Bidhaa

Kutumia Uber app, mbona simpo!

Tarehe 25 Juni, 2018 / Tanzania

Tunapenda kuona ukifurahia huduma ya Uber, na katika kuhakikisha hilo tumekutengenezea vidokezo vya kufanya maisha yako yawe marahisi wakati wowote pale unapotumia Uber; Kuanzia kwenye kupakua app mpaka kuwasiliana na huduma kwa wateja.

Kupakua app

Kupakua app ya Uber ni rahisi sana! Tembelea ‘Playstore’ kwa Android na ‘App store’ kama unatumia IOS, andika ‘Uber’ na uchague app ya juu kabisa.

Hakikisha unawasha location kwenye settings za simu yako ili uweze kuomba usafiri.

Kujisajili

Ili kupata huduma ya Uber ni muhimu kujisali, na haichukui hata dakika. Ili kujisajili fuata hatua hizi;

 1. Andika namba yako ya simu ( hakikisha ni namba ambayo inapatikana. Hakikisha unapoandika namba inaanza na (+255)  )
 2. Andika Jina lako la kwanza na la mwisho

Kuomba Usafiri

Wakati wa kuomba safari, Uber hukutafutia dereva ambae yupo karibu yako. Ili kufanikisha upatikanaji wa dereva aliye karibu, hakikisha umewasha location kwenye settings za simu yako halafu fuata hatua hizi;

 1. Andika unapoelekea
 2. Chagua aina ya usafiri
  1. UberPOA kwa bajaji
  2. UberX kwa magari ya kawaida (mpaka watu wanne)
  3. UberXL kwa magari makubwa (mpaka watu 6 mpaka 7)
 3. Hakikisha eneo la kuchukuliwa, baada ya hapo utaunganishwa na dereva aliye karibu nawe.
 4. Hakikisha umeangalia nauli yako na umekubaliana nayo kabla ya kupanda usafiri.

Huduma kwa wateja

Huduma yetu kwa wateja hupatikana ndani ya app yako ya Uber. Ili kuwasiliana na huduma kwa wateja, fuata hatua hizi;

 1. Fungua app yako
 2. Bonyeza ‘Menu’ (Mistari mitatu – kushoto juu ya app yako)
 3. Bonyeza ‘help’, na utaona sehemu ya kuripoti tatizo lolote kuhusiana na safari zako za Uber

Ni rahisi sana kutumia App ya Uber, Popote pale ndani ya Dar ES Salaam tutakufikisha. #UberMovingTanzania.