Ofa

Mabadiliko ya nauli ya UberX jijini Dar Es Salaam

Tarehe 2 Aprili, 2019 / Tanzania

Dhamira ya Uber ni kutoa usafiri salama, wa uhakika na kwa bei nzuri wakati wowote. Tunajali maslahi ya wasafiri sambamba na na madereva washirika na tuna juhudi endelevu za kuleta mabadiliko yatakayowafaidi wasafiri kadhalika madereva.

Septemba mwaka jana tulipunguza nauli ya UberX kwa asilimia 40% ili kuwapa wasafiri wanaotumia huduma ya UberX usafiri wa bei wanaoweza kuimudu. Ingawa tunafanya kila juhudi kuhakikisha bei zetu si ghali, ni muhimu kuzingatia uhalisia wa kupanda kwa gharama ya maisha kwa upande wa madereva-washirika. Ukizingatia hili, tumeongeza nauli za UberX jijini Dar Es Salaam kuanzia tarehe 3 Aprili, 2019. Hatua hii inakuja baada ya kufanya tathmini ya kina ya mapato ili kuhakikisha kwamba kipato cha madereva wanaotumia app ya Uber kinakidhi mahitaji yao ya kila siku, sambamba na kutoa usafiri wa bei nafuu kwa wasafiri wanaotumia Uber.

Tuna amini sana katika kuweka kudumisha uwazi tunapofanyia bei zetu mabadiliko yoyote na ni muhimu sana kwamba bado tunasalia kuwa usafiri wa bei nafuu katika jiji hili, bila ya msafiri kugharamika zaidi.

Bei Mpya

Huduma

Nauli ya Zamani

Nauli Mpya

Nauli Msingi

TZS 900

TZS 1000

Kwa kila Kilomita

TZS 350

TZS 400

Kwa kila Dakika

TZS 60

TZS 72

Kutekelezwa kwa nauli mpya kuna maana kwamba tuongeza uwekezaji kwenye teknolojia ya Uber ya sasa – kupitia maboresho tuliyofanya hivi karibuni ili kulinda usalama wako unapokuwa barabarani.

Nauli hii mpya ina athari gani kwa madereva?

Kupitia mabadiliko ya nauli tuliyofanya, sasa madereva-washirika watapata pesa zaidi kwa kuendesha gari. Nia yetu ni kuona madereva-washirika, wanaotumia App ya Uber kuendesha gari, wanapata kipato kinachokidhi mahitaji yao ya kila siku. Kwa hiyo, nauli hii mpya itawawezesha madereva-washirika kupata pesa zitakazowasaidia kulipia gharama za kuendeshea biashara yao na mahitaji yao ya kila siku.

Nauli hii mpya ina athari gani kwa wasafiri?

Kwa upande wa wasafiri, nauli hii mpya tuliyoweka ina maana kwamba tutaongeza uwekezaji kwenye teknolojia tunayotumia ili kuboresha huduma za Uber na kuimarisha mifumo yetu. Zana mpya za usalama zilizoongezwa kwenye app ya Uber zinakusaidia kuwasiliana na ndugu wa karibu na kukulinda ili ufurahie kila safari bila kuwa na wasiwasi wowote barabarani. Tumeanzisha bima ya kumkinga msafiri sambamba na zana ya kukusaidia kuwasiliana na ndugu wa karibu – tumejitolea kulinda usalama wako kuanzia pale unapochukuliwa na gari hadi mwisho wa safari yako.

Bei zetu bado ni nafuu, na tunajiaminisha kutoa huduma za ubora wa juu kwa kila mkaaji wa jiji la Dar Es Salaam. Tunashirikiana kutoa usafiri katika jiji lako.