Matangazo ya Madereva

Tumepata mabadiliko mengine kwa ajili ya dereva-mshirika

Tarehe 30 Oktoba, 2017 / Tanzania

Dereva-mshirika anavyojiunga na Uber, anakuja kwa nia ya kufanya kazi ambayo itaendana na ratiba zake. Kwa sababu ya hili,tunataka  ufurahie kuwa dereva-mshirika wa Uber

Tunapenda kukufahamisha kwamba kutakuwa na mabadiliko mazuri sana hizi wiki chache zijazo! Mabadiliko haya sio ya kuongeza vitu kwenye programu yako ya dereva-mshirika bali ya kukurahisishia wewe ufanyaji wako wa kazi, na kufanya ufurahie kuwa dereva-mshirika wa Uber.

Nini kimeongezeka?

Taarifa ya safari ndefu


Sasa utaarifiwa kama safari ni ndefu kabla ya kukubali ombi la safari, ili uweze kuamua kama utaikubali hiyo safari au la, hamna tena kushtukizwa!

Utalipwa wakati wa kumsubiria msafiri


Ikipita dakika tano baada ya kufika eneo la kumchukua msafiri, msafiri atalipishwa kwa kila dakika ambayo utakuwa unamsubiria ili kuanzisha safari. Hii itawafanya wasafiri waombe safari pale ambapo watataka kuondoka.

Tathmini ya nyota


Kuanzia sasa tathmini ya nyota  zako haitabadilika kutokana na mambo yaliyo juu ya uwezo wako, kama msafiri akitoa maoni ambayo hayaendani na huduma za dereva-mshirika tathmini ya nyota zako haitabadilika.

Uwezo wa kushare taarifa za safari

Kama wasafiri wanavyoweza kushare taarifa za zafari zao kwa marafiki, wewe pia kama dereva-mshirika unaweza kushare taarifa za safari zako kwa marafiki zako

Muda wa kuwasili kwenye eneo unalotaka kwenda

Hii ni feature ambayo itakusaidia kuchagua sehemu unayo taka kwenda, halafu unatafutiwa maombi ya safari yanayoeleka huko - Pia unaweza kuweka muda unaotaka kufika kwenye hilo eneo, nasi tutakusaidia kufika kwa wakati.

Hii sio mwisho, bado tunayakusanya maoni yenu, na kufikiria ni kwa jinsi gani tunaweza kuzidi kuboresha huduma hii.