Bidhaa

Dar Es Salaam UberBoda imefika!

Tarehe 24 Julai, 2019 / Tanzania

Dar es Salaam, tuna furaha kubwa kukutangazia kwamba sasa huduma ya Uber Boda inapatikana.

Sasa unaweza kufanya safari zako jijini bila ugumu wowote kwa nauli ndogo kuanzia TZS 1,000 na unapata usafiri wa kukuchukua na kukupeleka hadi mlangoni mwa mahali unakoenda. 

Epuka foleni na fika uendako kwa wakati kwa kutumia Uber Boda ndani ya app yako ya Uber. Huna uhakika jinsi ya kuomba safari ya Uber Boda? Hakuna shaka, hatua chache tu zitakuwezesha kusafiri bila shida.

> Fungua app ya Uber kisha andika unakoenda.

>Chagua Uber Boda Hakiki bei kisha hakiki Uber Boda

>Subiri dereva aliye karibu nawe kupokea ombi lako

>Sasa unaweza kuona taarifa za dereva wako na muda atakofika.


Kwa usalama zaidi tumewapatia madereva wa boda kofia ngumu 2 na reflective vest 2 na kila dereva hupitia mafunzo maalum ya usalama kabla ya kuingia barabarani kwa mara ya kwanza kama dereva mshiriki wa Uber.


Baadhi ya maeneo ambayo Uber Boda inapatikana kwa sasa: Mikocheni, Msasani, Kawe, Mbezi, Mwenge, Kinondoni, Kigamboni, Buguruni, Manzese and Kurasini.

Fika uendako kwa wakati ukitumia Uber Boda. Pia inapatikana kwenye app yetu mpya ya Uber Lite, pakua HAPA