Bidhaa

Technology features to help keep our roads safer

Tarehe 10 Mei, 2019 / Tanzania

Kwa heshima ya wiki ya usalama barabarani ya Umoja wa Kimataifa, tunajiunga na jamii ya usalama duniani kupaza sauti na kuongeza ufahamu juu ya athali za uendeshaji usio salama.

Shirika la Afya Duniani linasema kwamba kasi isiyofaa ni sababu kuu ya ajali barabarani, vifo na majeruhi. Uendeshaji wa kasi unaongeza uwezekano wa kupata ajali barabarani. Ni ngumu zaidi kwa vyombo vya moto kusimama au kufata mabadiliko barabarani vikiwa kwenye mwendo wa kasi, hivyo kusafiri kwa kasi inayofaa kunaweza kusaidia madereva kuepuka ajali.

Iwe ni kufunga mkanda au kuendesha kwenye kikomo cha kasi iliyowekwa, wote tunaweza kuchangia kufanya barabara zetu kuwa salama. Hapa Uber, mara kwa mara tunaunda mifumo na huduma  mbalimbali ili kuongeza uwazi,uwajibikaji na amani kwa watu wote wanaotumia app ya Uber. Jua zaidi hapa chini!

Tahadhari ya kasi

Tahadhari ya kasi ndani ya app inasaidia kuwakumbusha madereva kuendesha katika kikomo cha kasi kilichowekwa. Wataalamu wanasema kwamba kuwajulisha watu ni kwa kasi gani wanaendesha inaweza kusaidia kuendesha katika kasi yenye usalama na Uber imeweka kipengele hiki kwenye app na juu ya ramani! Madereva huonyeshwa kasi wanayoendesha  ikilinganishwa na kikomo cha kasi kilichowekwa, hii imethibitishwa na utafiti wa ndani kuwa imesaidia kutuweka sote salama barabarani.

Kikomo cha masaa ya kuendesha gari

Kikomo cha masaa ya kuendesha gari husaidia  madereva kufuatilia muda wawo, ambavyo tunaamini hii husaidia kufanya barabara zetu kuwa salama kwa dereva na abiria. Kipengele hiki huweka kikomo cha masaa unayoweza kuendesha kwenye Uber kabla ya kupumzika. App itakujulisha muda wa kupumzika baada ya masaa 12 ya kuendesha gari, na kisha utabidi uwe nje ya mtandao kwa muda wa masaa 6 kabla hujaruhusiwa kurudi mtandaoni. Baada ya kurudi mtandaoni utaweza kupokea maombi ya safari tena.

Hizi ni baadhi tu ya njia tunazotumia teknolojia kuboresha usalama na kusaidia madereva kutunza magari yao ili kuongeza usalama kwao na kwa abiria pia.