Ofa

Tunapaa angani na UBERCHOPPER! Kwa hisani ya Tigo

Tarehe 13 Desemba, 2018 / Tanzania

Jiandae kwa sababu msimu huu wa krismasi umenoga kweli na utapata huduma ya kipekee kabisa kuwahi kutokea. Wateja wa Tigo wanaweza kujishindia nafasi ya kusafiri kijanja zaidi na kufurahia mandhari ya jiji la Dar es Salaam kupitia huduma ya UBERCHOPPER ya siku moja tu!

Ijumaa tarehe 14 Disemba 2018 kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 5:00 mchana, unaweza kuita usafiri wa uberCHOPPER. Kumbuka kwamba huhitaji bando ndio uite usafiri – wateja wote wa Tigo hawahitaji kuwa na bando wanapotumia Uber, tafsiri yake ni kwamba unaweza kuita usafiri hata kama huna bando lolote ili muradi unatumia mtandao wa Tigo.

Jinsi ya kushiriki:

  • Hakikisha unafungua app yako ya Uber kati ya saa 3:00 asubuhi – 5:00 mchana Ijumaa tarehe 14 Disemba 2018.
  • Telezesha upande wa kushoto kwenye bango la UBERCHOPPER lililopo upande wa chini wa skrini ya app yako ya Uber.
  • Hakikisha umeweka eneo sahihi la kuchukuliwa kwenye app.
  • Bonyeza kwenye “thibitisha UBERCHOPPER”.

Ukibahatika na ufanikiwe kuita usafiri, gari la Uber litakuja kukuchukua likupeleke hadi Sea Cliff Resort, ambapo safari yako ya uberCHOPPER itaanzia.

Uhitaji wa huduma hii utakuwa mkubwa, kwa hiyo usikate tamaa na hakikisha unajaribu tena iwapo hutabahatika kwa mara ya kwanza.

Wateja wa Tigo wanaotumia usafiri wa Uber wana nafasi ya kujishindia safari ya ndege iwapo utatumia huduma zozote za Tigo wiki hii na ushiriki kwenye Jigiftishe na Tigo promotion kabla ya tarehe 12 Disemba 2018

  • Vigezo na Masharti