Promotions

Usiache kula bata msimu huu wa Valentines!

Tarehe 17 Februari / Tanzania


Siku ya Valentine’s imepita lakini mwezi wa wapendanao unaendelea!

Tunakupa punguzo la 25% kwenye safari 2 za UberX (thamani ya ofa haizidi 1700 kwa kila safari) kwa wiki moja zaidi, ndani ya mwezi wa pili. Tunapenda kuwakutanisha watu kwa hiyo endelea kufurahia na kuweka kumbukumbu nzuri mwenza wako na hata ndugu, jamaa na marafiki.

Je, ungependa kuwa na matembezi na mwenza wako? Changamkia punguzo la safari za Uber, uende Coco Beach na mpezi wako mpate upepe murua mkitembea ufukweni mida ya jioni au kwa ajili ya pikini ya ufukweni. 

Kilele cha mwezi huu wa Valentine’s ni kufurahia dina na mwenza wako. Kwa bahati nzuri jiji la Dar Es Salaama lina viwanja vingi vya kustarehe na kusherehekea siku ya Valentines ukifurahia mapochopocho ya kutamanisha na mwenza wako. Cape Town Fish Market ni sehemu nzuri ya kufurahia mandhari ya bustani ya kupendeza. Bila shaka utapenda upepo mwanana wa bahari huku ukifurahia muziki wa bendi inayotumbuiza live na chakula cha samaki kila aina, kuna milo ya aina mbalimbali ambayo unaweza kufurahia na mwenza wako.

Iwe unataka kutoka na mwenza wako kwa matembezi tu kwenye maeneo yanayovutia au kujumuika na marafiki kufurahia pamoja, usidhani umechelewa kwa sababu siku ya Valentine’s imepita. Ofa ya punguzo la safari za Uber inaendelea kupaisha mwezi wa Valentine’s kwa kukufikisha mahali popote katika jiji kiurahisi.