Bidhaa

Tumezindua huduma ya uberXL

Tarehe 24 Aprili, 2018 / Tanzania

Kupitia uberXL unapata usafiri wenye nafasi ya kubeba watu wengi

Bila shaka haifai sana unapolazimika kuita magari mengi kwa sababu uko na wasafiri wengi au una safari ya uwanja wa ndege na mizigo mingi na gari lenyewe ni dogo. Tumezindua huduma ya uberXL, itakayokuwa suluhisho la kero hii.

Ukitumia huduma ya uberXL, unaweza kuita gari ambalo linaweza kubeba wasafiri 7 ndani ya gari moja. Angalia nauli inayotozwa:

  • Nauli Msingi: TZS 2,000
  • Kwa kila Kilometa: TZS 800
  • Kwa kila Dakika: TZS120
  • Nauli ya Chini: TZS 5,000

Hakuna haja ya kuita magari mengi kwa sababu wasafiri ni wengi au kupata usumbufu wa safari ya uwanja wa ndege kwa sababu una mizigo mingi. Huduma ya uberXL inaleta mwafaka kwenye matatizo haya!