Bidhaa

Tunakulete Uber Lite

Tarehe 5 Machi, 2019 / Tanzania

Njia mpya na nyepesi ya kuomba safari.

Haijalishi wewe ni nani na wapi ulipo, dhumuni letu ni kukuwezesha kufanya safari iliyo salama, yenye kuaminika na unayoweza kumudu. Kufanya hivi inamaanisha tunaangalia ndani na nje ya mifumo yetu kuona jinsi gani tunaweza kukithi mahitaji ya watu kila sehemu. Ndio maana tunatambulisha Uber Lite iliyotengenezwa kwaajili ya Android.Uber Lite ni toleo la Uber app iliyotengenezwa kwaajili ya vifaa vyenye data, uhifadhi, na mtandao hafifu.

Chaguo bora kwaajili yako

Japo ni mtumiaji wa mara kwa mara wa Uber unaweza ukawa unatafuta njia ya kuomba safari ukiwa nchi nyengine, au ni mtumiaji mpya wa Uber mwenye bando dogo. Uber Lite inakupa uwezo zaidi wa kufanya mizunguko.

Kwa wakati gani utumie Uber Lite

 • Mara kwa mara umekua ukiwa na uhifadhi mchache na kulazimika kufuta app kwenye simu yako na kuzipakua tena pindi utakapo zihitaji.
 • Mara nyingi simu yako imekua ikipata shida kufungua app au kukwama ukiwa unaitumia.
 • Mara nyingi simu yako imekua na bando dogo na uokoaji wa bando ni kitu ambacho uko makini sana nacho au mara nyingi uko sehemu ambayo haina wifi.

Kwa wakati gani utumia Uber na Uber LIte

 • Mara nyingine umejikuta ukiwa kwenye eneo lenye mtandao hafifu.
 • Mara nyingine umekua ukiishiwa bando au kusafiri nchi nyigine ambapo bando ni la ghari.
 • Unatumia Uber ukiwa kenye eneo lenye wifi na Uber Lite ukiwa unataka kuokoa bando lako.

Kwa wakati gani utumie Uber

 • Unapenda utumizi wa Uber na ni kwa mara chache au hujawahi kabisa kuwa na tatizo la app,bando au mtandao.
 • Inaendana na simu yangu?
 • Itafanya kazi na app yangu kuu?
 • Uber Lite ina ukubwa gani?
 • Kuna tofauti gani kuu kwenye hizi app?
 • Inafanya kazi bila mtanadao?
 • Ramani ziko wapi?
 • Je UBER Lite ni ya gharama ileile?
 • Wapi naweza pakua Uber Lite.