Please enable Javascript
Skip to main content

Jinsi ya kulipia ada ya huduma

Ukiona salio hasi (-) kwenye akaunti yako ya Uber, ina maana kwamba unadaiwa ada ya huduma kutokana na hela ulizokusanya kutoka kwa wasafiri waliolipa pesa taslimu (cash).

Utakuwa na siku mbili za kufanya malipo baada ya kupokea ujumbe wa kukutaka ufanye malipo. Tafadhali fuata utaratibu ufuatao unapofanya malipo ya ada yako ya huduma:

M-pesa

  • 1. Fungua App yako ya Uber

  • 2. Fungua Inbox

  • 3. Bonyeza View payment details & Start Now

  • 4. Weka kiasi unachotaka kulipa

  • 5. Chagua M-pesa kama njia ya malipo

  • 6. Weka namba ya M-pesa unayotaka kutumia

  • 7. Thibitisha Malipo

  • 8. Weka pin kisha ubonyeze Send

  • 9. Muamala umekamilika

1/9
1/5
1/3

Tigo

  • 1. Weka kiasi unachotaka kulipa kutumia

  • 2. Chagua Tigo kama njia ya malipo

  • 3. Weka namba ya Tigo Pesa unayotaka

  • 4. Weka pin kisha ubonyeze Send

  • 5. Muamala umekamilika

1/5
1/3
1/2

Lipa ada ya huduma unayodaiwa mara kwa mara na kwa muda ili uendelee kufanya kazi na uepukane na adha ya kufungiwa akaunti yako.

X small

Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara:

  • Uber itakutumia ujumbe muda wa kufanya malipo ukifika, kiasi unachodaiwa, na jinsi ya kufanya malipo. Utatakiwa ufanye malipo ndani ya siku mbili baada ya kupokea ujumbe unaokutaka ulipe ada ya huduma.

  • Malipo huoneshwa papo hapo lakini, baada ya kufanya malipo, inaweza kuchukua hadi saa 48 kabla ya ada unayodaiwa kufutwa.

  • Ili kuwapa madereva uhuru wa namna wanavyolipa, Uber inaruhusu walipe kiasi kisichopungua ukomo fulani ambacho ni kidogo ikilinganishwa na jumla ya ada anayodaiwa. Kiasi cha chini, ni kiasi cha chini kabisa ambacho utatakiwa ulipe ili upunguze ada unayodaiwa. Ukikosa kulipa ada unayodaiwa au kiasi cha chini kinachoruhusiwa unaweza kufungiwa akaunti yako hadi utakapofanya malipo.

  • Hapana, huwezi kulipa zaidi ya ada ya huduma unayodaiwa.

  • Unaweza kulipa kiasi chochote kuanzia kiasi cha chini na hata ada yote ya huduma unayodaiwa.

  • Uber itakutumia ujumbe wenye maelezo ya muda wa kulipa, kiasi unachodaiwa, kiasi cha chini unachoweza kulipa na utaratibu wa kufanya malipo. Utakuwa na siku 2 za kufanya malipo baada ya kupokea ujumbe unaokutaka ulipe ada ya huduma.

  • Kiasi na unacholipa na jumla ya miamala inategemea uendeshaji wako mwenyewe na kiasi cha pesa unachokusanya kwa safari za pesa taslimu.

  • Akaunti yako itafunguliwa tena ukilipa kiasi cha chini, hata hivyo, ina maana kwamba utapata ujumbe mwingine wa kulipa nyingine ndani ya siku chache.

  • Ada unayotakiwa kulipa (yaani ada ya huduma) inategemea idadi ya safari unazofanya, na iwapo wasafari uliobebab walilipa kwa pesa taslimu. Ukifanya safari nyingi za pesa taslimu ikilinganishwa na safari za kadi basi utakuwa na salio hasi kwa hiyo ada utakayolipa itakuwa kubwa.

  • Akaunti yako itafunguliwa mara tu utakapolipa kiasi cha chini uliambiwa katika kulipa ada ya huduma unayodaiwa, hata hivyo, kuna mazingira ambayo inaweza kuchukua hadi saa 48. Hakikisha unalipa ada ya huduma kwa muda ili usipate usumbufu wowote.

  • Muamala huoneshwa kwenye akaunti yako ya Uber papo hapo lakini inaweza kuchukua hadi saa 48 ada ya huduma unayodaiwa kutoweka (hii inaoneshwa kwenye akaunti yako ya benki au makato kufanywa kwenye njia yako ya malipo) baada ya kufanya muamala wako.