
Dereva-mshirika anavyojiunga na Uber, anakuja kwa nia ya kufanya kazi ambayo itaendana na ratiba zake. Kwa sababu ya hili,tunataka ufurahie kuwa dereva-mshirika wa Uber
Tunapenda kukufahamisha kwamba kutakuwa na mabadiliko mazuri sana hizi wiki chache zijazo! Mabadiliko haya sio ya kuongeza vitu kwenye programu yako ya dereva-mshirika bali ya kukurahisishia wewe ufanyaji wako wa kazi, na kufanya ufurahie kuwa dereva-mshirika wa Uber.
Nini kimeongezeka?

Taarifa ya safari ndefu
Sasa utaarifiwa kama safari ni ndefu kabla ya kukubali ombi la safari, ili uweze kuamua kama utaikubali hiyo safari au la, hamna tena kushtukizwa!

Utalipwa wakati wa kumsubiria msafiri
Ikipita dakika tano baada ya kufika eneo la kumchukua msafiri, msafiri atalipishwa kwa kila dakika ambayo utakuwa unamsubiria ili kuanzisha safari. Hii itawafanya wasafiri waombe safari pale ambapo watataka kuondoka.

Tathmini ya nyota
Kuanzia sasa tathmini ya nyota zako haitabadilika kutokana na mambo yaliyo juu ya uwezo wako, kama msafiri akitoa maoni ambayo hayaendani na huduma za dereva-mshirika tathmini ya nyota zako haitabadilika.

Uwezo wa kushare taarifa za safari
Kama wasafiri wanavyoweza kushare taarifa za zafari zao kwa marafiki, wewe pia kama dereva-mshirika unaweza kushare taarifa za safari zako kwa marafiki zako

Muda wa kuwasili kwenye eneo unalotaka kwenda
Hii sio mwisho, bado tunayakusanya maoni yenu, na kufikiria ni kwa jinsi gani tunaweza kuzidi kuboresha huduma hii.
Posted by Uber Editor
Get a trip when you need one
Start earning in your city
Get a trip when you need one
Start earning in your city
Related articles
Most popular
Shinda Vocha za KFC na PizzaHut ukitumia App ya Uber
Pata 10% ya nauli yako ukilipia safari za Uber kwa TigoPesa!

Heshima ni kwa pande zote mbili
