Ruka uende katika maudhui ya msingi

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dallas Fort Worth (DFW)

Tumia Uber kwenda popote, iwe unasafiri kutoka Uwanja wa Ndege wa DFW hadi tangi la samaki la Dallas au bustani.

2400 Aviation Drive, Uwanja wa Ndege wa DFW, TX 75261
+1 972-973-3112

Njia bora zaidi ya kusafiri

Itisha usafiri kote ulimwenguni

Bonyeza tu kitufe ili upate usafiri wa angani katika zaidi ya viwanja vikuu 500.

Safiri kama mwenyeji

Acha App na dereva wako ashughulikie masuala ya kina ili usisumbuke kutafuta maelekezo katika jiji ambapo wewe ni mgeni.

Safiri bila wasiwasi kwa kutumia Uber

Pata vipengele unavyovipenda, ikiwa ni pamoja na bei zinazooneshwa moja kwa moja na uwezo wa kulipa bila pesa taslimu, hata ukiwa ugenini.

Punguzo la hadi $15

Pata punguzo la $5 kwenye safari zako tatu za kwanza. Tumia kuponi ya ofa NEWRIDER15. Muda wa kuitumia unakwisha siku 30 baada ya kuweka kuponi ya ofa kwenye akaunti yako ya Uber.

Aina za usafiri ukiwa eneo husika

 • UberX

  1-3

  Affordable everyday trips

 • Comfort

  1-3

  Newer cars with extra legroom

 • UberXL

  1-5

  Affordable rides for groups up to 5

 • Connect

  1-4

  Send packages to friends & family

1/4

Kupata gari kwenye Uwanja wa Ndege wa DFW

Ita gari ukiwa tayari kutoka nje

Chagua aina ya gari linalotosha idadi ya wasafiri na mizigo mliyo nayo.

Ondoka kupitia ghorofa ya wanaowasili

Elekea nje kisha utafute bango la kuchukua wasafiri. Hapa ndipo madereva wote washirika wa Uber katika uwanja wa ndege wa DFW huwapata na kuwachukua wasafiri.

Thibitisha mahali ulipo

Weka kituo chako na namba ya mlango ili dereva wako ajue mahali atakapokukuta.

Ada za maegesho katika Uwanja wa Ndege wa DFW

Ikiwa unapanga safari ya kwenda Uwanja wa Ndege wa DFW na unatarajia kuendesha gari, unaweza kupata ada za maegesho hapa.
Ada za maegesho katika Uwanja wa Ndege wa DFW

Ada

$31 kwa siku
$24 kila siku
$12 hadi $15 kila siku
$10 kila siku
Huenda ada za maegesho zikawa zimebadilika; taarifa hii iliwekwa Tarehe 20 Novemba, 2018.

Ramani ya Uwanja wa Ndege wa DFW

Uwanja wa Ndege wa DFW una vituo 5. Kila kituo kina maegesho karibu nacho. Kituo cha D kinashughulikia wanaowasili na kuondoka kutoka na kuenda safari za kimataifa.

Maswali ambayo wasafiri wanauliza sana

 • Ndiyo. Bonyeza hapa ili uone orodha ya viwanja vya ndege kote duniani unakoweza kuitisha usafiri wa Uber.

 • Nauli ya usafiri wa Uber kuenda (au kutoka) Uwanja wa Ndege wa DFW inategemea hali kama vile aina ya usafiri, kadirio ya umbali na muda wa safari, ada ya vibali barabarani na idadi ya maombi ya usafiri.

  Unaweza kuona kadirio la bei kabla ya kuitisha usafiri kwa kuweka eneo la kuchukuliwa na mahali unakoenda katika zana ya kukadiria nauli katika Uber hapo juu. Kisha, unapoitisha usafiri utaona nauli yako halisi kwenye app kwa kutegemea hali za wakati huo.

 • Maeneo ya kuchukuliwa yanategemea aina ya usafiri unaoitisha na ukubwa wa uwanja wa ndege. Fuata maagizo kwenye App kuhusu eneo utakakomkuta dereva wako. Unaweza pia kuangalia mabango yanayoashiria maeneo ya usafiri wa pamoja yaliyobainishwa kwenye uwanja wa ndege.

  Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kupitia programu.

 • Msimbo wa uwanja wa ndege DFW ni ufupisho wa Dallas Worth, Texas, Marekani.

Maelezo zaidi

Unatumia mfumo wa Uber kuendesha gari?

Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kurahisisha huduma unayopokea katika viwanja vya ndege, zikiwemo sheria na kanuni za nchi husika.

Je, unaelekea uwanja tofauti wa ndege?

Unaweza kupelekwa na kuchukuliwa kutoka zaidi ya viwanja 600 vya ndege kote duniani.

Maelezo kwa wageni kwenye Uwanja wa Ndege wa DFW

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dallas Fort Worth ni wa 4 kwa shughuli nyingi duniani, kwa kuzingatia idadi ya ndege zinazosafiri. Ni uwanja mkuu wa kimataifa kwa eneo zima la Dallas na Fort Worth, upo umbali unaokaribia kuwa nusu kwa nusu kutoka katikati ya jiji la Dallas (maili 20; kilomita 32) na Fort Worth (maili 23; kilomita 37). Inachukua juu kidogo tu ya dakika 20 kufikia uwanja wa ndege kutoka pande zote katika hali za kawaida za barabarani.

Vituo katika Uwanja wa Ndege wa DFW

DFW umegawanywa katika vituo 5: A, B, C, D na E. Kituo cha D ndicho kituo cha kimataifa huku kikiwa na malango 28, ingawa baadhi ya ndege za safari za kimataifa hutokea Kituo cha A. Kumbi za Uwanja wa Ndege wa DFW zipo katika vituo vyote. Unaweza kupanga safari yako ukitumia taarifa zilizo hapa chini.

Kituo cha A katika DFW

 • American
 • American Airlines Admirals Club

Kituo cha B katika DFW

 • American Eagle
 • American Airlines Admirals Club

Kituo cha C katika DFW

 • American
 • American Airlines Admirals Club

Kituo cha Kimataifa cha DFW (D)

Kupanda kwa ajili ya safari za kimataifa katika Uwanja wa Ndege wa Dallas hufanyika katika Malango ya D5 na D40. DFW una safari 57 za moja kwa moja za kimataifa. Kituo cha D kina kumbi za mashirika kadhaa ya kimataifa, yakiwemo British Airways, Lufthansa na Qantas. Kadhalika, kina American Airlines Admirals Club. Kituo hicho kina makampuni yafuatayo ya ndege:

 • Aeroméxico
 • American
 • Avianca
 • British Airways
 • Emirates
 • Icelandair
 • Interjet
 • Japan Airlines
 • Korean Air
 • Lufthansa
 • Qantas
 • Qatar Airways
 • Sun Country
 • Volaris
 • Wow

DFW Terminal E

 • Air Canada
 • Alaska
 • American
 • Delta
 • Frontier
 • JetBlue
 • Spirit
 • United
 • WestJet
 • Delta Sky Club
 • United Club

Kupata chakula DFW

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dallas Fort Worth una chaguo nyingi za sehemu za kula katika vituo vyote. Huku kukiwa na chaguo zaidi ya 100, wasafiri wanaweza kuchagua maeneo wanayopenda ya kupata chakula, yakiwemo maduka ya kahawa, migahawa inayouza vyakula vya kufungashiwa na baa katika Uwanja wa ndege wa DFW. Wasafiri ambao wanapendelea huduma ya kulia mezani wanaweza kuchagua migahawa iliyo katika uwanja wa ndege wa DFW.

Kusafiri ukiwa DFW

Baada ya kupita sehemu ya ukaguzi wa usalama, wasafiri katika DFW wanaweza kutumia Skylink, ambao ni mfumo wa treni ya kiotomatiki wa kusafiria kati ya vituo vyote 5. Treni husafiri kila baada ya dakika 2 na zinaweza kwenda kasi ya maili 35 kwa saa. Kila kituo kati ya vituo 5 kina stesheni 2, zilizo katika maeneo yafuatayo ya lango:

 • Kituo cha A: kati ya A13 na A16 na kati ya A28 na A33
 • Kituo cha B: kati ya B10 na B12 na kati B28 na B31
 • Kituo cha C: kati ya C8 na C12 na kati ya C27 na C31
 • Kituo cha D: kati ya D11 na D21 na kati ya D24 na D36
 • Kituo cha E: kati ya E8 na E12 na kati ya E31 na E32

Isitoshe, kabla ya ukaguzi wa usalama, Terminal Link huviunganisha vituo vyote katika Uwanja wa Ndege wa DFW na mfumo wa mabasi.

Mambo ya kufanya ukiwa DFW

Uwanja wa ndege wa DFW una mpango wa sanaa unaoonesha kazi za wasanii wa karibu, nchini na wa kimataifa, ikijumuisha wanaochonga vinyago, wanaochora, wanaounda nakshi na kadhalika. Sanaa nyingi zinapatikana katika Kituo cha D baada ya kupitia ukaguzi wa usalama na katika vituo vya Skylink. Sehemu ya watoto kuchezea karibu; kwa watu wazima, kuna sehemu 2 za watu wazima kuchezea (karibu na Lango 42 katika Kituo cha B na Lango 16 katika Kituo cha E) zinatoa michezo ya kisasa zaidi ya video kwa wasafiri, pamoja na vifaa vya kusikilizia masikioni na viti vizuri vya ngozi. Kuna saluni mbili kwa ajili ya nywele katika Kituo cha A na Kituo cha D.

Kubadilisha sarafu katika uwanja wa ndege wa DFW

Ofisi za kubadilisha sarafu katika uwanja wa ndege wa Dallas zipo waziwazi katika Kituo cha D (Kituo cha Kimataifa), karibu na malango ya 11, 22 (nje ya eneo la ukaguzi wa usalama), 24 na 36. Sehemu nyingine ya kubadilisha sarafu ipo katika Kituo cha A karibu Lango la 29.

Hoteli zilizo karibu na DFW

Iwe unasubiri ndege nyingine au ndege imechelewa usiku kucha, au kama unahitaji mahali pa kukaa karibu na DFW, kuna hoteli nyingi na maeneo ya kulala karibu.

Vivutio karibu na DFW

 • Bustani ya Fort Worth Botanic Garden, Fort Worth
 • Fort Worth Stockyards, Fort Worth
 • Pioneer Plaza, Dallas

Pata maelezo zaidi kuhusu DFW hapa.

Facebook
Instagram
Twitter

Ukurasa huu una taarifa kutoka kwenye tovuti za washirika wengine ambazo hazisimamiwi na Uber na zinaweza kugeuzwa au kubadilishwa mara kwa mara. Maelezo yoyote yaliyojumuishwa kwenye ukurasa huu ambayo hayahusiani moja kwa moja na Uber au kazi zake yanatumika kuarifu tu na hayafai kutegemewa, au kuchukuliwa au kufasiliwa kwa namna inayoweka dhamana ya aina yoyote, iwe ya moja kwa moja au inayokisiwa, kuhusu maelezo yaliyo hapa. Baadhi ya masharti na vipengele hutofautiana kutegemea nchi, eneo na jiji. Ofa ya punguzo inawalenga watumiaji wapya pekee. Huwezi kutumia ofa hii pamoja na ofa nyinginezo na haiwezi kutumiwa katika bakshishi. Inapatikana kwa muda mfupi. Vigezo na masharti ya ofa vinaweza kubadilika.