Ruka uende katika maudhui ya msingi
Uber
Uber

Uwanja wa Ndege wa Paris-Charles de Gaulle (CDG)

Iwe unasafiri kuelekea Paris kutoka Uwanja wa Ndege wa CDG au kutoka Paris kuelekea Uwanja wa Ndege wa CDG, iamini Uber kukufikisha unakoenda.

95700 Roissy-en-France, France
+33 1-70-36-39-50

Itisha usafiri kote ulimwenguni

Bonyeza tu kitufe ili upate usafiri wa angani katika zaidi ya viwanja vikuu 500.

Safiri kama mwenyeji

Acha programu na dereva wako ashughulikie masuala ya kina ili usisumbuke kutafuta maelekezo katika jiji ambapo wewe ni mgeni.

Safiri bila wasiwasi kwa kutumia Uber

Pata vipengele unavyovipenda, ikiwa ni pamoja na bei zinazooneshwa moja kwa moja na uwezo wa kulipa bila pesa taslimu, hata ukiwa ugenini.

Sampuli za bei za msafiri ni makadirio tu na hazioneshi mabadiliko yanayotokana na mapunguzo, kucheleweshwa kwenye foleni na mambo mengine. Tunaweza kutumia nauli isiyobadilika na bei za chini zaidi. Bei halisi zinaweza kubadilika.

 • UberX1-4

  Affordable, everyday rides

 • Berline1-4

  Premium rides in luxury cars

Fungua programu yako ili kuitisha usafiri

Ukishakuwa tayari, fungua programu yako na uitishe usafiri. Chagua usafiri unaotoshea idadi ya wasafiri na mizigo mliyo nayo.

Fuata maelekezo katika programu

Utapata maelekezo ya eneo la kuchukuliwa moja kwa moja kwenye programu. Pia kunaweza kuwa na alama katika uwanja wa ndege.

Kutana na dereva wako

Nenda katika eneo la kuchukuliwa jinsi ilivyobainishwa katika programu. Tafadhali kumbuka, eneo hilo huenda halitakuwa karibu kabisa na lango unaloondokea. Ikiwa humpati dereva wako, wasiliana naye kupitia programu.

WiFi katika uwanja wa Charles de Gaulle

Huduma ya WiFi inayotolewa na Uwanja wa Ndege wa CDG bila malipo unakuwezesha kufikia intaneti bila kikomo, pia kuna chaguo la WiFi ya kulipia kwa wanaotaka muunganisho wenye kasi zaidi.

Maegesho katika uwanja wa ndege wa Charles de Gaulle

Charles de Gaulle ina aina nyingi za maegesho, yakiwemo maegesho ya kuchukua na kushukisha wasafiri kwa haraka. Pia kuna maegesho ya muda mfupi na ya muda mrefu. CDG ina mabasi ya kusafirisha wasafiri kutoka katika maeneo ya maegesho kwenda kwenye uwanja wa ndege.

Kuhifadhi mizigo katika Uwanja wa Ndege wa Charles de Gaulle

Sehemu za kuhifadhi mizigo katika uwanja wa ndege wa CDG hukuruhusu kuhifadhi mzigo wako kwa saa au siku, kulingana na ratiba au mpango wako wa safari.

Uber inapatikana katika Uwanja wa Ndege wa Charles de Gaulle, kwa hivyo unaweza kufurahia usafiri wa starehe na uhakika popote unapotaka kwenda.

Ili kupata eneo la kuchukuliwa, angalia programu ya Uber baada ya kuitisha usafiri.

Hata kama safari si ndefu sana, ada za Uber kutoka na kwenda Uwanja wa Ndege wa Charles de Gaulle zinaweza kuathiriwa na muda, foleni na masuala mengine. Angalia mfumo wa kukadiria nauli wa Uber ili ufahamu makadirio ya nauli ya safari.

Muda wa kuchukuliwa unaweza kutofautiana kulingana na wakati, idadi ya madereva wanaopatikana na masuala mengine.

Unatumia mfumo wa Uber kuendesha gari?

Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kurahisisha huduma unayopokea katika viwanja vya ndege, zikiwemo sheria na kanuni za nchi husika.

Je, unaelekea uwanja tofauti wa ndege?

Unaweza kupelekwa na kuchukuliwa kutoka zaidi ya viwanja 500 vya ndege kote duniani.

Uber ni chaguo bora kwa wasafiri wanaowasili au kuondoka Uwanja wa Ndege wa CDG. Uwanja wa Ndege wa Charles de Gaulle—unaojulikana pia kama Uwanja wa Ndege wa Roissy—ndio uwanja mkubwa zaidi wa kimataifa nchini Ufaransa. Iwe unaelekea Disneyland au Paris, ni chaguo linalowafaa wasafiri wa nchini na wa kimataifa. Uwanja wa Ndege wa Charles de Gaulle unapatikana takribani kilomita 25 (maili 15) kaskazini mwa Paris, hivyo kuufanya chaguo bora zaidi kwa wageni wanaozuru mji huu mkuu na maarufu wa Ufaransa. Kuna watalii wanaotembelea eneo pana la Paris.

Vituo kwenye Uwanja wa Ndege wa Charles de Gaulle

Uwanja wa Ndege wa Charles de Gaulle una vituo 3 vya wasafiri: T1, T2 na T3.

Kituo cha 1 kwenye CDG

Mashirika yafuatayo,miongoni mwa mengine yanatoa huduma katika Kituo cha 1:

 • Aegean
 • Malaysia
 • Qatar

Kituo cha 2 kwenye CDG

Kituo cha 2 kimegawanywa katika zaidi ya vituo 7 vidogo, 2A hadi 2G na kina kituo cha reli cha TGV-RER kinachojulikana kama Aéroport Charles de Gaulle 2. Mashirika yafuatayo yanahudumia Kituo cha 2:

 • Air France
 • British Airways
 • Cathay Pacific

Kituo cha 3 kwenye CDG

Shirika hili miongoni mwa mengine yanahudumia Kituo cha 3:

 • Jordan Aviation

Vyakula katika Uwanja wa Ndege wa Paris-Charles de Gaulle

Utapata aina nyingi za vyakula na vinywaji katika Uwanja wa Ndege wa CDG. Vyakula hivi ni vya Kifaransa na vya kimataifa. Migahawa kwenye Uwanja wa Ndege wa Charles de Gaul hutoa huduma yoyote ya mapishi unayotaka.

Kusafiri kwenye Charles de Gaulle (CDG)

CDGVAL inaweza kukusafirisha kati ya vituo mbalimbali vya Charles de Gaulle kutoka maegesho yake 2. Pia kuna kituo cha mabasi na magari ya uwanja wa ndege. Unaweza pia kusafiri moja kwa moja hadi Paris kwa kutumia barabara ya RER B kupitia Vituo vya 2 na 3.

Mambo unayoweza kufanya katika Uwanja wa Ndege wa Charles de Gaulle

Maduka kwenye Uwanja wa Ndege wa CDG yana kila unachohitaji, iwe unatafuta mvinyo, vileo, vipodozi au zawadi za ukumbusho kutoka Paris. Elekea Chanel au Swarovski ili kupata vito na saa, au uchague baadhi ya mavazi ya kisasa zaidi kutoka Prada, Dior, Gucci na kwenye maduka mengine mengi ya mavazi yanayotambulika kote ulimwenguni. Uwanja wa Ndege wa Charles de Gaulle pia una sehemu ya watoto kucheza, pamoja na vyumba vya maombi na sebule.

Hoteli kwenye Uwanja wa Ndege wa Charles de Gaulle

Kuna hoteli 2 zinazopatikana ndani ya Kituo cha 2. Hii inawafaa watu wanaowasili jioni au alfajiri. Kando na haya, kuna hoteli mbalimbali za kifahari katika eneo la Roissy, ambapo uwanja wa Ndege wa Charles de Gaulle unapatikana. Mji wa Paris una vyumba mbalimbalii vya kulala vilivyoundwa kufaa kila msafiri kulingana na uwezo wake wa kifedha.

Maeneo ya kuzuru karibu na Uwanja wa Ndege wa Paris-Charles de Gaulle

Ukiwa kwenye kituo katika Uwanja wa Ndege wa Charles de Gaulle na una muda wa kutosha kufika katikati mwa mji wa Paris—utahitaji muda wa angalau saa 6—kuna maeneo mengi ya kihistoria unayoweza kuzuru. Magari mengi yanayounganisha CDG na katikati mwa Paris.

 • Arc de Triomphe
 • Champs-Élysées
 • Eiffel Tower
 • Makavazi ya Louvre
 • Notre-Dame de Paris
 • Kasri ya Versailles

Pata maelezo zaidi kuhusu Uwanja wa Ndege wa Paris-Charles de Gaulle hapa.