa, vifaa vya kielektroniki, vifaa muhimu kwa ajili ya usafiri na hidaya. Mashabiki wa Kandanda pia wanaweza kuzuru sehemu ya maduka ya bidhaa za michezo ili kupata bidhaa mahususi za Real Madrid.
Ikiwa una muda kabla ya safari yako, unaweza kufurahia kumbi kadhaa zilizo katika MAD ambapo wasafiri wanaweza kufanya kazi au kupumzika kwa muda. Vituo vyote vina kumbi ambapo wasafiri wote wanaweza kukaa kwa kulipia kiasi fulani cha ada, ikiwa ni pamoja na familia zilizo na watoto. Huduma zinazopatikana ni pamoja na vinywaji na vyakula baridi na moto, magazeti na majarida, bafu, viti vya kujimwaya na Wi-Fi bila malipo.
Uwanja wa Ndege wa Madrid una huduma mbalimbali kwa wasafiri ili kuwawezesha kuwa na safari njema bila usumbufu. Familia zinazosafiri pamoja na watoto wachanga zinaweza kupata maeneo ya kuchezea, kumbi za kunyonyeshea watoto, vijigari vya kusukumia watoto na kipaumbele katika ukaguzi wa usalama. Kuna huduma za usaidizi kwa watu walio na matatizo ya kutembea, lakini ni sharti huduma hiyo iombwe angalau saa 48 kabla ya wakati wa ndege kuondoka. Wanaosafiri kibiashara wanaweza kutumia sehemu za kufanyia kazi na vyumba vya mikutano na mawasilisho.
Kuna aina mbalimbali za sehemu za kulala karibu na uwanja wa ndege. Ikiwa ndege yako haitaondoka asubuhi sana, kuna mamia ya hoteli jijini Madrid, zinazoweza kufikiwa kwa urahisi kwa kutumia mfumo wa Uber kutoka kwenye uwanja wa ndege.
Madrid ndilo jiji kuu la Uhispania na wageni wanaweza kuzuru bustani, medani na barabara mbalimbali za jiji. Licha ya kuwa makao ya mojawapo ya vilabu maarufu zaidi vya soka duniani, Madrid ina sanaa, mijengo na migahawa mingi. Baadhi ya vivutio ni pamoja na:
Pata maelezo zaidi kuhusu MAD hapa.
Viungo kwa tovuti za nje vimeandaliwa kwa ajili ya kurahisisha shughuli za wageni. Hatua ya kuelekeza viungo kwenye tovuti nyingine itakuwa kwa hiari yako na Uber haitakubali dhima kwa tovuti zilizounganishwa au maudhui yaliyomo.