Matangazo ya Madereva

Njia rahisi ya kutoa pongezi

Tarehe 30 Agosti, 2017 / Tanzania

Kuna muda nyota 5 pekee hazijitoshelezi.

Ndio maana wasafiri huandika ujumbe wa asante kwenye app zao, kuwashukuru madereva kwa kutoa huduma nzuri kwenye safari zao. Muda mwingine ni vitu vidogo tu ambavyo vinaweza kufanya safari yako iwe nzuri zaidi, kama vile kuwekewa mziki mzuri, kusaidiwa ukiwa na mizigo. Tunataka kuhakikisha kwamba madereva wanapata pongezi unazotoa!

Sasa tunaifanya iwe rahisi kwa wasafiri kuwashukuru madereva-washirika. Msafiri akiacha ujumbe wa shukrani, ujumbe utapelekwa kwenye programu ya dereva-mshirika ili kumjulisha dereva ni kitu gani ambacho amekifanya kikakufurahisha katika safari yako.

Tunataka kuwapa wasafiri, fursa ya kuwashukuru na kutambua juhudi ambazo madereva wanaweka ilikufanya safari iwe nzuri zaidi. Ni hatua ndogo tunaichukua ili kurahisisha utoaji wa shukrani na kuwapongeza madereva wanao ongeza jitihada ili kuboresha huduma.

Baada ya abiria kutoa shukrani, dereva atapata ujumbe kwenye programu yake  utakaomuonyesha ni kitu gani kizuri ambacho amefanya kwenye safari, kama ilikuwa ni mziki mzuri, dereva mchangamfu, gari safi na vitu kama hivyo.

Hii ni kwasababu kuna muda ambao  vitu vidogo huleta mabadiliko, na nyota 5 pekee hazitoshi. Tunalitambua hilo, na tunajua kwamba kuna mengi tunaweza fanya kuboresha mazingira ya  kazi ya dereva-mshirka, tumeona ya kwamba kuwashukuru madereva kwa vile wanavyo fanya ni sehemu nzuri ya kuanzia.