
Tunapenda kuona ukifurahia huduma ya Uber, na katika kuhakikisha hilo tumekutengenezea vidokezo vya kufanya maisha yako yawe marahisi wakati wowote pale unapotumia Uber; Kuanzia kwenye kupakua app mpaka kuwasiliana na huduma kwa wateja.
Kupakua app
Kupakua app ya Uber ni rahisi sana! Tembelea ‘Playstore’ kwa Android na ‘App store’ kama unatumia IOS, andika ‘Uber’ na uchague app ya juu kabisa.
Hakikisha unawasha location kwenye settings za simu yako ili uweze kuomba usafiri.
Kujisajili
Ili kupata huduma ya Uber ni muhimu kujisali, na haichukui hata dakika. Ili kujisajili fuata hatua hizi;
- Andika namba yako ya simu ( hakikisha ni namba ambayo inapatikana. Hakikisha unapoandika namba inaanza na (+255) )
- Andika Jina lako la kwanza na la mwisho
Kuomba Usafiri
Wakati wa kuomba safari, Uber hukutafutia dereva ambae yupo karibu yako. Ili kufanikisha upatikanaji wa dereva aliye karibu, hakikisha umewasha location kwenye settings za simu yako halafu fuata hatua hizi;
- Andika unapoelekea
- Chagua aina ya usafiri
- UberPOA kwa bajaji
- UberX kwa magari ya kawaida (mpaka watu wanne)
- UberXL kwa magari makubwa (mpaka watu 6 mpaka 7)
- Hakikisha eneo la kuchukuliwa, baada ya hapo utaunganishwa na dereva aliye karibu nawe.
- Hakikisha umeangalia nauli yako na umekubaliana nayo kabla ya kupanda usafiri.
Huduma kwa wateja
Huduma yetu kwa wateja hupatikana ndani ya app yako ya Uber. Ili kuwasiliana na huduma kwa wateja, fuata hatua hizi;
- Fungua app yako
- Bonyeza ‘Menu’ (Mistari mitatu – kushoto juu ya app yako)
- Bonyeza ‘help’, na utaona sehemu ya kuripoti tatizo lolote kuhusiana na safari zako za Uber
Ni rahisi sana kutumia App ya Uber, Popote pale ndani ya Dar ES Salaam tutakufikisha. #UberMovingTanzania.
Posted by Uber Editor
Get a trip when you need one
Start earning in your city
Get a trip when you need one
Start earning in your city
Related articles
Most popular
Shinda Vocha za KFC na PizzaHut ukitumia App ya Uber
Pata 10% ya nauli yako ukilipia safari za Uber kwa TigoPesa!

Heshima ni kwa pande zote mbili
