Usafiri Salama, nafuu, wa uhakika, muda wowote!

Kampuni ya Uber imerudisha huduma zake nchini Tanzania kuanzia tarehe 18 Januari 2023, tafsiri yake ni kwamba sasa wasafiri wanaopenda bidhaa za Uber wataendelea kufurahia huduma za uhakika na kwa bei nafuu!  Kwa upande wa madereva, kurudishwa kwa huduma za UberX na UberXL ni fursa ambayo wameikosa kwa muda na sasa wataanza kutumia mfumo wa Uber kufanya kazi kwa muda wanaotaka ili kujiingizia kipato.

Tunaipongeza serikali kwa ushirikiano mkubwa ambao imetoa kwa sekta binafsi ikiwa ni juhudi katika kuhakikisha kwamba tunaweza kuendelea kutoa huduma zetu na kutoa mchango chanya kwa madereva, wasafiri na jiji la Dar es Salaam kwa ujumla. 

Tumerudisha huduma za usafiri za UberX na UberXL ambazo sasa wasafiri wanaweza kufurahia wanapofanya safari zao katika jiji la Dar es Salaam kwa gharama nafuu. UberX ni usafiri unaoweza kubeba hadi watu wanne, na Uber XL inafaa kwa safari za hadi watu sita, kwa familia, marafiki au pale msafiri anapokuwa na mizigo mingi. 

Kurudishwa kwa bidhaa za Uber jijini Dar es Salaam kunatoa unafuu kwa wasafiri wengi ambao walipenda huduma za Uber, hasa  vipengele vya usalama vinavyopatikana kwenye mfumo wa Uber kama vile:

  • Kuonesha mwenendo wa safari kwa watu wa karibu maarufu kama Trusted Contacts ili waweze kufuatilia safari.
  • Kufuatilia mwenendo wa safari pale gari linaposimama kwa muda mrefu bila sababu maalum. Kipengele hiki kinaitwa RideCheck

Sambamba na vipengele hivi, kuna kipengele kingine iwapo kutakuwa na dharura yoyote wakati wa safari, kipengele hiki kinapatikana ndani ya app ya Uber na kinatumia kitufe cha Ngao. Wasafiri wanahimizwa kukitumia pale kunapokuwa na dharura yoyote kama vile ajali au tukio linalohatarisha usalama wakati wa safari.

Sasa usafiri katika Jiji la Dar es Salaam umenoga. Jiongeze Download App ya Uber uanze kufurahia usafiri wa kijanja zaidi. 

Tunakupiga tafu ya punguzo la asilimia 40% kwenye safari zako tano (5) utakazofanya ndani ya wiki moja. Tumia kuponi hii hapa: TEAMTZ2023

 

Timu ya Uber,

#UberImerudi