Ofa

Uzoefu Bora kwa Wateja

Tarehe 18 Aprili, 2017 / Tanzania

Tunatamani kuwa moja wapo ya taasisi ambayo inatoa huduma nzuri na ya kuridhisha katika Afrika Mashariki. Hii ina maana ya kujiwekeza kwa watu wetu na sehemu mbalimbali ili kutoa uzoefu unaoridhisha, katika  muda muafaka na kwa ubora unaofaa. Hii si kwa ajili tu ya watu wanaotumia usafiri wa Uber bali hata kwa madereva washirika wetu ambao wamechagua kuitumia Uber kama fursa ya kutengeneza kipato.

Mwezi huu, tunazindua ofisi zetu mpya, zenye nafasi ya kutosha Kampala, Nairobi na Dar es Salaam. Hizi ofisi tunaziita Greenlight Hubs na ni kwa ajili ya madereva washirika ambao watakaotutembelea kwa ajili ya kuuliza maswali watakayokuwa nayo, ikiwa ni pamoja na usaidizi wowote katika kuwezesha akaunti zao kuwa hewani ili kufanya kazi.

Endelea kufuatilia upate kuona picha za ofisi zetu mpya ambazo tunayo furaha sana kuhamia.