Ruka uende katika maudhui ya msingi

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Rio de Janeiro-Galeão (GIG)

Pata gari la kukupeleka na kukurudisha kwenye Uwanja wa ndege wakati wowote, iwe unasafiri kutoka Uwanja wa Ndege wa Galeão hadi Rio de Janeiro au mji mwingine.

Av. Vinte de Janeiro, s/nº - Ilha do Governador, Rio de Janeiro - RJ, 21941-900, Brasil
+55 21-3004-6050

Njia bora zaidi ya kusafiri

Itisha usafiri kote ulimwenguni

Bonyeza tu kitufe ili upate usafiri wa angani katika zaidi ya viwanja vikuu 500.

Safiri kama mwenyeji

Acha App na dereva wako ashughulikie masuala ya kina ili usisumbuke kutafuta maelekezo katika jiji ambapo wewe ni mgeni.

Safiri bila wasiwasi kwa kutumia Uber

Pata vipengele unavyovipenda, ikiwa ni pamoja na bei zinazooneshwa moja kwa moja na uwezo wa kulipa bila pesa taslimu, hata ukiwa ugenini.

Aina za usafiri ukiwa eneo husika

 • UberX Promo

  1-3

  Economize esperando alguns minutos

 • UberX

  1-3

  Affordable everyday trips

 • Comfort

  1-3

  Better cars and premium experience

1/3

Kupata gari kwenye Uwanja wa Ndege wa GIG

Fahamu unakoweza kuchukuliwa

Ukiwa tayari kutoka nje, chagua kituo chako na eneo ambalo ungependa kuchukuliwa kwenye programu.

Angalia App ili upate maelezo

Punde unapoitisha gari, utapata maelekezo kupitia programu. Katika Uwanja wa Ndege wa GIG, wasafiri hukuchuliwa katika ghorofa ya wanaowasili (katika Kituo cha 1 na 2). Elekea kwenye ghorofa ya juu umkute dereva wako katika eneo la kuchukuliwa ulilochagua.

Kutana na dereva wako

Nenda kwenye eneo lililobainishwa la kuchukua wasafiri. Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kupitia programu.

Ramani ya Uwanja wa Ndege wa GIG

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Rio de Janeiro–Galeão una vituo 2, Kituo cha 2 hushughulikia wanaowasili kutoka safari za kimataifa.

Maswali ambayo wasafiri wanauliza sana

 • Ndiyo. Bonyeza hapa ili uone orodha ya viwanja vya ndege kote duniani unapoweza kuitisha usafiri wa Uber.

 • Nauli ya usafiri wa Uber kuenda (au kutoka) Uwanja wa Ndege wa Galeão Airport (GIG) inategemea hali kama vile aina ya usafiri, kadirio ya umbali na muda wa safari, ada ya vibali barabarani na idadi ya maombi ya usafiri.

  Unaweza kuona kadirio la bei kabla ya kuitisha usafiri kwa kuweka eneo la kuchukuliwa na mahali unakoenda katika zana ya kukadiria nauli katika Uber hapo juu. Kisha, unapoitisha usafiri utaona nauli yako halisi kwenye app kwa kutegemea hali za wakati huo.

 • Maeneo ya kuchukuliwa yanategemea aina ya usafiri unaoitisha na ukubwa wa uwanja wa ndege. Fuata maagizo kwenye App kuhusu eneo utakakomkuta dereva wako. Unaweza pia kuangalia mabango yanayoashiria maeneo ya usafiri wa pamoja yaliyobainishwa kwenye uwanja wa ndege.

  Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kupitia programu.

Maelezo zaidi

Unatumia mfumo wa Uber kuendesha gari?

Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kurahisisha huduma unayopokea katika viwanja vya ndege, zikiwemo sheria na kanuni za nchi husika.

Je, unaelekea uwanja tofauti wa ndege?

Unaweza kupelekwa na kuchukuliwa kutoka zaidi ya viwanja 600 vya ndege kote duniani.

Maelezo kwa wageni kwenye Uwanja wa Ndege wa GIG

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Rio de Janeiro-Galeão ni wa pili kwa shughuli nyingi zaidi nchini Brazil, huku ukiwahudumia zaidi ya abiria milioni 16 kila mwaka. Uwanja wenyewe upo kilomita 19 (maili 12) kutoka katikati mwa Rio de Janeiro, ni mwendo wa kama dakika 35 kwa gari wakati hakuna foleni au vikwazo vingine barabarani.

Vituo katika Uwanja wa Ndege wa GIG

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Rio de Janeiro-Galeão una vituo 2: Kituo cha 1 na 2. Hata hivyo, safari nyingi hutokea katika Kituo cha 2. Kumbi za Uwanja wa Ndege wa GIG zipo katika maeneo yote ya Kituo cha 2. Unaweza kupanga safari yako ukitumia taarifa zilizo hapa chini.

Kituo cha 1 katika GIG

 • Azul Linhas Aéreas
 • GOL

Kituo cha 2 katika GIG

 • Aerolíneas Argentinas
 • Air Canada
 • Air France
 • Alitalia
 • American
 • Avianca
 • Condor
 • Copa
 • Delta
 • Edelweiss
 • Emirates
 • Iberia
 • KLM
 • LATAM
 • Lufthansa
 • Passaredo
 • Royal Air Maroc
 • TAAG
 • TAP Air Portugal
 • United
 • American Airlines Admirals Club
 • Ukumbi wa GOL Premium
 • Ukumbi wa Plaza Premium

Kituo cha kimataifa katika Uwanja wa Ndege wa GIG

Uwanja wa Ndege wa GIG una safari za moja kwa moja za kimataifa kwenda maeneo 25 kutoka Kituo cha 2.

Kupata chakula katika Uwanja wa Ndege wa GIG

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Rio de Janeiro-Galeão una aina mbalimbali za sehemu za kula katika vituo vyote. Una zaidi ya maeneo 60 ya kula yakiwemo migahawa maarufu ya kuuza vyakula vya kufungashiwa na migahawa iliyo na huduma ya kulia mezani. Maeneo mengi ya kupata chakula katika Uwanja wa Ndege wa GIG yapo katika Kituo cha 2 na yanauza piza, sushi, gelato na vitafunio.

Kusafiri kwenye Uwanja wa Ndege wa GIG

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Rio de Janeiro-Galeão hauna mfumo wa usafiri wa ndani.

Mambo ya kufanya katika Uwanja wa Ndege wa GIG

GIG una zaidi ya maduka 65, yakiwemo yanayouza vifaa vya kielektroniki, zawadi, dafina na nguo. Kuna spaa katika Kituo cha 2 kwenye ghorofa ya 3.

Kubadilisha sarafu katika Uwanja wa Ndege wa GIG

Ofisi za kubadilisha fedha katika Uwanja wa Ndege wa GIG zipo katika zaidi ya maeneo 5 katika pembe zote za uwanja.

Hoteli karibu na Uwanja wa Ndege wa GIG

Iwe unasubiri ndege nyingine au ndege imechelewa usiku kucha, au kama unahitaji mahali pa kukaa karibu na GIG, kuna zaidi ya hoteli 15 na maeneo ya kulala karibu.

Sehemu za kuvutia karibu na Uwanja wa Ndege wa GIG

 • Christ the Redeemer
 • Copacabana Beach
 • Pão de Açúcar
 • Tijuca National Park

Pata maelezo zaidi kuhusu Uwanja wa Ndege wa GIGhapa.

Facebook
Instagram
Twitter

Ukurasa huu una taarifa kutoka kwenye tovuti za washirika wengine ambazo hazisimamiwi na Uber na zinaweza kugeuzwa au kubadilishwa mara kwa mara. Maelezo yoyote yaliyojumuishwa kwenye ukurasa huu ambayo hayahusiani moja kwa moja na Uber au kazi zake yanatumika kuarifu tu na hayafai kutegemewa, au kuchukuliwa au kufasiliwa kwa namna inayoweka dhamana ya aina yoyote, iwe ya moja kwa moja au inayokisiwa, kuhusu maelezo yaliyo hapa. Baadhi ya masharti na vipengele hutofautiana kutegemea nchi, eneo na jiji. Ofa ya punguzo inawalenga watumiaji wapya pekee. Huwezi kutumia ofa hii pamoja na ofa nyinginezo na haiwezi kutumiwa katika bakshishi. Inapatikana kwa muda mfupi. Vigezo na masharti ya ofa vinaweza kubadilika.