Bidhaa

Sasa unaweza kutoa tip!

Tarehe 16 Aprili, 2019 / Tanzania

Kuwa dereva ni zaidi ya kumtoa msafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine. Madereva washirika wanajituma kila siku kukurahisishia mambo yako – kwa kukupeleka kwenye mikutano muhimu ya kibiashara, mtoko wako wa kwanza au kushuhudia dimba likisakatwa – wanajituma sana.

Sasa unaweza kuwapa madereva tip moja kwa moja kwenye app ya Uber baada ya safari kama shukrani kwa juhudi yao. Tip ni namna nyingine ya kumshukuru dereva kwa kazi nzuri anayofanya ya kutoa huduma ya usafiri kwa weledi mkubwa.

Je, ulikuwa unawahi mali akatumia mchepuko kukwepa foleni kubwa ya magari? Je ulifurahia safari yako kwa mazungumzo ya kuchekesha? Unaweza kuonyesha shukrani zako  kwa kumpatia tathmini ya nyota 5 na umpatie tip mwishoni mwa safari yako.

Inavyofanya kazi:

  • Ongeza tip baada ya kutoa tathmni yako.
  • Chagua kiasi chochote au uweke kiasi unachotaka mwenyewe.
  • Bonyeza Nimemaliza ili utume tip.
  • Pesa zote za tip zitatumwa kwa dereva moja kwa moja, Uber haitatoza adayoyote ya huduma kwenye tip.

*Pakua toleo jipya la app. Mpango wa kutoa tip ndani ya app unatumika kwa wasafiri wanaotumia kadi ya benki kama njia yao ya malipo.