Driver Announcements

Anakuletea programu mpya, iliyoundwa kwa kuwahusisha madereva

May 29, 2018 / Tanzania

Tulitangaza mipango ya kuunda upya programu ya Madereva tarehe 10 Aprili, katika hafla maalum ya madereva huko Los Angeles. Mtazame Mkurugenzi Mkuu wa Uber, Dara Khosrowshahi, anakienda jukwaani kushiriki maono yake ya ushirikiano na kutoa maelezo kuhusu mabadiliko haya.

Yuhki Yamashita ni Msimamizi wa Bidhaa za Uber na aliitoa maelezo ya utangulizi kuhusu programu ya Madereva na ufafanuzi kuhusu baadhi ya vipengele vyake vipya.
Harry Campbell, ambaye ni mgeni maalum, pia anayejulikana kama Jamaa wa Safari za Pamoja, alijadiliana na Dara katika kipindi cha Maswali na Majibu kuhusu matumizi ya programu hii mpya.

Tunasonga mbele pamoja

“Tunahitaji kufanya mengi zaidi ya kuunda vipengele na kuangazia kuboresha maisha ya usoni tukiwa pamoja na wewe.”—Dara Khosrowshahi, Mkurugenzi Mkuu wa Uber.

Kwa hivyo, tulipokuwa tukiunda programu mpya ya Madereva, tulijua kuwa hatungefaulu bila ya usaidizi wako. Ili tuelewe mahitaji ya wasafiri wetu kikamilifu, tulijua kuwa tungehitaji kufanya kazi pamoja.

Hivyo, tulishirikiana na madereva na washirika wanaosafirisha mizigo duniani kote ili kuunda, kujaribu na kujenga programu mpya kwa ajili yako.

Matokeo yake ni kuwepo kwa programu bora ya Madereva ambayo imeundwa ili ikusaidie utumie wakati wako vizuri unapotumia Uber.

Kabla na baada ya tukio hili, Dara alikutana na baadhi ya madereva wa Los Angeles ambao walimsaidia kutengeneza na kuijaribu programu hii mpya.


Kuna vitu gani vipya?

Utapata muundo safi na zana zaidi za kukusaidia ufaulu na uendeshe gari bila wasiwasi. Huu ni muhtasari wa vipengele 3 ambavyo tunajua utavipenda:

Fuatilia mapato yako kwa urahisi

Angalia kwenye skrini yako kiasi halisi ambacho umepata kila baada ya safari na ujue jumla ya mapato yako ya kila siku na kila wiki kwa kugusa kitufe tu.

Fuatilia fursa

Ukiwa mtandaoni, utapokea taarifa za wakati halisi kuhusu maeneo yaliyo na wasafiri wengi wanaosubiri kusafiri. Ikiwa utataka kutumia fursa ya kupata safari nyingi, utaongozwa hadi eneo hilo kupitia ramani ya programu.

Endelea kupata taarifa mpya

Unaweza kupata SMS kutoka Uber kuhusu akaunti yako, vipengele vipya vya programu na mengineyo.

Ni nini kitakachofuata?

Vipengele hivi na vinginevyo vitatumika kwa miezi kadhaa ijayo. Hatua ya kukuletea programu mpya huambatana na mabadiliko makubwa. Hivyo, tungependa tuchukue muda wa kutosha ili tufanye mabadiliko yatakayokufaa zaidi. Tutaendelea kukusikiliza na kushirikiana nawe ili tupate maoni na kuboresha huduma tunapoendelea.

Tunajivunia mafanikio tuliyopata pamoja na tuna ari ya kutekeleza mengi siku za usoni.