Bidhaa

Usaidizi kwa kubonyeza kitufe

Tarehe 15 Machi, 2017 / Tanzania

Uber, sisi hufanya jitihada usiku na mchana ili kutoa huduma iliyo bora zaidi kadri iwezekanavyo kwa madereva na abiria katika miji yote duniani kote. Lakini pia tunafahamu kuwa ni lazima kutakuwa na nyakati ambazo utahitaji kuwasiliana na sisi: mkoba umesahaulika kwenye gari, nauli isiyo sahihi, tatizo kwenye programu yako.

Unapohitaji kuwasiliana na sisi, lengo letu ni kurahisisha mchakato huu wa kuwasiliana nasi kwa uwepesi kadri iwezekanavyo ili kuweza kupata huduma inayokuridhisha.

Licha ya yote, kama unaweza kufanya safari kwa kubonyeza kitufe tu, kwanini usiweze  kupata huduma nzuri ya msafiri vilevile kiganjani mwako iwapo umepata tatizo? Mrejesho? Njia rahisi ya kupata majibu kwenye programu yako.

 

Unahitaji kuulizia koti lako ulilopoteza ulivyotoka usiku? Unahitaji kuangalia tathmini ya msafiri wako? Wasilisha swali kuhusu risiti unayodhani haiko sawa au njia ya safari iliyo na mashaka.

Bonyeza “Usaidizi” kwenye programu na maelezo yote utakayohitaji yatakuwa hapo.

 

 

Usaidizi unaoweza kupata kwenye programu yako ni rahisi kama kuomba safari!