Pata chochote unachohitaji ili uweze kufuatilia mafanikio yako unaposafiri.
Dhibiti njia zako za kulipa, kagua historia ya safari na zaidi.
Unaona maelezo ya Washington D.C.. Ili uone vipengele na huduma zilizo mahali pengine, tafadhali chagua mji tofauti.
Tumia Uber kurahisisha safari za kutoka Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam, kuingia na kutoka jijini.
Julius K. Nyerere Road, Dar es Salaam, Tanzania
+255 22-284-4371
Bonyeza tu kitufe ili upate usafiri wa angani katika zaidi ya viwanja vikuu 500.
Acha App na dereva wako ashughulikie masuala ya kina ili usisumbuke kutafuta maelekezo katika jiji ambapo wewe ni mgeni.
Pata vipengele unavyovipenda, ikiwa ni pamoja na bei zinazooneshwa moja kwa moja na uwezo wa kulipa bila pesa taslimu, hata ukiwa ugenini.
Sampuli za bei za wasafiri ni makadirio tu na hazioneshi mabadiliko yanayosababishwa na ofa, jiografia kucheleweshwa kwenye foleni na mambo mengine. Tunaweza kutumia nauli isiyobadilika na bei za chini zaidi. Bei halisi za safari na safari zilizopangwa huenda zikawa tofauti.
Itisha bajaji kisasa zaidi na kwa bei poa
Affordable, everyday rides
Affordable rides for groups up to 6
Chagua gari linalotoshea idadi ya wasafiri na mizigo mliyo nayo.
Utapata maelekezo kuhusu maeneo ya kuchukua wasafiri moja kwa moja katika programu. Pia kunaweza kuwa na mabango katika uwanja wa ndege.
Nenda katika eneo la kuchukuliwa jinsi ilivyobainishwa katika App. Tafadhali kumbuka, eneo hilo huenda halitakuwa karibu kabisa na lango unaloondokea. Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kupitia App.
Ofisi ya kuweka vitu vilivyopotea na kupatikana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ipo kabla ya ghorofa ya kwanza katika Kituo cha 2. Ofisi hiyo inatoa huduma za kuulizia bidhaa zilizopotea, sajili ya bidhaa zilizopotea, kuchukua na kuhifadhi bidhaa zilizopotea.
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere una maegesho ya muda mfupi mchana na siku.
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere una kituo cha afya, kwa hivyo huduma za dharura za matibabu zinaweza kutolewa kwa wanaohitaji.
Iwe umewasili au unajiandaa kuondoka Dar es Salaam, Uber iko tayari kukufikisha unapotaka kwenda.
Nauli hutegemea wakati, upatikanaji na masuala mengine. Angalia mfumo wa Uber wa kukadiria nauli ili ufahamu itakugharimu hela ngapi kusafiri.
Maeneo ya kuchukuliwa yanaweza kubadilika, kwa hivyo hakikisha kwamba umeangalia programu ya Uber mara kwa mara baada ya kuitisha usafiri.
Hubadilika kutegemea wakati, foleni na idadi ya madereva walio kazini.
Uber ndio usafiri bora zaidi unaposafiri kati ya Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere hadi katikati mwa jiji la Dar es Salaam. Uwanja huu wa kimataifa upo takriban kilomita 13 (maili 8) kutoka katikati mwa jiji la Dar es Salaam; na jina lake linatokana na Rais wa kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere. Uwanja wa Ndege wa DAR huhudumia takriban wasafiri milioni 3.5 kila mwaka sambamba na safari hizi kuelekea nchi nyingine za Afrika, Ulaya na Mashariki ya Kati. Uber itakusaidia kurahisisha safari yako kwa kukusafirisha kutoka kwenye uwanja wa ndege hadi unakoenda na kukurudisha kwenye uwanja uda wa safari yako ya ndege ukifika.
Kuna vituo 2 vinavyohudumia wasafiri wa ndani ya nchii na wa kimataifa. Ujenzi wa kituo cha 3 utakamilika mwaka wa 2019. Kituo cha 1 kinahudumia wasafiri wa ndani ya na ndege ndogo. Kituo cha 2 kwenye Uwanja wa Ndege wa DAR kinahudumia wasafiri wa kimataifa na ndege kubwa za safari za ndani ya nchi.
Hakuna huduma za mabasi kati ya vituo. Kwa safari za kwenda katikati ya mji, unaweza kuabiri basi wakati wowote kutoka kwenye vituo vilivyo takribani mita 500 (theluthi moja ya maili) kutoka Kituo cha 1 na umbali wa mita 100 kutoka Kituo cha 2. Hoteli nyingi pia hutoa huduma za usafiri kutoka na kwenda kwenye uwanja wa ndege ni nzuri kwa safari za kuunganisha haraka.
Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam una vyakula vingi. Uwanja huu wa ndege una migahawa mbalimbali na aina nyingi za vyakula.
Uwanja wa Ndege wa DAR una maduka ya bidhaa zisizotozwa kodi ambako unaweza kupata bidhaa ikiwa ni pamoja na vitafunwa na sabuni kwa bei nafuu. Kuna uwezekano wa kupata unachohitaji, iwe unachukua hedaya au kitu cha kukumbuka safari
.Ikiwa unasafiri alfajiri au unahitaji mahali panapokufaa kutulia kabla au baada ya safari, hoteli karibu na Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam zina vyumba vya kulala. Kuna hoteli za mbali na za karibu na uwanja wa ndege kwa bei mbalimbali. Hutakosa inayokufaa. Angalia hoteli yako ili uone ikiwa ina huduma ya kupelekwa kwenye uwanja wa ndege, au uitishe usafiri wa Uber ili upelekwe kwa urahisi kwenye uwanja wa ndege.
Unaweza kufanya mambo mbalimbali mjini Dar es Salaam, yakiwemo kutembelea:
Pata maelezo zaidi kuhusu Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere hapa.