Habari

Asante Africa kwa miaka 4!

Tarehe 26 Septemba, 2017 / Tanzania

Hii ni kwa waafrika wote! Tumekuwa tukiwasafirisha kwa miaka minne sasa, na imekua ni furaha kubwa sana kwetu kupata nafasi hii.

Ilianza kwa kubonyeza kitufe na kupata usafiri, sasa imekua kitu kikubwa sana- Kuanzia kwenye kutembelea miji mikubwa, kukufikisha uendapo kwa wakati na maelfu ya kazi zilizopatikana kupitia Uber. Mmekua nasi katika kila hatua, na tusingefikia hapa bila nyie!

Tuangalie ni wapi tumetoka, na kikubwa zaidi ni wapi tunapoelekea.

Safari ndio kwanza inaanza! #UberMovesAfrica