
Jiandae kwa sababu msimu huu wa krismasi umenoga kweli na utapata huduma ya kipekee kabisa kuwahi kutokea. Wateja wa Tigo wanaweza kujishindia nafasi ya kusafiri kijanja zaidi na kufurahia mandhari ya jiji la Dar es Salaam kupitia huduma ya UBERCHOPPER ya siku moja tu!
Ijumaa tarehe 14 Disemba 2018 kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 5:00 mchana, unaweza kuita usafiri wa uberCHOPPER. Kumbuka kwamba huhitaji bando ndio uite usafiri – wateja wote wa Tigo hawahitaji kuwa na bando wanapotumia Uber, tafsiri yake ni kwamba unaweza kuita usafiri hata kama huna bando lolote ili muradi unatumia mtandao wa Tigo.
Jinsi ya kushiriki:
- Hakikisha unafungua app yako ya Uber kati ya saa 3:00 asubuhi – 5:00 mchana Ijumaa tarehe 14 Disemba 2018.
- Telezesha upande wa kushoto kwenye bango la UBERCHOPPER lililopo upande wa chini wa skrini ya app yako ya Uber.
- Hakikisha umeweka eneo sahihi la kuchukuliwa kwenye app.
- Bonyeza kwenye “thibitisha UBERCHOPPER”.
Ukibahatika na ufanikiwe kuita usafiri, gari la Uber litakuja kukuchukua likupeleke hadi Sea Cliff Resort, ambapo safari yako ya uberCHOPPER itaanzia.
Uhitaji wa huduma hii utakuwa mkubwa, kwa hiyo usikate tamaa na hakikisha unajaribu tena iwapo hutabahatika kwa mara ya kwanza.
Wateja wa Tigo wanaotumia usafiri wa Uber wana nafasi ya kujishindia safari ya ndege iwapo utatumia huduma zozote za Tigo wiki hii na ushiriki kwenye Jigiftishe na Tigo promotion kabla ya tarehe 12 Disemba 2018
Posted by Uber Editor
Get a trip when you need one
Start earning in your city
Get a trip when you need one
Start earning in your city
Related articles
Most popular
Shinda Vocha za KFC na PizzaHut ukitumia App ya Uber
Pata 10% ya nauli yako ukilipia safari za Uber kwa TigoPesa!

Heshima ni kwa pande zote mbili
