Drive

Vidokezo vyetu vya kuongeza usalama barabarani

January 17, 2018 / Tanzania

Kama dereva-mshirirka, umetembelea kila kona ya mji, umewapeleka wasafiri sehemu mbali mbali, na umeweza kujikimu kimaisha. Iwe unaenda safari ndefu au hata safari fupi ndani ya mji, ukiwa barabarani kwa muda mrefu kuna vitu vy kuzingatia.

Zingatia vidokezo hivi kwa usalama zaidi:

  • Paki gari na kunyoosha miguu yako kila baada ya muda, hata kama hujisikii kujinyoosha.
  • Kuwa makini kuendesha kati ya saa 8 usiku – saa 10 alfajiri, muda huu ndio muda ambao mara nyingi mwili wako hutaka kupumzika (kulala).
  • Kama umechoka usijilazimishe, pumzika maana ukiwa umechoka hata hamu ya kazi inapungua.
  • Kumbuka kujitunza, Kumbuka kula mara kwa mara, kunywa maji ya kutosha, na pumzika unapo hitaji kupumzika.
  • Kuwa makini, hata kama barabara unaijua hakikisha hutoi macho barabarani. Fuatillia alama za barabarani, traffic na fuata sheria za uendeshaji.