Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi

Huduma bora ya Uber kwa ajili ya biashara yako

Uber for Business hulipa shirika lako udhibiti zaidi, ufahamu wa kina na vipengele vilivyoundwa kwa ajili ya watumiaji wa biashara. Simamia na ufuatilie safari za kikazi, mipango ya milo na kadhalika kwenye dashibodi moja.

Tovuti ya kimataifa iliyojengwa kwenye mtandao mkubwa zaidi wa usafiri ulimwenguni

Punguza gharama kwa hadi asilimia 10 kwa kuboresha uzingatiaji wa kanuni

Wateja wetu walikubali kwamba walipunguza gharama za usafiri wa ardhini na milo.¹ Fuatilia matumizi na upate vidhibiti vya kutekeleza sera.

Fikia malengo ya uendelevu yenye hatua zinazoweza kutekelezwa

Fuatilia uzalishaji wa hewa ya ukaa kwa kila safari kwenye dashibodi ya Uber for Business. Vidokezi hivi vinaweza kukusaidia kuchukua hatua na kutumia machaguo ya usafiri endelevu kama vile Uber Green.²

Toa huduma ya kipekee kwa timu zako

Mbali na utaratibu rahisi wa kulipa na kipaumbele cha usaidizi, wafanyakazi katika miji mahususi wanapata machaguo ya safari kama vile Uber Business Comfort ambayo inaruhusu wafanyakazi wako kufurahia huduma ya usafiri wa starehe.

Tanguliza usalama na ulinzi wa biashara yako

Tunatoa arifa za ziada za ajali ya barabarani kwa watumiaji wa kikazi. Ripoti yetu ya hivi karibuni ya Usalama ya Marekani inaonyesha kwamba asilimia 99.9 ya safari za Uber hukamilika bila kuripotiwa kwa visa vyovyote vya usalama.

Jinsi kampuni zinavyotumia Uber for Business

Anza bila gharama zozote za mapema

Fanya mipango yako ya usafiri na milo iwe mahususi

Weka sera zako mwenyewe, saidia kuhakikisha uzingatiaji wa usafiri na gharama na uweze kuona kila safari na mlo. Unaweza kushirikiana na washirika wakuu wa malipo kwa urahisi bila kulipa ada ya huduma.

Wasajili watu kwa kasi yako mwenyewe

Weka watu binafsi, timu mahususi au shirika lako zima kwa wakati mmoja. Baada ya wafanyakazi wako kualikwa, wanaweza kuweka wasifu wa kazini kwa safari na milo ya kazini kwenye akaunti yao iliyopo ya Uber wanayoijua na kuiamini kwa safari na milo ya kikazi.

Weka vistawishi kwa ajili ya wateja

Tuma vocha za Uber katika mfumo wa kadi za zawadi na vocha kwa ajili ya safari, milo na kadhalika kwa haraka. Unaweza hata kuomba safari kwa niaba ya watu wengine ili kufanya huduma ya usafiri wanayopata iwe rahisi.

Jiunge na zaidi ya kampuni 170,000 zinazofanya kazi pamoja nasi, ikiwemo zaidi ya nusu ya idadi ya kampuni zilizo kwenye Fortune 500

Wateja 9 kati ya 10 wanapendekeza uchague Uber for Business³

Ungependa kupata maelezo zaidi?

Jinsi ya kupunguza uzalishaji wa hewa ya ukaa kwenye usafiri wa kikazi

Marupurupu na faida ambazo wafanyakazi wako wanataka sasa

Kuelekea uendelevu: waandamizi wanajadili juhudi zao za kukomesha uzalishaji wa hewa ya ukaa

Upatikanaji wa huduma na kipengele unaweza kutofautiana kulingana na soko na eneo. Ili upate maelezo zaidi, anzia hapa.

¹Kulingana na zaidi ya wateja 275 wa Uber for Business waliofanyiwa utafiti kote ulimwenguni mwezi Februari mwaka 2023. Wateja walikubali kwamba waliweza kupunguza gharama za usafiri wa ardhini na/au milo kupitia uzingatiaji bora wa kanuni.

²Uber Green inapatikana katika baadhi ya miji pekee. Isitoshe, upatikanaji unaweza kuwa mdogo nje ya maeneo ya biashara ya mji mwanzoni.

³Kulingana na utafiti wa mwezi Novemba mwaka 2021 ulioagizwa na Uber, ambapo wateja 323 wa Uber for Business walijibu swali la “Una uwezekano gani wa kupendekeza Uber for Business kwa mfanyakazi mwenzako au mtu katika mtandao wako wa kikazi?”

Chagua lugha ambayo unapendelea
EnglishKiswahili