
Sasa unaweza kutumia App ya Uber kufanya delivery ya bidhaa/mizigo kwa ajili yako, rafiki zako au hata kwa ajili ya wateja wako. Ni rahisi sana kutumia huduma hii;
UberConnect ni nini?
UberConnect ni huduma ya kusafirisha mizigo/bidhaa zako binafsi na hata za kibiashara. Sasa unaweza kufanya delivery ya vitu vyako kwa urahisi, usalama, uhakika na kwa gharama nafuu zaidi kupitia App ya Uber.
Huduma hii itaanza rasmi tarehe 17/05/2021 na madereva wetu wa UberBODA ndio watakaokuwa wakisafirisha bidhaa hizi kwa kutumia boda boda zao, na hivyo kufanya bei za usafirishaji kuwa sawa sawa sawa na bei ya sasa ya huduma ya UberBODA.
Base fare | TZS 700 |
Kwa kilometa | TZS 250 |
Kwa dakika | TZS 55 |
Nauli ya chini | TZS 1000 |
Jinsi inavyofanya kazi
- Fungua App ya abiria ya Uber.
- Chagua huduma ya Connect ndani ya app ya Uber, kubali vigezo na masharti, thibitisha kwamba mzigo wako hauna bidhaa zilizopigwa marufuku, na uite usafiri.
- Jibu ujumbe utakaopokea kwenye app ya Uber utakaokuomba uweke jina la mpokeaji sambamba na maelekezo mengine yoyote ambayo ungependa kumwambia dereva wako.
- Kutana na dereva na umkabidhi mzigo ambao unataka usafirishwe.
- Share safari na mtu unaetaka kumpelekea mzigo ili na yeye aweze kuifuatilia mzigo wake.
Mizigo inayosafirishwa
Ukomo wa bidhaa zinazosafarishwa kupitia Uber Connect ni kilo 15 na thamani yake isizidi TZS 115,000 na lazima zizingatie sheria na masharti yote ya serikali sambamba na sera za Uber. Ni marufuku, kutuma bidhaa haramu au bidhaa nyingine zilizopigwa marufuku.
Ukituma mzigo wowote unaokiuka sheria yoyote ya nchi au sera zetu, ikiwa ni pamoja na zile zilizoainishwa kwenye ukurasa huu, tutakuchukulia hatua za kinidhamu inavyostahili, ikiwa ni pamoja na kusitisha au kufunga akaunti yako mara moja. Unaweza kuchukuliwa hatua za kisheria kama vile kushtakiwa kwa makosa ya jinai iwapo utatuma mizigo haramu au hatari.
Bidhaa zilizopigwa marufuku ni pamoja zifuatazo;
- Bidhaa haramu.
- Bunduki, silaha, na vipuri vya silaha.
- Pombe, madawa ya kulevya au bidhaa za tumbaku
- Vyakula au vinywaji vinavyoharibika haraka (kama mayai).
- Bidhaa hatari au zenye madhara mabaya, ikiwa ni pamoja na vilipuzi, bidhaa zenye sumu au zinazowaka moto rahisi, uchafu wa hospitali na bidhaa nyingine ambazo zina madhara kama inavyoainishwa na sheria husika.
- Pesa, kadi za zawadi (gift cards), tiketi za kamari au hisa zinazohamishika.
- Vitu/ bidhaa za wizi.
- Vitu ambavyo vinaweza kuvunjika kwa haraka kama glass.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara;
- Ni huduma gani itatumika kusafirisha vitu/bidhaa hizi
- Ni bidhaa gani ambazo mtu anaweza kutuma kupitia uber Connect?
- Je huduma ya Connect inapatikana maeneo mengine nchini Tanzania
- Je, ninaweza kuagiza nikalatewa mzigo
- Ninawezaje kufuatilia mzigo unaosafirishwa
- Nitashare vipi safari ili mwenye mzigo aweze kuifuatilia?