Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi

Nauli Unazojulishwa Mapema, zimeelezwa

Pata maelezo kuhusu jinsi Nauli Unazojulishwa Mapema zinavyohesabiwa, ni taarifa gani mpya utakayopata na jinsi zinavyoweza kukusaidia ujipatie mapato zaidi siku nzima.

Kwa nini uhamie kwenye Nauli Unazojulishwa Mapema?

Kwa sababu kila safari inapaswa kuwa uamuzi wako. Utapata mwonekano na udhibiti zaidi wa mapato yako.

Utapata taarifa ya ziada kuhusu kila safari mapema ili uweze kuamua ni safari zipi zinazokufaa.

Nauli Unazojulishwa Mapema hurekebishwa ili zipatane kile kinachotokea kwa wakati halisi ili kukusaidia kupata fursa zaidi za kujipatia mapato.

Nauli Unazojulishwa Mapema huhesabiwa vipi?

Ingawa tovuti nyingi bado zinahesabu nauli kwa kila dakika na maili, kwenye Uber, tunajua kwamba kuna mengi kuhusu safari kuliko urefu na umbali wake. Kwa hivyo tuliunda teknolojia ili kufanikisha jambo hili.

Tunapohesabu Nauli Unazojulishwa Mapema, tunazingatia aina 3 muhimu: maelezo, uhitaji na data.

Maelezo ya safari

Maelezo ya msingi ya safari yatazingatia kila wakati jinsi Nauli Unazojulishwa Mapema zinavyohesabiwa. Hii inajumuisha:

  • Urefu wa safari uliokadiriwa

  • Muda wa safari uliokadiriwa

  • Eneo la kuchukuliwa

  • Eneo la kushushwa

Uhitaji wa wakati halisi

Kiasi cha pesa unachoweza kujipatia huathiriwa na uhitaji wa sasa katika eneo lako. Hii inajumuisha:

  • Kuongezeka kwa nauli

  • Ina shughuli nyingi kiasi gani katika eneo lako

  • Ina shughuli nyingi kiasi gani mahali unakoenda

  • Una uwezekano gani wa kupata safari nyingine haraka

  • Msongamano wa magari

Data ya kihistoria

Mienendo na data ya mapato muhimu husaidia kuunda utabiri sahihi zaidi. Hii inajumuisha:

  • Maeneo yenye uhitaji mkubwa na mdogo

  • Maeneo yenye mapato ya juu na ya chini

  • Kadirio la uhitaji katika maeneo

  • Kadirio la uhitaji kwa nyakati mbalimbali siku nzima

Utakachoona mapema

Fanya maamuzi sahihi kuhusu safari unazokubali.

Kiasi cha pesa utakachojipatia, ikiwemo nyongeza ya nauli

Mahali utakapoenda

Muda na umbali hadi eneo la kuchukuliwa

Muda na umbali hadi eneo la kushushwa

Nauli Unazojulishwa Mapema zinaweza kuwa za juu au chini kuliko bei kulingana na bei za muda uliowekwa na umbali. Kwa nini?

Ili kuunda fursa thabiti zaidi za kujipatia mapato kwa kila mtu katika eneo moja. Tunaangalia masharti baada ya kila sekunde ili kuhakikisha kwamba kila ofa unayopata ni sawa na ile unayokosa.

Mabadiliko yanapotokea

Teknolojia inaweza kutabiri kiasi fulani tu. Wakati msongamano wa magari, ujenzi au muda mrefu wa kusubiri usiotarajiwa unapotokea, utapata marekebisho ya kiotomatiki ya nauli ili kuirekebisha.

Kufuatilia mapato yako

Kuelewa mapato yako kunaweza kukusaidia upange siku yako. App ina nyenzo zinazoweza kukusaidia kufuatilia mapato yako, kuona jumla katika muda halisi, kupata maelezo kuhusu safari mahususi, kulinganisha mapato kwa wiki na zaidi.

Utaratibu wa kuhesabu nauli

Utapata mapato kulingana na muda na umbali wa kila safari.

  • Nauli ya kawaida ya safari

    Nauli ya kawaida inategemea muda na umbali kwa kila safari.

  • Ongezeko la Nauli

    Angalia ramani ya rangi kwenye App yako ili ujue wakati na maeneo ambako kuna wasafiri wengi wa Uber, ili utengeneze hela zaidi.

  • Kughairi

    Tunathamini muda wako. Msafiri anapoghairi zaidi ya dakika 5 baada ya kukubali safari ombi lake, utalipwa ada ya kawaida ya kughairi safari au muda na umbali halisi uliotumia kuendesha gari kuelekea eneo la kumchukua, kiasi chochote ambacho kitakuwa zaidi.

  • Ada ya huduma

    Ada hii inatusaidia kulipia huduma kama kuboresha App, usaidizi kwa wateja, na kuchakata malipo.

  • Ada ya kuweka nafasi

    Wasafiri hulipa ada ya kuweka nafasi ili kutuwezesha kugharimia huduma za usalama, usimamizi na gharama za huduma kama vile bima.

1/5

Endesha gari kupitia App