Ofa

Bei imeshuka kwa 40% kwenye safari za uberX jijini Dar es Salaam!

Tarehe 25 Septemba, 2018 / Tanzania

Dhamira yetu ni kutoa usafiri salama, wa uhakika na nauli nafuu kwa kila mtu mahali popote pale. Ndio maana tumepunguza nauli za safari za uberX kwa 40% jijini Dar es Salaam, hii ina maana kwamba sasa utaweza kufanya safari zako kwa nauli nafuu zaidi!

Ubora wa huduma zetu umeimarika zaidi na utarajie  usafiri mzuri kutoka kwetu, kuanzia pale unapoita usafiri mpaka ufike mahali unakoenda. Kwa kuwa nauli za uberX sasa zinaanzia TZS 4,000 pekee, una kila sababu ya kusafiri!

Kielelezo cha nauli:

 

Nauli ya zamani (TZS)

Nauli mpya (TZS)

Posta hadi Mwenge

13,000

7000

Posta hadi Ubungo

16,000

9,000

Mwenge hadiTegeta

16,000

9,000

Nauli ni nafuu sana na isitoshe unaweza kutumia app ya Uber bure kupitia mtandao wa Tigo, una kila sababu ya kutumia huduma zetu – unachotakiwa kufanya ni kubonyeza tu na utapata usafiri wa nauli nafuu!